Sheikh Farid Hadi Ahmed
mmoja kati ya viongozi wa ngazi za juu wa UAMSHO visiwani Zanzibar
nchini Tanzania ameachiliwa huru jana
usiku, baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi la nchi hiyo kwa muda wa siku
tatu.
Taarifa kutoka Zanzibar zinasema kuwa, Sheikh Farid Hadi Ahmed
amethibitisha mwenyewe wakati
alipowaambia waandishi wa habari jana usiku kwamba,
askari kadhaa wa jeshi la polisi ndiyo waliomkamata siku ya Jumatano
usiku, na kumpeleka mahala asipopajua kwa mahojiano.
Wakati jeshi la polisi
likiendelea kumhoji kwa siri kiongozi huyo wa UAMSHO, Mussa Ali Mussa Kamishna wa Polisi Zanzibar
aliviambia vyombo vya habari kuwa, jeshi
hilo halifahamu mahali alipo kiongozi huyo, na kwamba litaendelea na zoezi la
kumtafuta.
Kutoonekana kwa Sheikh Farid Hadi kulipelekea kuibuka ghasia na
vurugu mjini Zanzibar, na
kusababisha askari mmoja wa jeshi
la polisi kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Hapo jana baada ya
mshuko wa sala ya Ijumaa, askari polisi walipambana na Waislamu wenye
hasira katika maeneo ya Mji Mkongwe Town
wakilalamikia kutoonekana kwa kiongozi wao.
EmoticonEmoticon