WASTARA: KUNA MAKUNDI YALIKAA NA KUSEMA WASTARA HAUMWI, ANACHANGISHA TU PESA (AUDIO)
Na Rich Sam & Global Publishers
WENGI tunafahamu kabisa kuwa Msanii katika Ulimwengu wa Filamu za kitanzania , WASTARA JUMA siku kadhaa alilalamika kuwa Mguu wake ambao ulipata ajali na kukatwa, ulikuwa na matatizo mengine ambayo aliyafafanua na tuliweka wazi pia kupitia harakati zetu za kukuhabarisha
Lakini baada ya Wadau mbali mbali kujitokeza na kutoa michango yao, hatimaye Wastara amejitokeza tena na kuweka wazi huku akiwashukuru sana kwa kujitoa katika kupigania afya yake, kwa hali na mali.
Pia weastara hakusita Kutoa Kiwango cha Mkwanja ambao mpaka hivi sasa umeshapatikana sanjari na kiwango ambacho kimebakia, kama anavyosikika hapa
Tofauti na hayo, Wastara pia ameweka wazi kuwa, kumekuwa na makundi ya Wasanii mbali mbali ambao wamekuwa wakisambaza taarifa negative kuwa yeye haumwi bali anachangisha watu fedha kwa ajili ya matumizi mengine kitu ambacho amekikanusha kabisa, kama anavyosikika hapa
AUDIO : RICH HOMIE QUAN ADAI KUWA MZIKI WA KENDRICK LAMAR NI WA KUFANYIA MAZOEZI, HAUWEZI KUPIGWA CLUB
Na Rich Sam
SIJUI kama kauli hii itawakwaza mashabiki wa Rapper KENDRICK LAMAR ama lah, lakini huu ndio mtazamo wa Rapper Mwenzake anayefahamika kwa jina la RICHIE HOMMIE QUAN ambaye naye pia yupo kama hayupo katika Game
Rich Homie Quan, ambaye aliwahi kuutikisa ulimwengu na "Mkwaju" wa TYPE OF WAY, amedai kwa Nyimbo za Kendrick Lamar ni maalum kwa ajili ya kufanyia mazoezi, na wala huwezi kukuta zinapigwa sehemu nyingine tofauti
Ukiachilia mbali Kufanya mazoezi tu, Rich Hommie Quan amedai kuwa mazingira anayotokea, yaani katika kitaa chake, Mikwaju kama ya Kendrick Lamar huwa haikubaliki sana, na hata ukiingia Club huwezi kukuta inapigwa hata kidogo
Kwa upande wake yeye, sio kwamba hakubali mizigo na style ya Kendrick Lamar, ila huwa anaisikiliza akiamka asubuhi, lakini hawezi kui-feel akiwa Club

