UNAMKUMBUKA? : NYANSHINSKI WA X-KLEPTOMANIA ANARUDI TENA KATIKA GAME
KUPITIA Mtandao wake wa Kijamii, Mkali Nyansinski ametangaza ujio wa Track yake mpya ambayo anaiandaa hivi sas katika moja ya Studio zilizopo CHICAGO Nchini Marekani.
Nyanshinski ambaye ni X-Memba wa X-Crew ya Kleptomania Boys Nchini Kenya, ameuwa kimya kidogo huku Mwenzake COLO akioneka kukaza zaidi katika Level Nyeusi na Ngumu za Kuchana.
Nshinski amewahi kutisha Katika Collable yake na Amani "Bad Boy" na Nynginezo
PICHA : HOYCE TEMU ALIVYOIFARIJI FAMILIA YA MAREHEM DAVID MWANGOZI
POLE MAMA: Bi. Temu akiwa amewapakata watoto wa marehemu
aliifariji familia hiyo akiwataka kutokata tamaa na kuwa Mungu yupo na kwa kuwa
watanzania ni wamoja mambo yatakwenda sawa.
TUKO PAMOJA: Hoyce Temu akimfariji mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi.
Itika Mwangosi alipoitembelea familia hiyo mkoani Iringa.
FARAJA:Bi. Itika Mwangosi akionyesha uso wa matumaini baada ya
kupewa maeneo ya faraja na Hoyce Temu.
MSAT: MOHAMED DEWJI
Related Posts :
MAKUBWA : SPIKA WA BUNGE ATUMIWA UJUMBE MFUPI WA MATUSI NA KUMUAMURU AJIUZURU
Inaripotiwa kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, amepokea
jumbe za maneno 400 na za miito ya simu 200 zenye matusi ya nguoni kutoka kwa
watu wakimtaka ajiuzulu.
Aidha inasemekana kuwa amesemea jumbe hizo zimerekodiwa.Kwamba, Spika alianza kupokea jumbe
hizo kuanzia juzi, baada ya viongozi wa CHADEMA kutangaza namba za simu za
Spika kwenye mkutano wa hadhara na kuendelea jana ili kutumia ‘nguvu ya umma’,
kumlazimisha ajiuzulu.
Sababu ya kutumwa jumbe hizo inaripotiwa kuwa ni baada ya
hatua ya Spika Makinda kutangaza mabadiliko ya Kamati za Bunge, yaliyoivunja
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na shughuli zake kuwekwa
chini ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ambapo katika mabadiliko hayo,
aliyekuwa Mwenyekiti wa POAC, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
hakuridhishwa nayo na hivyo kumshitaki Spika Makinda kwa Wananchi ili wamng’oe.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema uamuzi huo
haukufanywa na Spika Makinda peke yake, bali ni baada ya kushauriana na Kamati
ya Kanuni za Bunge, ambayo iliridhika na sababu za kuchukuliwa uamuzi huo.
Wajumbe wa Kamati iliyoridhia makubaliano hayo mbali na
Spika na Naibu Spika, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA). Wengine ni Mbunge wa Mbulu, Mustapha
Akunaay (CHADEMA), Mbunge wa Kibondo, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), Mbunge wa
Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed
(CUF). Pia Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), Mbunge wa Bariadi
Magharibi, Andrew Chenge (CCM), Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani (CCM),
Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod
Mkono (CCM).
CHANZO : HABARI LEO
Related Posts :
MAPIGANO GEITA: MCHUNGAJI AUAWA
MCHUNGAJI wa Kanisa la Pentecoste Assemblies of God Tanzania
(PAGT) Buseresere, Wilaya ya Chato, Mathayo Kachila (45) amefariki dunia huku
watu wengine 15 wakijeruhiwa kwa mapanga kufuatia vurugu kutokana na mgogoro wa
bucha. Tukio hilo lilitokea jana saa 2:27 asubuhi kwenye Soko la Buseresere
baada ya kundi la wananchi kuvamia bucha iliyokuwa na maandishi ya ‘Bwana Yesu
Asifiwe, Yesu ni Bwana’, kuwataka waliokuwa wakiuza kuifunga hali iliyozusha
vurugu. Kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo, wananchi hao wanaodaiwa kuwa waumini wa Kiislamu
walikuwa wamechukizwa na kufunguliwa kwa bucha hiyo, ndiyo wakachukua uamuzi wa
kwenda kuamuru ifungwe.
Inadaiwa kabla ya kufunguliwa kwa bucha hiyo, Wakristo
walifanya mkutano wa Injili Uwanja wa CCM Katoro na kutangaza kuwa, watachinja
nyama yao na kuiuza kwenye bucha maalumu.
“Tulipata taarifa za kufunguliwa kwa bucha hii na tulipofika
kuwaomba waache kuuza nyama yao, waligoma na kuendelea kuuza, baada ya kuona
hilo wafuasi wa Dini ya Kiislamu walikimbilia msikitini na kuunda kikosi cha
kupambana nao,” alisema Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata)
Wilaya ya Chato, Yusuf Idd.
Alisema licha ya kuwasihi hawakumsikiliza, waliamua kwenda
kupambana.
Katika vurugu hizo, duka la Idd lilivunjwa na kuporwa simu
na fedha, huku pikipiki mbili ambazo hazijafahamika wamiliki zilichomwa moto.
Katika vurugu hizo nyama ndani ya bucha hiyo ilimwagiwa
maji, ikiwamo kuharibiwa kwa madirisha na milango yake.
Licha ya majeruhi kutajwa kuwa 15, waliotibiwa Kituo cha
Afya Buseresere na kuruhusiwa ni Abdallah Shaaban (25), Abubakar Shaaban (27),
Faruk Shaaban (14), Kassim Almasi (23), Yusuf Shaaban (18), Bilal Hassan na
Abdallah Ibrahim.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Dk John
Lumona alisema majeruhi wengine waliofikishwa ni Yasin Rajabu (56), Said
Taompangaze (47), Masoud Idd (21), Ramadhan Pastory (36), Haruna Rashid (61) na
Sadiq Yahya (40), ambaye hali yake ameieleza kuwa mbaya na alipelekwa Hospitali
ya Rufani Bugando. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geira, Paul Katabago
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa rasmi baada ya
kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo aliwataka wananchi
kutulia kwa vile suala hilo linashughulikiwa na serikali na litapatiwa
ufumbuzi.











