CHANZO: BBC (PICHA ZOTE NA DAILY MAIL)
Ndege ya shirika moja la ndege la Urusi,
iliyowabeba abiria zaidi ya 200, imeanguka katika eneo la Sinai nchini Misri,
afisi ya waziri mkuu wa Misri imethibitisha.
Ndege hiyo aina ya Airbus A-321 ilikuwa imetoka
mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St Petersburg nchini Urusi ilipoanguka.
Vyombo vya habari nchini Misri vinasema ambaki
ya ndege hiyo yamepatikana na ambiulensi zaidi ya 20 zimetumwa eneo la ajali.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametuma risala za
rambirambi kwa jamaa za waathiriwa na kuagiza uchunguzi ufanywe.
Awali, kulikuwepo na utata kuhusu hatima ya
ndege hiyo, baadhi ya ripoti zikisema ilitoweka karibu na visiwa vya Cyprus.
Lakini afisi ya Waziri Mkuu wa Misri Sharif Ismail imethibitisha kwamba ndege
hiyo ilianguka katikati mwa eneo la Sinai.
Afisi hiyo imeongeza kuwa Bw Islmail ameunda
kamati ya dharura ya kushughulikia ajali hiyo.
Wengi wa abiria walio kwenye ndege hiyo ni
watalii kutoka Urusi.
Ndege hiyo ni ya shirika la ndege la
Kogalymavia. Ripoti za karibuni zinasema ilikuwa imewabeba abiria 217 na
wahudumu saba.
Instagram @babajuti