BABA AKE DIAMOND PLATNUMZ KUMBE ALIKUWEPO KATIKA 40 YA MJUKUU WAKE KWA HAMISA MOBETO
Na Baba Juti
BAADA ya kila kitu kuwekwa Wazi, Basi Hamisa Mobeto ameendelea kuporomosha "picha" kadha wa kadha ambazo zinathibitisha kabisa kuwa hakuna ujanja, Diamond alikuwa na haki ya kukubali kuwa yule ni Mtoto wake
Tofauti na kupost katika account yake tu, Hamisa pia ametumia account ya Instagram ya mtoto wake huyo aliyempata na Mondi, kumpost Baba Mzazi wa Diamond Platnumz ambaye alikuwa katika 40 ya Mjukuu wake "AbdulLatif Naseeb Abdul"
SHAMSA FORD : " TUNAHITAJI MAOMBI "
Na Instacop
SIJUI kama bado anazungumzia Vugu vugu la hamisa Mobeto na Diamond Platnumz ama lah, lakini hiki alichokisema Muigizaji Wa Bongo Movie SHAMSA FORD, nadhani kinawalenga wanawake wote kabisa
Kupitia Instagram account yake, Shamsa alidai kuwa, adui wa Mwanamke siku zote ni mwanamke mwenzake, na kamwe haitokuja kutokea kamwe wanawake wakapendana
Katika kukazia zaidi kauli yake (ingawa bado hatujui nani mlengwa ingawa tunahisi kamzungumzia Mobeto), Shamsa ambaye hivi sasa yupo katika Ndoa yenye furaha na mahaba tele, aliandika kuwa, mwanamke ndo huwa mstari wa mbele kumuumiza na kumdhalilisha mwanamke mwenzie
Tunamnukuu
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie.haitakuja kutokea kamwe wanawake tukapendana.mwanamke ndo huwa mstari wa mbele kumuumiza na kumdhalilisha mwanamke mwenzie.kabla ya kumuumiza mwanamke mwenzio jaribu kuvaa viatu vyake ingekuwa wewe ungefanyaje..wanawake sisi daaa####TUNAHITAJI MAOMBI
Related Posts :
ALERT? : NAY WA MITEGO NA CHIDDI BENZ KUNANI TAREHE 14/10/2017 ?
Na Rich Sam & Insta Cop
UKIMCHUKUA Chiddi Benz, halafu ukafuatili Historia Yake, kuna mambo mengi sana ambayo utayabaini na hata katika kipindi cha Sasa. Hasa tukigusa katika Flows na Hitsongs ambazo Chiddi ameshazifanya na kuzithibitisha kwa umma tangu alipoanza Game, basi utakubaliana na Sisi kuwa huyu Jamaa ni "King Kong" kweli
Pia ukimchukua Nay Wa Mitego, maarufu kama True Boy, "ukapuyanga" kuzinyaka harakati zake Since anaanza, utakubaliana na sisi kabisa kuwa huyu jamaa ana amsha za kutosha kabisa kwa wana kibao na kila akiachai "Jiwe" huwa ni Jiwe kweli
Sasa, kupitia Instagram ya Nay Wa Mitego, Chiddi Benzi na True Boy mwenyewe, huenda wakaja na jambo ambalo pengine litakuwa linawahusisha wote wawili, ama kuna mmoja kati yao ambaye atakuja na kitu tofauti siku ya OCTOBER 14, 2017
Ingawa kumekuwa na posts kadhaa ambazo zinamuonesha Chiddi akiwa katika msimamo wa kauli yake ile ya kuja na ngoma aliyofanya na TUPAC, lakini hizi video Clip na Post zenye caption ya Tarehe tu, zinaanshiria kuna jambo
Related Posts :
INSTACOP: GOOD MORNING AFRICA... HERE IS WHAT ZARI IS TELLING YA'LL !!!
Na Insta Cop
#WatuWaMungu as Longer yameshaisha kwa Hivi sasa, lakini sijui kwanini wabongo bado mnaendelea tu kuyaanika haya mambo, waacheni watu wapumzike Tafadhari
Asubuhi ya Leo, kupitia Instagram, Zari tayari keshasema anajipanga na Birthday yake, hivyo mengine yote ambayo yametokea, tyaache Nyuma na tuyachukulie kama Changamoto
Related Posts :
ITAPENDEZA EEH: UKARIBU WA JANET JACKSON NA EX WAKE JERMAIN DUPRI UNAWEZA KURUDISHA MAHABA YAO YA KIPINDI CHA NYUMA?
Na Rich Sam
#WatuWaMungu Kuna kila dalili ya kuwepo kwa "I Still Cant Forget You" baina ya Couple ya kipindi cha nyuma, Jermain Dupri pamoja na Janet Jackson
Kwa Mujibu wa Info ambazo "Watu Wa Mungu" tumezinyaka ni kwamba, tangu Janet Jackson aachane na Mumewe WISSAM AL MANA, na hata kubainika kuwa kuna mengi ya kikatili katika Ndoa yake ambayo kayapata, basi Ex- Wake wa kipindi cha Nyuma, Jermain Dupri ameanza kuwa Karibu naye kumpa Faraja
Chanzo aminifu kabisa kutoka kunako familia ya JACKSON'S, kimedai kuwa, ni kweli bado hali ya Janet haijakaa sawa hasa kisaikolojia, na amekuwa ni mtu ambaye analia mara kadhaa kulingana kile ambacho tayari kimeshawekwa wazi.
"Na kulingana na hilo, Jermain Dupri ambaye ni Mpenzi wake wa Zamani kabla hata hajaolewa, hivi sasa yuko naye karibu hasa kwa njia ya Mawasiliano zaidi. Hii inampatia Faraja mara kadhaa Janet Jackson, na kuendelea kupata Nguvu"
Kuhusu kuwepo na Uwezekano wa wawili hao kurejesha mahusiano yao, chanzo hicho kilidai kuwa hakifahamu chochote, lakini lolote linaweza kutokea, maana huwezi jua ni jambo gani ambalo lipo katika hisia zao.
Related Posts :
IMEKULA KWENU !!!! : HII NDIYO "CHUMA" MPYA YA TYGA....PESA KAZITOA WAPI?
Na Baba Juti:
KUNA Wengi sana ambao wanatamani kujua ni wapi ambapo Rapper TYGA a.k.a "T RAW" katoa wapi Kiburi na nguvu ya kununua Gari kali kama lile na kujiachia nalo katika Mitaa kadha wa Kadha
"Wakuda" wa Mambo ndio ambao wamejaa maswali hayo, ukizingatia ni muda kidogo tangu makali ya Tyga yameonekana katika MUSIC INDUSTRY hapa Duniani
PICHA LIKO HIVI
Hitmaker huyo "1 ON 1" alionekana akiondoka kunako mgahawa mmoja huko LOS ANGELS, akiwa na Binti yule ambaye ana muonekano wa Kylie Jenner.
Lakini ukiachilia mbali Kuwa na mwanamke huyo, alikuwa ndani ya Ndinga Mpya aina ya BUGGATI ambayo kutoka sokoni, itakugharimu USD MILIONI 2 na Uchafu huko, kitu ambacho ndicho kimezua Maswali mengi sana
Ingawa yeye kwa upande wake huwa anajitetea kuwa ana biashara zake kadha wa kadha, lakini wataalamu wa "Umbea" wanadai kuwa, Biashara za Tyga, haziwezi kumfanya kumiliki ama kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kiasi hicho, na hata kufikia hatua ya kununua BUGGATI kwa ghafla hivyo.
Related Posts :
HAIWAHUSU !!!!!! : KARRUECHE TRAN KAFANYA KAMA ALIVYOFANYA FAIZA ALLY?
Na Baba Juti
HIVI, Karrueche Tran aliwahi kutizama picha ya Kipindi kileeee, ya mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini-JOSEPH MBILINYI, anayefahamika kwa jina la FAIZA ALLY ?...maana duuuh
Ex-Girlfriend wa Chris Brown , Karrueche alijikuta akitoa Version ya FAIZA ALLY baada ya kuzama Club akiwa amevalia Nguo ambayo iliruhusu "Makalio" yake yawe wazi bila kificho cha kuficha, bali iwe na kificho cha kutamanisha.
Kupitia Picha hizo, wengi walishtushwa na muonekano huo, huku baadhi wakionekana kutolea mimacho tamnye hilo ambalo bibie huyo alikuwa nalo.
Ukiachilia mbali muonekano huo wa kutamanisha, inasemekana kuwa Karrueche hivi sasa ameamua kutumia njia hiyo kuweza kufanya kile ambacho amekipanga, yaani style yake mpya ya uvaaji, pamoja na Brand za mavazi ambazo anataka kuanza kuzifanyia kazi
Moja kati ya Waajiriwa wake katika Brand atakayokuja nayo, anadai kuwa, Wengi ni kama wanamchukulia hajielewi, lakini anachokifanya ni kutimiza ndoto zake
"Ni Kweli wengi wanadhani kuwa Karrueche ameanza kupoteza akili na hata kufuata yale maisha ya kutafuta Umaarufu. Hapana, kuna kitu kipya ambacho anakileta muda si mrefu." Alisema Mfanyakazi huyo









