AMBER ROSE: TAYARI AISEE !!! SIO MASIHALA TENA
Na Baba Juti
#watuWaMungu Naona sasa Mahaba yameanza kunoga mpaka hatua kubwa imechukua nafasi yake kwa hivi sasa.
hatimaye Amber Rose ambaye ni Mzazi mwenzake na Wiz Khalifa wakikubaliana kabisa kila mtu kula zake baada ya kuvunja Ndoa yao, sasa amevalishwa Pete ya Uchumba Tayari na Mpenzi wake wa Hivi sasa, rapper 21 Savage
Amber Rose alianika mahusiano yake na Rapper Huyo mapema tu mwaka huu, huku akiweka wazi kabisa kuwa anahisi huyo ndiye mwanaume ambaye anajua kile ambacho Amber anakihitaji katika Maisha ya Mapenzi
Hata Hivyo, Pete hiyo aliionesha kupitia Instagram Story na kumuacha kila mtu akimpongeza kwa hatua Nzito aliyofikia.
Wiz Khalifa pia ana mahusianoa na Mwanamke mwingine lakini bado wanapeana ushirikiano Mzuri na amber Rose katika Malezi ya Mtoto wao SEBASTIAN
MUNGU NI MKUBWA: HIKI NDICHO KITU ANACHOKIFANYA ALICIA KEYS KWA HIVI SASA
Na Baba Juti
INAWEZA ikawa ni Njia moja wapo ya kuhamasisha hasa lengo kubwa ikiwa ni kwa wanawake ambao wanapatikana Barani Afrika, ukizingatia Tamaduni zetu zilivyo
Alicia Keys na Mbunifu wa Mavazi kutoka uingereza, Stella McCartney, wameamua kuvalia njuga suala la Kansa ya Titi kwa Wanawake Wengi ambao ni waafrika lakini wanaishi Nchini Marekani
Alicia ambaye pia anadai kuwa mama yake ni mmoja kati ya Watu walioponea chupu chupu katika Tatizo la Ugonjwa huo wa Kansa ya Titi, amesema kuwa kuwa kwa mujibu wa Takwimu ambazo zipo wazi, ni kwamba wanawake wengi ambao ni African-American kwa asilimia 45, hubainika kuwa na kansa ya titi iliyokomaa kuliko wamarekani weupe kwa sababu hawana muamko wa kupima na kubaini matatizo yao
Ukiachilia mbali suala la kupima, pia hata Nguo za ndani wanazovaa, yaani Braa, huchangia kwa asilimia kubwa kupatikana kwa Tatizo hilo
Mbunifu wa Mavazi Stella, pia amethibitisha kuwa alimpoteza mama yake kwa tatizo hilo hilo, hivyo ameamua kufanya kazi na Alicia keys, ikiwemo kubuni Bra ambazo zitasaidia kwa asilimia kubwa kupunguza maambukizi yasiyo naulazima
Related Posts :
JAMANI JAMANI JAMAAAANIIIII !!!: AMEJIUA KISA SNAPCHAT
Na Baba Juti
#WatuWaMungu hili linmaweza kuwa ni Tukio la kwanza kabisa kufanyika Snap Chat ikiwa ni mara nyingi sana matukio haya huwa yanafanyika Kupitia mitandao Mingine ya Kijamii
Bruno Monteiro mwenye miaka 30, aliamua kujiua kwa kujirusha katika Daraja la RIO NITERIO huko huko Nchini Brazil kwa sababu aliingia katika Ugomvi Mzito na Mke wake kabla hajaamua kujiua
Taarifa ambazo tumezipata na hata kupitia Video Clip ambayo ilimuonesha Bruno ambaye pia ni Msanii kutoka Huko huko Brazil, ni kwamba kwa siku kadhaa amekuwa katika mgogoro wa Kimahusiano na Mke wake Huyo, kitu ambacho kilimfanya alalamike mara kadhaa kupitia Mitandao ya Kijamii
Katika Hali nyingine, inasemekana kuwa, ugomvi mkubwa ilikuwa ni Mtandao wa Snap Chat ambao Mke wake amekuwa akiutumia vibaya, ikiwemo kujianika kwa wanaume wengine, lakini pia amekuwa akiutumia mtandao huo huo kufanya Biashara ya Ngono kitu ambacho kilimkwaza sana Marehemu
Baada ya kuona Mke wake amemblock kupitia Snapchat, aliamua kuchukua jukumu la kujiua na kuanika moja kwa moja kupitia Snapchat huku akidai kuwa chanzo kikubwa ni mtandao huo huo.
Ingawa baadhi ya Madreva piki piki na wasamalia wema kujitahidi kumzuia, Bruno alitupa Simu Chini na kisha kujirusha ikiwa ni baada ya kutoa malalamiko yake huku akiutuhumu Mtandao wa Snapchat kuwa kama chanzo cha hayo yote Kutokea




