Hebu muone huyu Mpuuzi asivyo na akili. Kama Mimi ni hakimu, Ninamhukumu kwa Makosa Manne Huyu Jamaa
1. Kuwadhalilisha Wanawake
Kwani kaambiwa wanawake wanakasoro mpaka amfuate huyu Mbuzi?
2. Kuwadhalilisha Wanaume.
Hii ni kuonesha kuwa Wanaume hatuna akili kiasi kwamba kila kitu sisi Tuna******
3. Kavunja Haki za Wanyama.
Tunakubali Mbuzi tunamtafuna Nyama zake kama Kitoweo...Lakini haimaanishi hii ni haki Nyingine ya Mbuzi huyu ambaye ana haki ya Kutokudharirishwa hivi
4. Ubakaji
Sina Imani na Sintokuja Niamini Kama Huyu Mbuzi alikubali kutopa Huduma ama Burudani hii Kwa Jamaa
"STAREHE ZINAPELEKEA UMASIKINI WA KUJITAKIA"- Chuchu Hans"
Chuchu Hans
MSANII wa filamu anayetokea mkoani Tanga, Chuchu Hans,
amesema kuwa suala la umaskini kwa wasanii huwa linakuja kwa kujitakia kwani
walio wengi wanashindwa kufanya kazi kuweka akiba ya pesa na badala yake
wakipata chochote kidogo wanashinda wakifanya ufuska na uzinzi.
Chuchu alisema kuwa inawezekana wengi wanajisahau na kuamini
kuwa kila siku watakuwa wanapata pesa, na ndiyo maana kila kile kidogo
wanachokipata wanakitumia kwa hasara bila kujua siku ya kesho itakuwaje.
‘'Sidhani kama mashabiki wetu wanakuwa wanatuelewa
wanapotuona tukifanya starehe na anasa kila siku, umaskini tunajitakia kwa
sababu endapo tukiwa na tabia ya kujiwekea akiba si dhani maisha duni yatakuja
tena kikubwa ni kujipanga na kuacha kujisahahu,” aliongeza.
Related Posts :
"JAMANI...WANAUME ACHENI KUNIPIGIA SIMU !!...MIMI SIYO SHOGA" - BOB JUNIOR
Bob Junior "Chocolate Flavour"
IKO HIVI..................
IKO HIVI..................
HATIMAYE staa wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’
ameifungukia skendo yake ya kwamba yeye ni shoga...
Akizungumza kupitia kipindi cha runinga moja usiku wa Ijumaa
iliyopita, Bob Junior alisema chanzo cha yeye kudaiwa ni shoga ni wimbo wake
maarufu wa Oyoyo.
Alisema mara baada ya kuitoa video ya wimbo wake huo akiwa
anakata sana mauno, watu walikuwa wakimpigia simu, wengine wakimtumia meseji
kwamba, anaonekana ni ‘chakra’ maana anayaweza sana mauno.
“Watu wanasema mimi ni shoga, lakini si kweli. Kisa
kilianzia kwenye ule wimbo wangu wa Oyoyo. Unajua katika video ya ule wimbo
nilikata sana mauno, watu wakaamini mimi shoga.
“Wengine walikuwa wakinitumia hata meseji wakiamini hivyo.
Kwa hiyo sababu kubwa ni ile video tu, watu wana mambo ya ajabu sana,” alisema
Bob Junior huku watu alioongozana nao
usiku huo wakitingisha vichwa kukubaliana naye.
Ishu ya Bob Junior kuonekana ni chakra pia iliwahi
kusababisha amfikishe kortini kwenye Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Miss
Tanzania 2006, Wema Sepetu akidaiwa kumtukana msanii huyo matusi ya nguoni
likiwemo hilo la ushoga.
Katika kesi hiyo iliyofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa mara
ya kwanza Mei 4, 2011 na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi Mariam Masamalo, Wema
alihukumiwa kulipa faini ya shilingi 40,000 au kwenda jela miezi 6 ambapo
alifanikiwa kulipa.
Related Posts :
KESI YA LULU BADO "MAGUMASHI" TUPU...
Elizabeth "Lulu" Michael
KESI ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael
maarufu kama Lulu, imeendelea kupigwa kalenda kutokana na upelelezi wake
kutokukamilika.Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven
Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo
nyumbani kwa marehemu Aprili 7, mwaka huu.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo,
Agustina Mmbando, jana ilitajwa mahakamani hapo lakini kwa mara nyingine upande
wa mashtaka uliendelea kudai kuwa upelelezi haujakamilika.Wakati kesi hiyo
ilipotajwa Novemba 5, mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilisha
ili hatua nyingine ziweze kufuata, Wakili wa Serikali, Seth Sekwao alidai
upelelezi haujakamilika.
Kutokana na taarifa hiyo ya upande wa mashtaka, mmoja wa
mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Peter Kibatala alitaka kuharakisha upelelezi wa
kesi hiyo, ili iweze kusonga mbele.
Wakili Kibatala, ambaye pia ni Makamu Rais wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS), alidai kila mara upande wa mashtaka umekuwa ukidai
upelelezi haujakamilika, jambo ambalo linaifanya kesi hiyo ishindwe kuendelea
katika hatua nyingine.
“Ni muda mrefu sasa, kesi hii imekuwa ikitajwa mara kwa mara
upande wa mashtaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika. Hivyo tunawakumbusha
upande wa mashtaka ujitahidi kuharakisha upelelezi ili iweze kusonga mbele,”
alidai Wakili Kibatala.
Upande wa mashtaka uliiomba mahakama ipange tarehe nyingine
ya kutajwa.
Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 3, mwaka
huu itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa
umekamilika.Lulu alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili 11, mwaka huu
na kusomewa shtaka moja la mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.
Akimsomea shtaka hilo, Wakili wa Serikali Mwandamizi,
Elizabeth Kaganda alidai Aprili 7, mwaka
huu eneo la Sinza Vatcan alimuua msanii, Steven Kanumba.
Related Posts :
TUME TA MABADILIKO YA KATINA YAANZA KUKUSANYA MAONI WILAYANI KARATU
Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Daudi Ntibenda
akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (hawapo pichani) jana
jumatatu Novemba 19, 2012 wakati wajumbe hao walipofika ofisini hapo kabla ya
kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya Wilayani
humo. Kushoto ni mjumbe wa Tume, Bi. Mwantumu Malale.
Akina Mama wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya
ya Karatu mkoani Arusha wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa
mkutano wa kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya
ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (mwenye shati jeupe) akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za maoni kuhusu Katiba Mpya kwa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Audry Veldan kilichopo kijiji cha Shahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.
Mkazi wa kijiji cha
Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Thimos Mushi (51)
akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano wa kukusanya maoni
ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijiji hapo jana jumatatu Novemba
19, 2012.
Mkazi wa Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, John
Nando (73)akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo jana jumatatu
Novemba 19, 2012 katika Kata hiyo.
PICHA : TUME YA KATIBA














