Video making ya wimbo huu imefanyika
chini ya director EDDYSON wa Creative Mind Tz. Utengenezaji wa video hii
umekamilika tar 27/4/2014...... video hii inategemewa kutoka mapema mwezi ujao
kabla mwezi wa 6
STAY CONNECTED na TTM ili kufahamu Video Hii iko Vipi. Ni Noumar Mazee...Pia Soon Tutakuletea TEASER ya Video hii kutoka kwa Msanii THE KISSER-STRAWBERY
WAZINZI, WEZI, KUNA ADHABU YENU IKO HAPA
Serikali ya Brunei
iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.
Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni
jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki
hii.
Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni
pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na
hatia ya kushiriki Zinaa.
Sheria hii itatekelezwa katika awamu tatu katika
kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake
kuhusu sheria hiyo.
Taifa la Brunei tayari linafuata sheria kali za
kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na Indonesia pamoja na
kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe.
Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha
Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah na imepata utajiri wake kutokana
na kuuza nje mafuta na gesi yake.
Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika nchi
hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza
ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha
wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.
Sheria yenyewe itaanza kutumika katika kipindi
cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa ya kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja
na kutozwa faini.
Katika awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza
kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia ya wizi , huku awamu ya tatu
ikihusu kupigwa mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Sultani anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa
matajiri wakubwa duniani na tayari amewaonya watu kukoma kushambulia mipango
yake kupitia mitandao ya kijamii.
Umoja wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha
mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo inaambatana na sheria za kimataifa
kuhusu haki za binadamu.
Related Posts :
RIPOTI YA KITENGO CHIMBUA CHIMBUA-UGOMVI WA P SQUARE UMEZUA MAKUBWA MAWILI
KWA MUDA wa Wiki Kadhaa, Ishu ya Kugombana kwa
Ndugu watatu, PETER,PAUL (P SQUARE) na JUDE OKOYE ambaye ni kaka yao, Zimkuwa
Zikivuma sana Huku na Kule, huku baadhi wakibaki kustaajabu kuhusu Mtiti Huo.
CHANZO ambacho kilidaiwa Kuwakosanisha watatu
hao, ni pamoja na Mke wa Peter, anayefahamika kwa jina la LOLA, ambaye huwa
hana maelewano mazuri na JUDE
Lakini baada ya Info hizo kuzagaa kila kona na
kuwaacha watu wakiamini ule Msemo wa NDUGU WAKIGOMBANA, BEBA JEMBE KALIME,
Hatimaye yakazuka Mengine kuwa huenda wawili hao wakapigana Chini, huku Judee
ambaye amekuwa kama Meneja na Director wa Video za kwa Miaka 10, akitweet kuwa
anaachana na Shughuli hizo ikiwa ni baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu
Kiujumla Kitengo hiki amininfu kilipata Info nyingine
kuwa, kampuni ya Simu za Mkononi iliyokuwa ikifanya nao Kazi, ilikuwa na Mpango
wa Kumwagana na P-SQUARE endapo Watashindwa kufikia Muafaka, na Kundi hilo
kuvunjika kama sio Kusambaratika.
Baada ya Siku Kadhaa, hatimaye zikaibuka Details
Nyingine kuwa, watatu hao wamemaliza Ugomvi wao na Kila Kitu Kiko sawa, huku Jamaa
ambaye ni Mtoa Taarifa wa Kundi Hilo (PUBLICITY) akifungua ukurasa Mwingine kwa
kudaiwa kuwa ETI alisema ishu hiyo haikuwa ni ya Kweli, bali ilikuwa ni SKENDO
ili kutambulisha Ujio Wao mwingine, jambo ambalo jamaa mwenyewe amelipinga
SASA Basi….Baada ya hayo Kuvuma, hatimaye
KITENGO kimebaini kuwa Ugomvi Ule Umesababisha mambo Makuu Mawili yafuatayo:
1.
WAMEONGEZA NGUVU MPYA KATIKA KAZI
ZAO
Tofauti hizo ambazo zinadaiwa
kuwa ni Kweli zimetokea (kwa Mujibu wa Peter) hakika zimewapa nguvu kubwa sana
ya kufanya kazi mpya, tena kwa bidii za dhati. Peter amedai kuwa wanatarajia
kumimina kazi kibao Mpya.
2.
WAMEPATA MZUKA WA KUPIKA VIDEO YA
TESTMONY
Ili kudhirisha kuwa Hakuna baya
Linaloendelea baina yao, Peter amepost Tweet ikisema kuwa watu wanatakiwa
kusikilizia video lao la TESTMONY, huku akipost Picha za Behind The Scene….
Related Posts :
MAFIKI ZOLO WAMEMFUATA DAVIDO NIGERIA.
WASHINDI wa Tuzo 8 Za Muziki Nchi Afrika ya
Kusini, MAFIKI ZOLO, wamefunga Safari kuelekea Nchini NIGERIA kumfuata Mtu
Mmoja tu, ambaye wanaamini ana kitu kwao, DAVIDO
TTM Tumeunyaka Mtonyo huu kutoka Nchini Nigeria,
baada ya kuzinyaka Picha zao wakiwa katika Jiji la Lagos ambalo huwa halipatikani
sehemu nyingine zaidi ya NIGERIA.
Unaweza kujiuliza kuwa Sababu ambayo imewafanya
kumfuata Davido Nchini humo, lakini bila kupoteza Time, TTM tumeinyaka pia, na
sababu yenyewe ni Kutambulisha Ngoma ambayo Wamefanya pamoja na ilipikwa Huko
kunako studio za Afrika ya Kusini..
Kwaju ambalo linatarajiwa kuzinduliwa na Vichwa
Hivi pamoja na Davido, Linafahamika kwa Jina la TCHELETE, na wamesema kuwa
wanatarajia makubwa sana kutoka kwa wadau wao wa Muziki.
Pia Wameongeza kiuwa, wamefurahi sana kutua
LAGOS, sambamba na kufanya Kazi na DAVIDO, ambaye wote kwa Pamoja watakuwa naye
Kunako TUZO za MAMA













.jpg)







