DONGO KWA T.I !!!! : WENDY WILLIAMS NAYE KAJIBU PIGO......
Na Baba Juti
#WatuWaMungu mnakumbuka Vizuri kile ambacho tulikuambia kuhusu WENDY WILLIAM, moja kati ya watangazaji anayemiliki Kipindi chake kinachoitwa WENDY WILLIAM'S SHOW, baada ya kuonekana kwa Picha yake akiwa Ufukweni na BIKINI?
Yah !!!
Wengi walianza kuongea kuhusiana na Umbile lake ambalo halina Mvuto hata kidogo, huku baadhi wakisema kuwa Umbile lake ni kama herufi kubwa ya P, kitu ambacho kiliamsha Hisia zake pia.
Mtu ambaye alikuwa ni Miongoni mwa watu waliorusha Dongo kutokana na Umbile hilo, ni Rapper T.I ambaye pia aliwahi kukandiwa na Wendy Williams mara kadhaa
WENDY KAMJIBU T.I
Katika Mfululizo wa Kipindi chake, Wendy Williams aliamua kumtolea Uvivu Pia T.I ingawa alikubali kweli ana Umbo kama Hilo ambalo wengi wamelisema
Wendy aliongeza kuwa, Sio kwamba anashindwa Kuweka Makalio bandia naye akawa na Kalio kubwa, ila hapendi kufanya hivyo sababu ameridhika, na alijiachia vile sababu anaamini hana dhambi juu ya mwili wake
Lakini kuhusu T.I, alisema ni kweli, T.I karusha dongo kwa Kuandika Post ambayo ilijiweka wazi na alisema kabisa kuwa kaandika ama kurusha Dongo kwa njia ya USTAARABU, ila mbona na yeye ni MFUPI na ndio maana anavaa Viatu vikubwa ili apate Kuonekana ni Mrefu?
HAIWEZEKANI !!!!!! : MARIAH CAREY HAWEZI TENA KUIMBA?
Na Baba Juti
#WatuWaMungu ifikie Muda tukubali tu kabisa kuwa yametushinda kabisa maana ni kama tunavyolazimisha ni kama tunaharibu tu
MARIAH CAREY, amethibitisha hilo baada ya kuonekana kabisa kuwa Muziki unaanza kumtupa Mkono baada ya kuonekana aki-lip sync katika perfomance ya Hip Hop HonorsTukio hilo lilifanyika wakati akiimba na Jermain Dupri kupitia Mkwaju wa HONEY.
Wengi awali hawakuwa wamegundua kama Bibie huyo alikuwa akichezesha Lips zake tu kuigiza kuwa anaimba, lakini kumbe wajanja walikuwa wameshagundua hilo na kuanza kuamsha hapo hapo japo kwa Uchache
Tofauti na hilo, Mariah Carey aliwahi kukutana na janga kama hilo la ku-chezesha Mdomo juu ya wimbo, huku baadhi wakidai kuwa hata sauti yake haina Ubora kama ilivyokuwa awali.


