RIPOTI YA KITENGO CHIMBUA CHIMBUA: MWANAMKE AMEUAWA KIKATILI BAADA YA KUDHANIWA ANATAKA KUWATEKA WANAFUNZI
MKUU WA TTM
Ama Kweli Binadamtunaunyama ambao kijumla hautabiriki.
Mwanamke huyu anaeonekana katika Picha, Ameuawa Kikatili na Wananchi Wenye Hasira kali, baada ya Kutuhumiwa kuwa alitaka kuwateka watoto wadogo waliokuwa Wakienda Shule
MKASA WENYEWE..
Ripoti ya KITENGO CHIMBUA CHIMBUA, imebainisha kuwa., mama Huyo aliwasimamisha watoto wadogo hao waliokuwa na umri unaokadiriwa Kuwa Miaka 7-10, na kuwaambia atawapeleka Shule, huku akiwaambia waongozane
Baada ya Kufikia uamuzi huyo, Mpita njia mmoja aliyemuona, alihisi huenda mama huyo anataka kuwateka watoto hao, na kuanza kupiga kelele za Msaada, na wananchi kuanza kumshughulikia.
Mpaka Mwanamke Huyo anakufa Kikatili, hakuna aliyekuwa na Uhakika kama Mwanamke huyo ni Mtekaji..au Lah
MWISHO WA RIPOTI:
KICHICHI-Kitengo Chimbua Chimbua, NIGERIA
TAARIFA NA PICHA KUHUSU BOMU LILILOLIPUKA JIJINI MWANZA
MHUDUMU wa
nyumba ya kupumzikia wageni wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa
Victoria, jijijini hapa, amejeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu
lililokuwa limewekwa kwenye korido la nyumba hiyo.
Tukio
hilo lilitokea jana (Jumatatu), kati ya saa 1:45 na saa 2:20 usiku, katika eneo
la Makongoro wilayani Ilemela wakati mhudumu huyo Bernadetha Alfred (25)
alipofungua kifurushi cha mzigo alichodhani kimesahaulika kwenye eneo hilo,
kabla ya kumlipukia.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Dayosisi hiyo, Mollel Rogart, kifurushi hicho kilichokuwa
kwenye mfuko mweusi wa nailoni, kilikuwa juu ya kreti (tupu) za soda, karibu na
eneo la kulia chakula lililopo katika nyumba hiyo.
“Ule
mfuko ulikaa pale siku tatu ndiyo usiku huo mhudumu wetu akakichukua
kukiangalia akidhani ni mzigo wa mtu umesahaulika.” Alieleza Katibu huyo na
kudai kuwa kifurushi hicho kilimlipukia mara tu alipokifungua na kujeruhi
vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili.
“Bernadetha
kajeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni na usoni na siwezi kusema
kwamba chanzo cha mlipuko huo ni mambo ya kidini japo ulinzi wetu haukuwa mkali
kiasi cha kudhibiti watu walioingia na vitu.” Alisema
Kamanda
wa polisi mkoani Mwanza, Valentino Mlowola akithibitisha tukio hilo, alisema kwamba
uchunguzi wa awali uliofanywa na kikosi maalum kutoka Dar es salaam umebaini
kuwa bomu hilo limetengenezwa kienyeji.
“Bado
tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili tubaini ni nani kafanya ili kama ni
mtu au kikundi kimehusika tuchukue hatua haraka. Natoa wito kwa wananchi
kutochukua vitu ambavyo hawa uhakika navyo, wanapoona vitu vya aina hiyo, watoe
taarifa kwetu.” Alisema Kamanda Mulowola.
Mlowola
alieleza kuwa, Bernadetha aliyejeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za
mwili, alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando ambako anaendelea na
matibabu.
Kamanda
huyo alieleza kwamba, mabomu (yakiwemo ya kienyeji) yako katika mifumo
mbalimbali hivyo wananchi hususan wahudumu wa sehemu za mikusanyiko wawe na
tahadhari na vitu vinavyoonekana kusahaulika na wasisite kuwajulisha polisi
vinapoonekana hivyo.
Mlipuko
huo uliozusha hofu kwa waumini mbalimbali wakiwemo wa Kanisa hilo, umetokea
ikiwa ni wiki moja baada ya maadhimisho ya ‘Huduma ya Mtoto’ kwa makanisa
mbalimbali ya Kikristu jijini hapa yaliyofanyika kwenye kanisa hilo,
yakitanguliwa na maandamano kutoka uwanja wa furahisha hadi KKKT.
Related Posts :
HIVI NDIVYO UNAVYOTAKIWA KUISHI NA RAFIKI HUYU
MARAFIKI ni watu Muhimu sana katika maisha ya
kawaida. Kuna muda huwa tunakutana na watu mbali mbali ambao huwa tunawafanya
kuwa marafiki kulingana na Muonekano, tabia, Historia za Kimaisha, na
mengineyo.
Kuna ukweli kwamba, kuna marafiki ambao huwa
wanakubali kile ambacho unakifanya, na hata kujivunia kuwa karibu na Wewe, ili
kufanikisha Suala hilo, ama Kukupa Ushauri mzuri na hatimaye kufikia pazuri.
Lakini Pia kuna marafiki ambao huwa
hawatabiriki. Leo anakupenda, kesho anakuchukia, Wiki ijayo anapenda
ushirikiano wako, Wiki nyngine hataki umuingilie katika mambo yake, lakini kuna
muda hataki hata kukusikia.
Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba huyo bado
ni rafiki ako, na unatakiwa ufanye yafuatayo:
- · Muamini katika kila anachokifanya
- · Mpongeze katika mafanikio anayofikia.
- · Mkumbushe mambo ya Msingi ambayo huenda ameyasahau.
- · Kuwa Mstari wa Mbele katika kufanikisha Kazi yake, Yaaluma, Kipaji, na hata Shughuli zake
- · Kumbuka Kujishusha Chini unapobaini hayuko katika Mood Nzuri
- · Mshirikishe katika Baadhi ya mambo yako ya Msingi hata kama hatofurahishwa nayo
- · Kubali ushauri wake, na kuuboresha Kama Una mapungufu.
- · Mheshimu, na uthamini utu wake, huku ukiepuka Kuhisi Mambo mabaya Juu yake.
- · Kuwa wa Kwanza Kumuombea kwa Mungu ili awe na maisha Bora
- · Mfanyie Kitu Kizuri ambacho hakiamini kama unaweza kukifanya.
- · Kubali na Pokea Lawama, Matusi, hasira, Chuki na Mengine, kutoka kwake dhidi yako.
- · Onyesha Furaha kila siku unapokutana naye, na epuka kumlaumu pindi asipozingatia Salamu yako, Ushauri wako, na hata anapokuona huna mchango wowote katika Maisha yake
Related Posts :
#BRING BACK OUR GIRLS..BOKO HARAMU BADO WANAZIDI KUTEKA WANAFUNZI
Habari kutoka Nigeria zinasema kuwa, watu
wanaoaminika kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamewateka nyara wasichana 8 katika
kijiji cha Warabe kilichoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Habari zaidi
zinasema kuwa, wasichana hao wenye umri wa kati ya miaka 12 na 15 walitekwa
nyara wakati watu hao wenye silaha walipovamia kijiji hicho na kupora mifugo
pamoja na vyakula. Tukio hilo limejiri siku moja baada ya Boko Haram kutangaza
kwamba linawashikilia zaidi ya yanafunzi wa kike 200 waliotekwa nyara katika
shule moja mjini Chibok mwezi uliopita. Kiongozi wa Boko Haram,
Abubakar Shekau
ametishia kuwauza wasichana hao ndani na nje ya Nigeria.
Umoja wa Mataifa umeonya kundi la Boko Haram
ukisema kuwauza wanafunzi hao wa kike ni kinyume cha sheria za kimataifa
zinazopinga biashara ya utumwa na hatua hiyo itapelekea wanachama wa kundi hilo
kutafutwa kwa kosa la kutenda jinai dhidi ya binadamu.
Siku ya Jumapili Rais Goodluck Jonathan alisema
serikali yake inafanya juhudi zote kuwatafuta na kuwaokoa wasichana hao na
akaziomba baadhi ya nchi za Magharibi kuisaidia serikali yake katika suala
hilo.













