BUNGENI: NAY WA MITEGO, SHILOLE WAMEZUNGUMZIWA TENA BUNGENI


DODOMA, Tanzania
Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo, imetolea ufafanuzi hatua ambazo zinaendelea katika Tukio la Kutokea kwa Vitendo visivyo na Maadili katika Kumbi na Maonesho mbali mbali ya Starehe.


Ufafanuzi huo umetolewa Mapema Leo Hii Bungeni, katika Kikao cha 25, cha Mkutano wa 15 wa Bunge la 10 La Bajeti Linaloendelea Hivi sasa, baada ya Mheshimiwa Catherine  Magige kuhitaji Ufafanuzi kutoka Wizara Husika, ambapo Majibu yalitolewa na Naibu Waziri, 
Mheshimiwa Juma Nkamia

Katika kutoa Ufafanuzi zaidi, Mheshimiwa Nkamia ametoa Mfano kuwa, moja kati ya watu ambao wamepewa Onyo ni pamoja na wasanii kama Vile NAY WA MITEGO, SNURA na SHILOLE, huku Mashindano ya MISS UTALII yakifungiwa

Related Posts :