Mahakama nchini Afrika ya Kusini imemtia hatiani kiongozi wa kundi lenye itikadi kali za ubaguzi wa rangi la Boer Army ya kutaka kuipindua serikali iliyokuwa inaongozwa na Rais wa zamani Nelson Mandela mwaka 2002.
Nelson Mandela |
Kiongozi huyo aliyekuwa mhadhiri wa chuo kikuu nchini humo Mike du Toit, alipanga kumuua Mandela kwa mashambulizi ya mabomu kisha aungóe madarakani utawala wa watu weusi. Kesi hiyo imedumu kwa miaka tisa. Hukumu yake inatarajiwa kutolewa mwezi ujao na huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha jela.
Wafuasi wengine 21 wa kundi hilo hukumu zao zitatolewa wiki chache zijazo. Jaji Eben Jordan aliyeendesha kesi hiyo amesema kuwa mashahidi wameeleza namna kundi hilo lilivyopanga kufanya mauwaji hayo. Lilipanga pia kuwaua kwa risasi raia weupe wa nchi hiyo wanaounga mkono utawala wa watu weusi.
EmoticonEmoticon