UTAFITI: MTUMIAJI WA POMBE ANAWEZA KUJIFUNZA KUTUMIA LUGHA NYINGINE (YA KIGENI) KWA UFASAHA ZAIDI
Na baba Juti
UCHUNGUZI umefanyika na kubainika Kuwa Unywaji wa Pombe unaweza kumfanya Mtu akazungumza Lugha za mataifa Mengine
Uchunguzi huo umebaini kuwa, unywaji wa Pombe kiasi fulani (hasa Kidogo) kinaweza kumfanya Mtumiaji akawa na ujuzi wa Lugha Nyingine hasa kutoka mataifa Mengine
Team ya Utafiti Kutoka Liverpool Uingereza, Vyuo Vikuu vinavyofahamika kwa Majina ya MAASTRICHT UNIVERSITIES, Na KING'S COLLEGE zilitoa taarifa kuwa, unywaji wa Pombe husababisha athari ama hudhuru sehemu kadhaa za binadamu ikiwemo Nguvu ya Kufanya kazi kwa Ubongo, na Nguvu ya Mwili.
Tofauti na hayo, Ilidaiwa kuwa kupoteza kumbu kumbu, kukosa nguvu na uwezo wa Kufikiria, lakini pia uvivu wa kimwili, husababishwa na Unywaji wa Pombe
Ila sasa, kuna faida mpya ambayo imebainika safari hii, kuwa kunywa Pombe kunaweza kumfanya Binadamu akatumia Lugha zaidi ya Moja hasa zile kutoka Nje ya Nchi ambayo binadamu husika anatumia Lugha yake Mama au ya kitaifa.
Pia watafiti hawa Wapya wameongeza kuwa, Pombe hujenga Ujasiri Binafsi kwa Mtumiaji na hata kutumia Fursa hiyo kuzungumza na mwenzake ama wenzake ama Wenyewe Lugha Nyingine za Kigeni zaidi kuliko hata Lugha yake Mama
Hivyo, kwa utafiti wa Awali, imegundulika kuwa, Mtumiaji wa Pombe kwa kiasi fulani, hata kama hajui, huweza kukusanya hata maneno mawili matatu licha ya kuchapia katika lugha ya kigeni, lakini atazungumza na kueleweka kwa kiasi Fulani
Pia Mtumiaji wa Pombe, hupendelea mara kwa mara kutumia Lugha Nyingine tofauti na ile ambayo huizungumza siku zote katika Majukumu yake ya kila siku
Mmoja kati ya Watafiti, Dr. Inge Kersbergen kutoka Chuo Kikuu cha Liverpool, taasisi ya Saikolojia, Afya na Jamii alisema Hivi, tunamnukuu
" Utafiti wetu unaonesha kuwa unywaji wa Pombe, unaweza kuwa na manufaa katika kutamka maneno ya Kigeni hasa kwa wale ambao anagalau wameshajifunza Lugha hiyo. Hii pia husaidia ama huleta faida ya kujifunza zaidi hasa ukiizungumza ukiwa na wale ambao wanaifahamu lugha husika kwa ufasaha zaidi"
SIKU YA HESHIMA DUNIANI: VANESSA MDEE ANASHUKURU KUIMALIZA VIZURI NA WANAFUNZI WA AGAKHAN MZIZIMA SECONDARY SCHOOL (PICHA)
Na Insta Cop
SIKU ya jana, October 18, ilikuwa ni Siku ya Heshima Duniani (Global Dignity Day) ambayo hufanyika Kila Mwaka katika Mataifa Mbali mbali
Lakini kwa Mwaka huu, Mahali fasaha pa kuiadhimisha , ilikuwa ni katika Shule mbali mbali Duniani, ili kutoa hamasa kubwa na heshima kubwa kwa wanafunzi mbali mbali ambao wamekuwa wakijituma zaidi katika masomo na malengo yao ya Baadaye.
VANESSA MDEE, maarufu kama Vee Money, alikuwa katika Shule ya AGA KHAN MZIZIMA SECONDARY SCHOOL iliyoko Dar Es Salaam kwa ajili ya kujumuika na wanafuzni wa Shule Hiyo
Hivi Ndivyo ilivyokuwa
Related Posts :
NICKI MINAJ: "NITATOA $ 100,000 KWA ATAKAYENIPA USHAHIDI JUU YA HILI"
Na Rich Sam
WAUNGWANA wameamua kumfanya Nicki Minaj apate Hasira za kutosha mpaka kutangaza Dau la USD 100,000 kwa yeyote atakayempatia Ushahidi ambao mpaka hivi sasa umemuweka katika wakati mgumu hapa Duniani aisee
Hitmaker Huyu wa "ANACONDA" alijikuta akimiminiwa "Ndimu" za Kutosha ikiwa ni baada ya kudaiwa kuwa aliropoka kwamba yeye ndiye kawafanya Wasanii Wote wa Rap kwa Jinsia ya Kike wawe katika Ramani ya Muziki, kitu ambacho kwa upande wake amekikanusha na kuamua kuandika walaka Mrefu sana kupitia Instagram account Yake.
Katika Post alioipost bibie huyu baada ya kukutana na janaga hilo, aliandika kuwa, anahitaji kuweka sawa kuhusu kauli hiyo ambayo imenukuliwa Tofauti na Mitandao ya Kijamii na Tv Station mbali mbali, huku akimtaka yeyote yule atakayeona "nukuu" hiyo, basi amcheki na kumpatia USD 100,000.
Tunamnukuu tafadhari
NICKI MINAJ
"Ninanona Watu wana-remix maneno yangu, hivyo ngoja nipost kile nilichokisema haswa kwa wale ambao wana uelewa. Sasa, kama utapata Sehemu ambayo nilisema "Nimewafanya Rappers wa Kike kuwa katika Main Stream", nitakupatia USD 100,000. Blogs na Tv shows mbali mbali huwa hawajalishi utafiti, huwa wanajali kuchukua hisia zako. Hebu fikiria mie kusema nimewaweka katika Ramani ya Muziki rappers wa Kike wakati kuna wengi ambao tayari walishaingiza albums zao Platnum kupitia Nguvu zao. Lauryn mpaka nakala Milion 10 ya moja kati ya Albam zake. Eve alikuwa na Nyimbo zilizogusa Pltnum akiwa na Alicia Keys, Gwen Stefani, Tv Show yake na Mavazi yake, Missy Eliot Pia Nyimbo zake. Foxy Brown na Lil Kim walikuwa Album ambazo ziliingia Pltnum na walitengeneza vizuri Sound ya Wasanii wa Kike wanao Rap kutoka New York. Akina Queen Latifah, Trina naye alikuwa na Album ambayo ilifika mpaka Billboard. Ninapenda sana upendo wa watu lakini sijawahi kusema hivyo.........."
Related Posts :
MAHABA NIUE !!!: JENNIPHER LOPEZ ANAUZA NYUMBA YAKE KWA SABABU ANAHITAJI KUISHI PAMOJA NA ALEX RODRIGUEZ
Na Baba Juti
JENNIFER LOPEZ kwa Kinywa Chake alitamka Rasmi kuwa mahusiano yake na Alex Rodriguez ndiyo mahusiano yake Ya Kwanza kabisa kufurahia, na hilo limeanza kuthibitika rasmi.
Mahusiano hayo ambayo yameanza mwaka huu wa 2017, yanaonekana kupiga hatua nzuri kadri ambavyo siku na Muda unavyosonga Mbele mpaka kufikia maamuzi ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyafanya.
Jennifer Lopez anasadikiwa kuiweka Sokoni Nyumba yake ya Kifahari iliyoko NEW YORK Marekani hivi sasa, maana anahitaji kuishi Pamoja na Mpenzi wake huyo Alex Rodriguez.
Taarifa zinazidi kumiminika kuwa, Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona kuwa kuna uhitaji mkubwa wa wawili hao kuanza kuishi pamoja na kuanza kutekeleza Mipango yao Muhimu zaidi katika Maisha yao, Mapenzi yao, na Kazi zao
Tofauti na Hilo, wawili hao wanatajwa kuwa, wako katika Harakati za kuwekeza pamoja katika Biashara zao za pamoja ambazo zitazidi kuwaweka imra katika Mahusiano na maisha yao kiujumla
Related Posts :
NDOA YA BIRDMAN NA TONI BRAXTON HAIPO WAUNGWANA JAMANI !!!!!
Na Baba Juti
#WatuWaMungu kumekuwa na Taarifa ambayo Pia kupitia Sehemu kadha wa kadha zimekuwa zikizungumzwa sana kuhusu "ndoa" ya wapenzi wawili BIRDMAN na TONI BRAXTON ambayo inadaiwa kuwa ni Ya Siri na ilifungwa Miezi miwili iliyopita.
Taarifa hizo pia zilitolewa na chanzo aminifu kabisa ambacho kipo karibu na "wapenzi" hao kwa kudai kuwa Birdman hakutaka kabisa Ndoa yao ijulikane ingawa wapo mbioni kuandaa Sherehe yao maalum hivi karibuni ikiwa ni njia ya kujitangaza Rasmi kuwa tayari ni Mke na Mume
Sasa Siku ya Jana, Taarifa Nyingine zimeibuka na kukana kabisa kabisa kabisaaaaaa !!!...kuwepo kwa Ndoa ya Birdman Na Toni Braxton
Msemaji Maalum wa Toni Braxton alidai kuwa Bibie huyo hajasema "I Do" kwa Rapper Huyo Mkongwe na Mwenye "Mkwanja" mrefu, ila Bado wanadate tu.
Katika kuongezea juu ya hilo, Msemaji huyo alisema kuwa hivi sasa Toni Braxton ana mkwaju unaoitwa "DEAD WOOD" ambao utatoka kwenye Album yake mpya ya SEX & CIGARETTE itakayoachiwa Rasmi 2018
Related Posts :
MNAONAJE !!!: HUU NDIO MUONEKANO MWINGINE WA BARAKA THE PRINCE KATIKA SEKTA YA KICHWA
Na Rich Sam
#WatuWaMungu Hakuna Mtu ambaye anapenda kuwa na muonekano wake huo huo tangu alivyoanza ama kwa muda fulani, lazima tu atabadili kidogo ili awe tofauti.
Hii tumekuwa tukiiona kwa wasanii wengi sana hapa Duniani wakifanya hivyo, ili angalau kuwa na mvuto wa aina fulani katika mwili wake na hata katika biashara yake kiujumla
Nchini Tanzania katika Muziki wa "Bongo Flava" kuna wasanii wengi ambao hubadili muonekano wao mara kwa mara, Mfano Mzuri ni Young Dee, Diamond Platnumz, Janjaro, Harmonize, Young Killer, na wengine wa kutosha
And This Time, Msanii ambaye Origin yake ni MWANZA, Barakah Da Prince au "The African Prince" naye pia katuletea Muonekano wake Mpya kichwani. Kama hujauona, basi hebu utizame tafadhari
Related Posts :
HUDDAH : "NIMEKUWA TOM BOY KWA SABABU............"
Na Baba Juti
#WatuWaMungu Socialite kutoka Nchini Kenya, HUDDAH MONROE maarufu kama "Huddah The Boss Chick- Star Girl" ameamua kufunguka upande wake mwingine wa maisha ambao pengine wengi walikuwa hawaufahamu
Kupitia Instagram account Yake, Huddah amedai kuwa, huwa hapendelei kuvaa Magauni kwa sababu huwa hapati nafasi ya kujiachia tofauti na namna ambavyo huwa anajiachia akiwa amevalia Suruali ama Kaptula.
Katika kukazia zaidi, Huddah tangu awali alikuwa akipendelea kuvaa mavazi ya kiume na hata kuitwa TOM BOY kwa sababu hajawahi kuwa na Dada. Hivyo muda mwingi alikuwa akiutumia kuwa na kaka zake, na hata kucheza michezo ya kiume na kaka zake, na ndio maana huwezi kumuona akujitupia mavazi ya Gauni mara kwa mara.
A post shared by STAR GAL 💥 🇰🇪 (@huddahthebosschick) on










