Mufti Mkuu Nchini, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba |
Kwa Mujibu wa Taarifa Zilizotufikia Hivi Punde, Ni kwamba Waumini wa Dhebu la Kiislama Wilayani TUNDURU, MKOANI RUVUMA, wameshinikiza Kutengana na Dhehebu la Kikiristo Katika Wilaya Hiyo.
Tarifa za Uhakika kupitia Mwanahabari wa Kituo cha Redio cha WAPO RADIO FM cha jijini Dar es Salaam Zinaeleza kuwa, Shinikizo hilo limeleta hali ya Wasi wasi kwa Wakazi wa Dhehebu la Kikristo Wilayani Tunduru, huku wakihisi kuwa huenda hali hiyo Ikaleta Mgogoro Mkubwa wa Kidini Baina yao.
HALI HALISI.
Taarifa Zinaeleza Kuwa, katka Matukio mbali mbali ya kushinikiza Utengano Huo, Waislaam Hao wamekuwa wakionesha Matukio mbali mbali ya Kiudharirishaji katika Mihadhara yao wanayoifanya.
Moja ya Matukio Hayo, ni Kuigiza namna ambavyo Wachungaji mabli mbali wanavyowaombea Waumini wao huku wakianguka chini kama Watu wenye Mapepo.
Licha ya Hali hiyo kuonesha Udharirishaji, baadhi ya Wakristo wameelezea kuwa huenda hali hiyo ikaanzisha Mgogoro wa Kidini wilayani Humo.
MASHINIKIZO YA KUNDI HILO LA KIISLAAM HAO.........
Kundi hilo la Waislaam katika Wilaya hiyo ya TUNDURU, linawashinikiza Waislaam Wenzao Kutengana Kabisa na Wakristo katika Hali zifuatazo.
- Kuahama Makazi ambayo yanamilikiwa na Wakristo (Ikiwa Waislam ni Wapangaji)
- Kuwaondoa Wakristo ambao watakuwa Wamepanaga katika Makazi ya Waislaam
- Kuvunja Ndoa iwapo Muislaam atakuwa ameolewa au kumuoa Mkristo.
- Kutengana na Waumini wa Kikristo Kabisa.
Tunduru, Ruvuma |
CHANZO CHA HAYO YOTE.
Chanzo cha Mashinikizo hayo kutoka Katika Kundi hilo la Kiislaam bado hakijabainika Rasmi
Baadhi ya Waumini wa Dhehebu la Kiislaam Jijini Dar es Salaam wakiwa Katika Ibaada Takatifu |
VYOMBO VYA USALAMA NA SERIKALI NZIMA......................
Aidha kwa Mujibu wa Taarifa kutoka kwa Mwanahabari huyo, ni kwamba Vyombo vya Usalama Wilayani humo bado havijachukua Uamuzi wowote ule wa Kisheria....jambo ambalo huenda Wakristo wakaamua Kujibu Mapigo
EmoticonEmoticon