Na Ibra-The Insta-Cop
#WatuWaMungu Nyie mnataka nini lakini?...maana kila kinachokuja kwenu huwa hakikosi kasoro.... mmepewa Macho ya aina gani lakini
Haya, Wakati napita huku na kule kwenye Instagram account za Watu mbali mbali, nikakutana na Instagram account ya Mama Mzazi wa Diamond Platnumz-KENDRA MICHAEL
Nikakagua kagua weeeeee, nikavutiwa na kile ambacho amepost kuhusu yeye na Mwanaye Diamond Platnumz, hasa ukizingatia huu ni Mwezi wa Toba (Ramadan), pamoja na picha mbali mbali za wajukuu wake, yaani kiukweli anawapenda sana inavyoonekana
Lakini nikaona kitu kama Simu Hivi, nikasema basi ngoja niangalie Kile alichopost Bi Mkubwa Wetu...Well, ni Simu nzuri, kali, SAMSUNG EDGE...safi sana kiteknolojia...
Ila Watanzania sasa walivyo "Wakuda" hawakujali simu, ishu nzima ikahamia kwenye Vidole Vyake...
Mbona viko poa Tu jamani?...au Nyie mnasemaje?
JAMANI !!! : AFARIKI KWA KUOGELEA NA TATTOO MPYA
Na Baba Juti
#WatuWaMungu Ni wangapi Mnapenda Kuchora Tattoo Jamani?. Na
Wangapi huwa mnatamani Siku moja mjekuwa na Tattoo?
Sasa, haijalish kama unataka Uichore Puani ,Mdomoni, ama Shingoni
ni Wewe tu, lakini kuna hii Taarifa Hebu tuchangie wote na Tufahamu.
Mwanaume mmoja Mwenye Umri wa Miaka 31 huko TEXAS Marekani,
amepoteza Maisha ama amefariki baada ya Kuoga akiwa na Tattoo Mpya
Kwa Mujibu wa Taarifa kamili kutoka kwa Daktari ambaye alikuwa
akimuhudumia ,Jamaa huyo alikuwa amechora Tattoo, lakini baada ya Siku 5,
Tattoo ikiwa bado ni Mbichi Mbichi hivi, alienda kuogelea Baharini na huko ndiko
lilitokea la kutokea
Inasemekana Jamaa huyo alienda kuogelea huko GULF OF MEXICO,
hali ambayo ilimfanya ashambuliwe na Backteria ambao walimsababishia Kifo Hicho.
Dr. Nicolaus Hendren ambaye ndiye alimhudumia, anadai kuwa jamaa
alifika Hospitalini hapo akidai kuwa Mguu wake wa Kulia ambao ndo wenye Tattoo
ulikuiwa ukimuuma, na Ndipo ilikuja kubainika kuwa katika Tattoo yake ambayo ilichorwa
na kuandikwa “YESU NI MAISHA YANGU: ilikuwa Imeshambuliwa na Bacteria hao
Pia Daktari huyo anadai kuwa, hali hiyo ilisababisha Miguu yake
yote kuuma na kisha kupatwa na Homa kali, huku upande wa Tattoo ukiwa umetafunwa
tayari
Related Posts :
LIL KIM: NDO KWISHA HABARI YAKE?
Na Baba Juti
#WatuWaMungu Tunafahamu Vizuri Heshima ya Rapper wa Kike LIL
KIM hasa linapokuja suala zima la Hip Hop haswa kwa Wanawake
Lakini Najua mnalifahamu hili kuwa Lil Kim amekuwa akiishi maisha
ambayo kila Mtu huwa anasema daah, bibie huyu hawezi Fulia hataSiku Moja
.
Sababu kubwa ni kwamba, amekuwa akivaa mavazi ya gharama sana,
Kuendesha Ndinga za Gharama, na hata kuhang out na watu ambao wana maisha
Fulani Heavy kidogo, lakini Kumbe hizo zote ni Mbwembwe za kutuzuga tukupitia
Ma-social Networks
Hakim kutoka Mahakama ya NEW JERSEY ,Marekani, ameamuru Lil
Kim kunyang’anywa Mjengo wake baada ya kushindwa kulipa Deni la Mkopo
Bank inayofahamika kwa jina la HSBC ilimfikisha Mahakamani
Lil Kim mwaka 2010 kwa madai ya kusitisha Ulipaji wa Deni la Mkopo huo ambao ulikuwa
ni Mkopo wa Nyumba
Pia Bank hiyo ikaongeza kuwa, Mwaka
2002, walikubaliana na Lil Kim kuwa wampe Mkopo wa Nyumba na atakuwa akilipa
USD 10,000 kwa Mwezi kama mallipo ama marejesho ya Mkopo.
Ingawa mpaka Hivi sasa haijafahamika kama ni kwanini Lil Kim
aliacha kulipa Mkwanja huo, mpaka hivi sasa, Lil kim anatakiwa kulipa USD Milioni 2 kitu ambacho
huenda ni kweli asifanikiwe kukilipa hata kidogo
Related Posts :
MAKUBWA !!! : ETI WATOTO WA J-LO HAWAMPENDI BABA YAO WA KAMBO MPYA !
Na Baba Juti
#WatuWaMungu Mahusiano ya Mwanamama Jeniffer Lopez a.k.a
J-Lo na jamaa anayefahamika kwa jina la ALEXANDER RODRIGUEZ yamekuwa na Mwendokasi
wa hali ya Juu, na inabidi tulipokee kama lilivyo.
Lakin ipia, wawil ihao ili kuwekama husiano yao yawe Imara zaidi,
tayari wameshatambulishana kwa watoto wao,
maana ukizingatia kila mmoja alikuwa tayaria na watoto kabla hawajaanza mahaba yao
ya Mwendokasi
Lakini Picha kali lipohapa, ambapo Taarifa zilizotufikia zinadai
kuwa, Watoto wa JLo ni kama hawajamkubali ama kumpokea kwa moyo mweupe Baba yao
wa kambo, ambaye ni “Mupenzi ya Mama Yao”
Inasemekana kuwa, watoto hao hawajaonesha “Amsha” yoyote mpaka
Hivi sasa kwa Alexander Rodriguez kama ambavyo ilikuwa kwa Casper Smart, kitu ambacho
kinamfanya hata J-Lo Mwenyewe ajiulize maswali Mengi
Mvujisha Umbea ambaye yuko karibu na J-Lo anadai kuwa Mapacha
wake ambao wana Umri wa Miaka 9 Hivi sasa wanaonekana dhahiri kabisa kama wanamuogopa Mzee Mwenzetu Alexander ingawa bado
wanavuta Subira kuona kitakachoendelea
Tofauti na Hilo, Alexander anajitahidi sana kuwa karibu nao na
hata kuwafahamu vizuri mapacha hao ambao J-Lo alizaana Marc Anthony lakini bado
kama inakuwa Ngumu
Pia Hitmaker huyo wa “LOVE DON’T COST A THING” amedai kuwa hatakama
watoto wake watamchukia au kutokumpenda Mupenzi wake mpya, haimzuii kuendelea kula
maraha ya kimahaba naJamaa huyo, watazoea tu









