Mgonjwa Wa Ebola |
Rais Wa Uganda, Yoweri Kagutta Museveni |
Na Frank M. Joachim
Watu sita zaidi wamelazwa hospitalini kwa kushukiwa kuwa wameambukizwa virusi hatari vya Ebola Magharibi mwa Uganda. Ugonjwa huo hatari ulizuka wiki tatu zilizopita. Inaripotiwa kuwa vijiji vingi katika eneo hilo sasa vimeathirika. Wizara ya Afya ya Uganda na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO zilithibitisha mwishoni mwa wiki kuwa virusi hivyo vimewaua watu 14 mwezi huu. Rais wa Uganda Yoweri Museveni jana pia alithibitisha kupitia vyombo vya habari kuwepo ugonjwa huo na kuwataka watu kuepuka kugusana ili kuepukana na hatari ya kuambukizwa. Hakujakuwa na visa vilivyothibitishwa vya maambukizi kuenea katika mji mkuu Kampala. Uganda imewahi kukumbwa na matukio matatu ya kuzuka ugonjwa wa Ebola katika kipindi cha miaka 12 iliyopita. Kisa kibaya zaidi kilikuwa mnamo mwaka wa 2000 ambapo watu 425 waliambukizwa. Zaidi ya nusu yao waliaga dunia. Hakuna chanjo ya kuzuia ugonjwa huo kufikia sasa.
EmoticonEmoticon