Sudan kusini imefutilia mbali mazungumzo ya amani yaliokuwa
yafanyike kati yake na Sudan Kaskazini huku ikiishutumu nchi hiyo kwa
kushambulia moja ya miji yake karibu na mpakani.
Msemaji wa jeshi Kanali Philip Aguer jana alisema kulikuwa na
shambulizi la bomu katika eneo la Rubaker.
Aguer alisema mabomu
takriban manane yalirushwa katika eneo hilo na ndege za kijeshi za
Sudan na kuwajeruhi watu wawili.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
Mzozo wa mafuta na maswala ya mipaka kati ya nchi hizo mbili
umendelea baada ya Sudan Kusini kujitenga na Sudan mwaka mmoja
uliopita.
Habari hii ya mashambulizi inakuja takriban wiki mbili baada ya
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhimiza mataifa hayo
mawili kusuluhisha tofauti zao kabla ya tarehe 2 Agosti ambao ndio
muda wa mwisho uliowekwa na umoja huo kwa mataifa hayo
kuelewana.
Related Posts :