Barabara ya Darajani Visiwani Zanzibar. Askari wa kutuliza ghasia wameshaanza
kurusha mabomu ya machozi kutawanya kundi la uamsho ambao wapo Barabara ya
Darajani wanachoma matairi na kurusha mawe kwa askari. Fujo hizo zimetokana na
kukamatwa kwa kiongozi wa Uamsho Sheikh Farid.
Huyu ndiye Kiongozi
wa Kundi linaloitwa UAMSHO la Zanzibar Sheikh Farid aliyekamatwa huko Visiwani
Zanzibar. Kundi hilo shughuli zake ni za mihadhara ya Kidini hasa ya Kiislam.
|
EmoticonEmoticon