Ripoti iliyotolewa na gazeti la Daily Mail linalochapishwa nchini Uingereza
imeeleza kwamba dikteta wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi aliuliwa na ajenti
wa siri wa Ufaransa kwa amri ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nicolas Sarkozy.
Inasemekana kuwa jasusi huyo wa Ufaransa alijipenyeza kwenye kundi moja la
vikosi vya wanamapinduzi wa Libya lililomkamata mateka Gaddafi kwenye bomba la
majitaka katika mji alikozaliwa wa Sirte na kumpiga risasi.
Likizinukuu duru za
Libya Daily Mail limeandika kuwa ajenti huyo wa Ufaransa aliamriwa na Rais wa
zamani wa nchi hiyo Nicholas Sarkozy kumuua Gaddafi ili kumzuia asije akafichua
mahusiano yake na Sarkozy endapo angesailiwa. Kabla ya kuuawa na kufuatia
mashambulio ya anga yaliyofanywa na shirika la kijeshi la NATO nchini Libya,
Muammar Gaddafi alitishia hadharani kwamba angefichua kwa undani uhusiano wake
na rais huyo wa zamani wa Ufaransa.
Sarkozy, ambaye aliwahi kumwita dikteta wa zamani
wa Libya 'kiongozi ndugu' wakati alipofanya safari nchini Ufaransa anasemekana
kuwa alipokea kutoka kwa Gaddafi kitita cha yuro milioni 50 kusaidia kampeni
zake za uchaguzi wa rais wa mwaka 2007.
Gazeti la Kitaliana la Corriere della
Serra nalo pia limeripoti kuwa duru za Libya zimeeleza kwamba muuaji wa kigeni
mwenye uraia wa Ufaransa ndiye aliyemuua Gaddafi
EmoticonEmoticon