STOPA RHYMES : STYLE TATU ILIWAFANYA WASANII WABADILIKE NA KUANZA KUIFUATA TONGUE TWISTA NA KUPATA UJASIRI WA KUTUMIA LUGHA ZA KIGENI KATIKA NYIMBO ZAO
Na Baba Juti
RAPPER kutoka Arusha na Hitmaker wa STYLE TATU, Stopa Rhymes Okoyi, kupitia Hit Zone, ameweka wazi kabisa kuwa katika Game kwa asilimia kubwa, kuna baadhi ya Wasanii ambao huangalia kuna kitu kimefanyika halafu na wao wafuate
Akiweka Wazi kuhusu Hilo, Mkali huyo ambaye aliua pia na Zigo la Boom Bye Bye, amesema kuwa, Kipindi ambacho yeye anaachia Style 3, Wasanii Wengi walianza kupata Ujasiri wa kufuata Mfumo na kutumia Tongue Twista na hata kutumia Lugha za kigeni kama Vile Kiingereza
Tofauti na Hilo, Stoppa anaamini kuwa, Support ya Mashabiki katika Kipindi hiki Imekuwa Ngumu, maana wanasupport kwa kucomment tu, kulike, na mengineyo, lakini katika kununua bidhaa zao, imekuwa Ngumu
MAADHIMISHO YA SIKU YA MABOGA: IZZO BUSINES ANADAI KUWA UBACHELOR ANAOISHI DAR, UMEMFANYA ASHINDWE KULA MABOGA MPAKA ATAKAPORUDI KWA MAMA YAKE (AUDIO)
Na Baba Juti & Cathberth Mazigo
KAMA wewe unapenda kula kula kama wengine ambao tulishajaliwa kula vyakula vya aina tofauti tofauti sana, basi utakubaliana na mie kabisa kuwa, Kuna Chakula ambacho ni Jamii ya Tunda kinachoitwa BOGA
Boga haizalishi Tunda tu, bali hata majani yake huwa ni Mboga Nzuri, na unaweza kuiita Msusa, au kuyapika Kama Mrenda kwa jamii mbali mbali kama vile wasukuma, Wanyamwezi na wengineo
Lakini Kama Haitoshi , unaweza kufurahia Juice ya Maboga, na Hata Ile Mbegu yake, hutumika kama kitoweo pia, na hunoga sana ikiwa na Viazi Vitamu
LEO, OCTOBER 26, Ni Siku Maalum ya Maboga, na huazimishwa Sehemu Mbali mbali Hapa Duniani, lakini Pia Huazimishwa kwa Njia Tofauti.
Baadhi ya Mataifa Husherekea na kutumia Maboga kama kihisishi cha Siku ya HALLOWEEN, Lakini kuna Badhi ya Mataifa hupinga Vikali matumizi hayo ya Maboga katika Siku Hiyo
Mataifa hayo huamini kabisa kuwa, Heshima ya Boga Ni Chakula Maalum na siku ya Maboga ni Siku ya kufaidi kitu Kizuri na Rahisi zaidi kupika ama kuandaa.
Tofauti na hayo, Boga kwa Kiingereza huitwa PUMPKIN , jina liliotokana na Lugha ya Kigiriki ambao huliita PEPON wakimaanisha TIKITI MAJI KUBWA
Ukiachana na Hilo, Ufaransa huliita Boga kama POMPON, Kisha Uingereza wakaliita PUMPION, lakini Wamarekani Wakaliita PUMPKIN na ndivyo linafahamika hivyo Tayari.
Izzo Business , Msanii wa Kizazi Kipya Hapa Nchini Tanzania, anasema kabisa kuwa Ni Kitu ambacho Huwa anakipenda, ila kutokana na Maisha ya Kibachelor ambayo anaishi Dar, hajala Boga Muda Mrefu wala Mboga ya Msusa, lakini akienda Mbeya kwa Mama yake, lazima alikule
Lakini Pia, anakiri kuwa anapenda sana hicho kitu na anajivunia kulipenda
Related Posts :
NISHER: ANAAMINI KUWASIKILIZA WATU, NI NJIA YA KUPIGA HATUA
Na Baba Juti
DIRECTOR Nisher Kutoka Hapa Hapa Nchini Tanzania, amepotea kidogo katika Industry ya Production, but Guys, mujamaa yuko na mashine Very Classic na Expensive Bya Hatari !!!
Kitu ambacho Director huyu aliyewahi kusumbua kabla hata ya akina Hascana kutake Over, ni kwamba kuwaheshim na kuwasikiliza Watu sometimes, inakusaidia kuzingatia na kufanya kazi yako kwa Ufanisi...
Akizungumza hayo kupitia Channel yake ya Youtube, Nisher ambaye hivi sasa ameachia Series yake ya ALEX, amesema kuwa, kwa asilimia kubwa huwa anapitia Comments za Wadau wake na kuchambua vizuri, ili kuweza kupata japo kitu cha msingi katika Kazi yake
Tofauti na Hayo, Nisher amesema hajaacha kufanya Video za Muziki kama ilivyokuwa awali, bali hivi sasa anafanya kwa Malengo, tofauti na zamani alvyokuwa akifanya kwa sababu ya kutafta jina, na alikuwa akifanya hata kama ni Kulipua
Kwa Upande Mwingine, Nisher amesema kuwa, anapenda kuwasuprise zaidi, hivyo hatoshea vitu vingine, ila ni bora mkamfuatilia katika mitandao yake ya kijamii ili kujua what is Next.
Related Posts :
KEKO: HATIMAYE AMERUDI KATIKA FLOW..KUPIGA SHOW NCHINI KENYA
Na Baba Juti
ANGALAU sasa wale ambao tulikuwa tuna hamu na Flows na Matamshi Matamu kutoka kwa Ugandan Female Rapper - KEKO, tunaweza anaza kupata matumaini ya Ujio Wake
Baada ya Kuhusishwa na matumizi ya dawa Za Kulevya, ikiwemo pia kufulia kimuziki, na hata kuminywa sana na management yake na hata kutamka kuwa sasa anabwaga manyanga katika Music Industry, hatimaye Keko hivi sasa ana matumaini ya kurudisha heshima yake katika Stage.
Hit Maker huyo wa HOW WE DO IT, anatarajia kupiga Show katika Jukwaa litakalofungwa katika Makao Makuu ya KENYA, Nairobi, katika Show ya QUEENS OF THE MIC itakayokunjwa November Mwaka huu
Keko ambaye kwa asilimia kubwa ana hamu ya kurejesha heshima yake katika Muziki wa Africa Mashariki , aliwahi kupitia majanga kadha wa kadha ya kukatishwa tamaa, baada ya kufutwa katika Mfululizo wa COKE STUDIO kwa Mwaka Jana, na hata kutimuliwa katika Moja ya Hotel Kubwa Nchini Kenya, kwa madai kuwa alilewa sana na kusababisha fujo.
ALL THE BEST KEKO.
Related Posts :
ANGELINA JOLIE: AMESITISHA MASUALA YA MOVIE KULE HOLLYWOOD ILI KUWA KARIBU NA WATOTO WAKE,
Na Baba Juti
MUIGIZAJI Angelina Jolie ameamua kuweka Kando suala zima la Kuporoduce Filamu aliyokuwa na hamu nayo sana, ili kuwa Karibu na Watoto wake
Uamuzi huo unatokana na Vuguvugu la Talaka na Mumewe wa Muda Mrefu, BRAD PITT, ikiwa ni baada ya kuwepo kwa Madai kuwa, Mumewe huyo amekuwa akiwanyanyasa watoto wao kutokana na matumizi ya Pombe pamoja na Madawa ya Kulevya.
Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Hollywood ni kwamba Bibie huyo hivi sasa hajihusishi tena katika Kumalizia Filamu yake ya FIRST THEY KILLED MY FATHER ili kuhakikisha kuwa suala la malezi linaenda sawa kwa watoto wake
Tofauti na hilo, inasemekana kuwa, Watayarishaji wa Filamu hiyo wamekuwa wakijitahidi kumuhusisha Angelina Jolie kwa Njia ya SKYPE, lakini amekuwa hajibu Chochote.
Pia inawezekana kabisa Angelina Jolie akahamia LONDON.
Lakini Kwa Upande Mwingine, Mume Wake Brad Pitt anatarajia kutokea katika RED CARPERT ya Uzindz wa Filamu ya ALLIED itakayoachiwa Rasmi na kuingizwa Sokoni NOVEMBER hii.
Related Posts :
TONI BRAXTON: NI MBISHI BALAA, AMEAMUA KUPIGA SHOW AKIWA NA KIFAA CHA HEART CONTROL
Na Baba Juti
SIKU Kadhaa zilizokata, kama utakuwa unakumbuka Vizuri, tulikupa Info Kuwa, Mwanamama Toni Braxton, alikumba na tatizo baya la Kiafya hali ambayo ilimlazimu apelekwe Hospital Mara mbili kabla ya Show yake na hata kuahirishwa Mara Kadhaa.
Lakini Ili Kuonesha kuwa ni Mbishi Kupita Maelezo, Hit maker huyo wa Breath, aliamua kupanda jukwaani na kifaa maalum cha Kupima muelekeo wa Moyo Wake yaani HEART CONTROL.
Tatizo kubwa la LUPUS ambalo madhara yake huvamia kila sehemu ya mwili hasa Ngozi na sehemu ya Moyo, ndilo lilikuwa likimsumbua sana Bibie Huyu, lakini Hiyo bado haikumzuia yeye kufumua Show yake huko maeneo ya Savanna, lakini alionekana akiwa na kifaa hicho.
Kwa Mujibu wa Maagizo ya Madaktari wa Toni Braxton, bibie huyo anatakiwa kuvaa kifaa hicho masaa 24 kwa Wiki, ili kubaini Maumivu ya Kifua, pamoja na Shambulio la Moyo au Stroke kama ikibidi.
Related Posts :
JUSTIN TIMBERLAKE HUENDA AKAINGIA MATATANI BAADA YA KUPOST PICHA AKIPIGA KURA.
Na Baba Juti
SIJAFAHAMU kwa Nchi ya Tanzania kama ni Kinyume cha Sheria kupost Picha ukiwa unapiga Kura hasa ya kumchagua kiongozi wa Nchi au lah, lakini asilimia kubwa huonekana wakiwa Tayari wana wino katika Vidole vyao.
JUSTIN TIMBERLAKE huenda akautana na kifungo cha Siku 30 Jela pamoja na Fain ya Mkwanja, baada ya kupost Picha akiwa anapiga Kura, katika Maeneo ya TENNESSEE huko Nchini Marekani
Kwa Mujibu Mawanasheria wa Jimbo la SHEBY huko huko Tenessee, inasemekana kuwa Hitmaker huyo wa Cant Stop The Feeling hivi sasa yupo katika mahojiano na ukaguzi mkubwa hasa kubaini kwanini alikiuka Sheria za Nchi Hiyo, kupiga Picha ukiwa unapiga Kura, na kupost katika Mitandao ya Kijamii
katika Sheria ambayo iliboreshwa na kuhimizwa kufutawa zaidi kuanzia mwaka Jana, Ni Marufuku kwa Mtu yeyote kupiga picha au kurekodi mazungumzo ya aina yoyote yanayotokea katika Eneo la Kupiga Kura. na Endapo itabainika kuwa, umevunja Sheria hiyo, basi unakula Nyundo ya Siku 30 Jela, pamoja na Faini ya USD 50
SIJAFAHAMU kwa Nchi ya Tanzania kama ni Kinyume cha Sheria kupost Picha ukiwa unapiga Kura hasa ya kumchagua kiongozi wa Nchi au lah, lakini asilimia kubwa huonekana wakiwa Tayari wana wino katika Vidole vyao.
JUSTIN TIMBERLAKE huenda akautana na kifungo cha Siku 30 Jela pamoja na Fain ya Mkwanja, baada ya kupost Picha akiwa anapiga Kura, katika Maeneo ya TENNESSEE huko Nchini Marekani
Kwa Mujibu Mawanasheria wa Jimbo la SHEBY huko huko Tenessee, inasemekana kuwa Hitmaker huyo wa Cant Stop The Feeling hivi sasa yupo katika mahojiano na ukaguzi mkubwa hasa kubaini kwanini alikiuka Sheria za Nchi Hiyo, kupiga Picha ukiwa unapiga Kura, na kupost katika Mitandao ya Kijamii
katika Sheria ambayo iliboreshwa na kuhimizwa kufutawa zaidi kuanzia mwaka Jana, Ni Marufuku kwa Mtu yeyote kupiga picha au kurekodi mazungumzo ya aina yoyote yanayotokea katika Eneo la Kupiga Kura. na Endapo itabainika kuwa, umevunja Sheria hiyo, basi unakula Nyundo ya Siku 30 Jela, pamoja na Faini ya USD 50
Related Posts :
ANNE KANSIIME : KUWANIA TUZO ZA UK AWARDS - BAWR
Na Baba Juti
HAKIKA kila mtu hivi sasa anamfahamu vizuri Binti
mchekeshaji kutoka Nchini Uganda, ANNE KANSIIME !!!
YEs, The Good News ni kwamba Bibie huyu ambaye
amejichukulia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki, amechaguliwa kuwania Tuzo za
Kimataifa za UK BLACK AFRICAN WOMAN ROCK (BAWR) ambazo zinatarajia kufanyika
Uingereza , DECEMBER 03 2016
Tuzo hizo ambazo zilianzishwa na LINDANI MOYO mwaka 2013,
ziko maalum kwa ajili ya kuwapa Moyo wanawake wa Kiafrica, kuelimisha, na hata
kuhamasisha wanawake ambao wana mizizi ya Kiafrika katika harakati zao
Kansime amekuwa ni Msanii wa Vituko wa Kike Pekee kutoka
Afrika mashariki, asiyeogopa kuthubutu na hata kupambana mpaka kupata Deals
Nyingi sana
Related Posts :
TUMEMMIS KANYE WEST WA ZAMANI?
Na Baba Juti
WANGAPI wanakubali kuwa Rapper Kanye West Wa Zamani
alikuwa ni Bora kuliko Kanye West Wa Hivi Sasa?... Lakini Pia, ni wangapi
wanakubali kuwa Kanye West wa sasa ni Bora kuliko yule wa Zamani?
Swali hilo pia imebidi team tujiulize kama yanayosemwa na
Business patner wa Jay Z yana ukweli wowote, ikiwa ni baada ya kuwepo na
Mgogoro wa majibizano baina ya Jay Z na Kanye West
KAREEM BIGG BURKE ambaye ni Patner wa Jay Z katika Studio
ya ROCA FELLA RECORDS amedai kuwa, mara ya kwanza wakati anamsikia Kanye West
akimzungumza vibaya Jay Z na kudai kuwa hata watoto wao hawajawahi kucheza
pamoja, iliweza kumshtua kila Mtu.
BURKER ANASEMA...
"Nilishtuka sana kasikia kile ambacho Kanye aliksema
kwenye Jukwaa. hakukuwahi kuwa na tatizo baina yao.. kwa hiyo ukisikia kitu kama
hicho tena hadharani , lazima ushtuke kidogo. Mara ya Mwisho namuona Kanye ,
alizungumza vizuri na Jay Z. Sina uhakika sana kama mahusiano yao yamefikia
hatua hii. Na nilipozungumza na Jay Z kuhusu Ishu aliyoisema Kanye West, kila
mtu alibaki akisema TUMEMMISS KANYE WEST WA ZAMANI. Kwa kile ambacho ninafahamu
kutoka kwa Kanye, ni kwamba huwa ni mkweli sana. hivyo inaonekana kabisa kuwa
kuna kitu ambacho kinaendelea baina yao kwa hivi sasa. Anaweza kuzungumza kitu
kama hicho, lakini baada ya Wiki kama tatu, utamsikia tena akisema "Jay Z
ni Kaka Yangu kabisa. "
Tofauti na Hilo,
Nicki Minaj pia aliwahi kutamka kauli ambayo kila mtu ilimshtua kuhusu Kanye
West, ambapo alidai kuwa Kanye West wa Zamani sio wa hivi sasa, maana kupitia
kwa mkwaju wa GOLD DIGGER, alikuwa akiwapondea wanawake tegemezi sana na
wanaotafuta pesa kwa njia za kijanjanja kijanjanja, huku akihamasisha Wanaume
Weusi, kutwaacha wanawake Weusi kisa wanawake weupe. Lakini hivi sasa, imekuwa
tofauti, na Kanye West ana Mke Mweupe na Gold Digger ambaye ni Kim Kardashian.
Related Posts :
SUGE KNIGHT: NAMSHTAKI DR DRE KWA KUNITUMIA WATU WA KUUA.
Na Baba Juti
MENGINE yameibuka na kuzidi kumuweka Dr Dre katika Wakati
Mgumu ambapo hivi sasa amefunguliwa Mashtaka ya Kutaka kuua.
SUGE KNIGHT ambaye alikuwa Mkuu wa DEATH LAW ambaye hivi
sasa yuko anatumikia Kifungo chake Jela, amedai kuwa anafungua mashtaka dhidi
ya aliyekuwa Swahiba Wake, DR DRE kwa madai kuwa amekuwa akijaribu kumuua
kwa kumchora kwenye michongo ya kuuawa mara kadhaa na watu ama na mazingira
tatanishi.
Kwa Mujibu wa File la Mashtaka ya SUGE KNIGHT ambaye pia
anatuhumiwa kuhusika kwa asilimia fulani katika kifo cha Marehemu Tupac,
inasemekana kuwa, sababu ya DR Dre kutaka kumuua, ni baada ya kutaka kumdhurumu
asilimia zake za mapato katika BEATS BY DRE ambazo zilinunuliwa kwa mkwanja mnono
na Kampuni ya APPLE
Kwa mujibu wa Mkataba ambao upo mpaka hivi sasa, ni
kwamba Dre alitakiwa kumlipa 30 ya mavuno katika masuala ya burudani, lakini
ikaja kusemekana kuwa, Dr Dre alihitaji kusitisha makubaliano hayo baada ya
Apple kutokuhitaji kufanya kazi na SUGE KNIGHT
Pia Maelezo ya kesi yanaongeza kuwa, SUGE anaamini kitendo cha yeye kupigwa Risasi
mara 7 nje ya Ukumbi wa 1 OAK katika Week ya BET Awards mwaka 2014, ilikuwa ni
Njama na maagizo ya Dr Dre.
Related Posts :
JAGUAR: BADO SIJAOA MPAKA HIVI SASA
Na Mwamba-Kenya
AKINA dada mnaweza kuchangamkia Hii Tenda aisee !!!!
LICHA ya kufanikiwa Kimuziki na hata kumiliki mkwanja
mzuri ambao unaweza kumfanya yeye na maisha yake yakawa katika mstari ulionyoka.
Kama ulikuwa hufahamu, licha ya kuwa na hayo yote , kumbe
mpaka hivi sasa Jaguar hajaoa, na hiyo ni kwa mujibu wake yeye mwenyewe
Kupitia Facebook fan page yake mwenyewe, JKaguar alijibu
swali akidai kuwa, mpaka hivi sasa hajaoa, hivyo hawezi kuonesha au
kumzungumzia mwamke ambaye hayuko naye au ambaye hajamuoa.























