Nchi za kiarabu zimemtolea wito rais wa Syria Bashar al-Assad kuachia madaraka mara moja ili kumaliza mgogoro
wenye umwagaji damu ambao unaendelea nchini mwake.
Akizungumza muda mchache uliopita baada ya mkutano wa
mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Doha, Qatar,
waziri mkuu wa nchi hiyo Sheikh Hamad bin Khalifa al-Thani, amesema mkutano huo unamtaka Assad kuchukua
kile alichokiita uamuzi wa kishujaa ili kuinusuru Syria na
umwagaji damu zaidi.
Sheikh Hamad amesema kwamba Jumuiya ya Nchi za
Kiarabu imewataka waasi wanaojulikana kama jeshi huru la
Syria kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa, na kupendekeza
kumpa mpatanishi wa kimataifa katika mgogoro wa Syria
Kofi Annan, jukumu la kutunga sera ya serikali hiyo.
Rais Wa Syiria Bashar Al Asad |
Hayo yanaarifiwa wakati nchini Syria kwenyewe mapigano
makali yakiendelea kati ya jeshi la serikali na waasi,
ambapo watu zaidi ya 120 waliripotiwa kuuawa jana
Jumapili. Mkutano wa Doha pia umeahidi msaada wa nchi
za kiarabu wa dola milioni 100 kusaidia wakimbizi wa Syria.
Baadhi Ya Mauaji yanayofanyika Syria |
EmoticonEmoticon