MKUBWA FELA: "ASLAY MWENYEWE HAJANITAFUTA, SIWEZI KUAMINI MAMBO YA MITANDAONI !!!"
Na Rich Sam
#WatuWaMungu Kuvunjika kwa Mahusiano ya Aslay na Mzazi mwenzake Tessy Abdul Maarufu kama Tessy Chocolate yamekuwa ni moja kati ya mazungumzo makubwa sana kunako mitandao ya kijamii
Hali hiyo imewafanya wengi ambao walikuwa wakifuatyilia na kuenjoy mahusiano ya wawili hao kwa ukaribu, wajiulize maswali mengi vichwani mwao hasa kuhusu sababu kubwa iliyowafanya wawili hao wabwagane chini
Ukiachilia mbali watu wengine kuwa na Maswali, hata aliyekuwa Manager wa Aslay ambaye pia ni kama mlezi kwake, Mkubwa Fella, naye anashindwa kujua ni kipi ambacho kinaendelea kati ya wawili hao kiasi cha kufikia maamuzi hayo ilihali wana mtoto mdogo anayeitwa MOZAH
Katika Suala la kuwapatanisha kama ilivyo kwa Wengine, Mkubwa Fella amedai kuwa yeye mpaka muda huu hajaitwa kutoa ushauri ama kuelezwa tatizo ni nini, hivyo kama ataitwa, basi atafanya hivyo maana hata Aslay mwenyewe hajampigia simu bado
#AnotherOne : SIKIA HII MPYA KUTOKA KWA RJ THE DJ AKIWA NA LYDIA BROWN-TONIGHT
Na Baba Juti
GOOD MORNING Tanzania !!!!. Project za Romy Jons a.k.a RJ THE DJ still zinaendelea ikiwa ni baada ya kuachia Project yake ya BORA IWE ambayo amemshirikisha Barakah The Prince.
This time, RJ ameshusha Brand New Song ambayo inafahamika kwa jina la TONIGHT na amemshirikisha Bibie mwenye sauti yake-LYDIA BROWN
Check It Out !!!!
Related Posts :
SHABAAAAAASH !!! : KANYE WEST KAPONEA CHUPUCHUPU !!!!
Na Rich Sam
#WatuWaMungu ilikuwa Bado kidogo tu Rapper Kanye West akutane na Kesi ya madai na kutakiwa kulipa zaidi ya USD 50,000 baada ya kusababisha usumbufu, lakini maamuzi yaliyotoka, yanaweza wanyima Rappers wengine uhuru wa kujiachia.
Kanye West alikuwa na shughuli ya ALBUM LISTENING PARTY katika eneo la WYOMING, ambalo hufahamika sana kwa kutokuhusishwa na watu wenye ngozi nyeusi, na alikuwa na timu ya watu wengi sana kwa ajili ya shughuli hiyo.
Kwa Mujibu wa mmiliki wa eneo hilo, JANE GOLLIHER, Kanye West alikodi eneo hilo lakini kwa makubaliano ya kufanya shughuli hiyo upande wa Ndani, yaani IN DOOR, lakini Rapper huyo alikuwa akibadili maamuzi kila baada ya Dakika 30, hali ambayo ilipelekea afanye shughuli hiyo Upande wa Nje
Mmiliki huyo anaongeza kuwa, Kanye alichukua uamuzi wa kufunga Speaker nyingi na kubwa katika eneo la uwazi, yaani nje na kuachia Bash la aina yake huku akisababisha usumbufu kwa Watu waliokuwa eneo la Jirani hasa Lodge mbali mbali zilizokuwa zina watu waliokuwa wamepumzika
Pia mmiliki huyo akadai kuwa, alikuwa akipigiwa simu za malalamiko mara kwa mara, hali iliyomfanya amtafute Kanye West ambaye aliahidi kumaliza Shughuli hiyo majira ya Saa Nne Usiku ili kuwaacha watu wa Pumzike, lakini cha ajabu bata hilo lilianza Majira ya Saa tatu za Usiku.
Hata Hivyo amemaliza kwa kusema kuwa, hana Ugomvi na Kanye West maana angemtoza faini ya USD 50,000 ama zaidi, lakini hatoruhusu Rapper yeyote afanye shughuli yake katika eneo lake
Related Posts :
KUTANA NA MWANAMKE AMBAYE AMEFANIKIWA KUPANDIKIZWA UKE KWA NGOZI YA SAMAKI, BAADA YA KUISHI BILA "UKE" KWA MUDA MREFU
Na Rich Sam
HAKIKA Mungu atabaki kuwa Mungu na hakuna namna ya kushindwa kumuita Mungu na kuheshimu jina lake kwa muujiza huu alioutenda, japo ni kupitia kwa Binadamu.
Unaweza ukazaliwa Bila matumaini ama ndoto ya kupata kiungo fulani muhimu katika mwili wako, lakini ikafikia muda, watafiti na wataalamu kadha wa kadha wakabaini ni namna gani ambavyo wanaweza kufanya hivyo ili kukuweka sawa.
Hii tumekuwa tukiiona katika matukio mbali mbali, Mfano, mtu ahana mguu, lakini anawekewa mguu mwingine, mtu hana jicho, mkono, pua, sikio, lakini wataalamu wanafanikiwa kulifanya.
JUCELINE MARINHO, Binti kutoka Nchini Brazili, mwenye umri wa miaka 23, ambaye alizaliwa bila "Uke", hatimaye amekuwa ni binadamu wa kwanza Ulimwenguni hasa Mwanamke, kupandikiziwa Uke hasa kwa kutumia Ngozi ya juu ya Samaki.
Bi Marinho amekuwa katika hali hiyo ya kukosa hasa viungo muhimu kama vile Ovari na Kiungo muhimu katika kizazi maarufu kama Cervix kwa kitaalam zaidi.
Utaratibu wa kumsaidia binti huyu ulianza ikiwa ni baada ya kubainika kuwa ana mampungufu mnamo April Mwaka jana, hali ambayo ilimfanya ashindwe kupata mtoto na hata kufanya tendo la ndoa, kitu ambacho kilimuumiza kwa asilimia kubwa
Lakini baada ya kupatikana kwa wataalamu kutoka FEDERAL UNIVERSITY OF CEARA huko huko Brazil, ilibainika kuwa tatizo hilo linaweza kusaidika kiurahisi zaidi kwa kupandikiza Ngozi ya samaki (Ile yenye magamba) katika njia za ndani za uke wake ambazo zitamuwezesha kushiriki tendo la Ndoa bila tatizo na hata kufanya jitihada za kunasa ujauzito
Hata Hivyo, Baada ya kufanyiwa Zoezi hilo kwa Takriban wiki tatu Hospitali bila kutoka, Bi Marinho amefanikiwa kufanya Tendo la Ndoa kwa mara ya kwanza na Boyfriend wake MARCUS SANTOS (24) ambao tangu waanze mahusiano katika mwaka mmoja, hawakuwahi kufanya hivyo
TUNAMNUKUU
"ilikuwa ni muda mzuri sana kwa sababu kila kitu kilienda sawa, hakukuwa na mamuvu hata kidogo, na nilifurahia sana na kuburudika Sana
Kwa kinywa chake mwenyewe, Marinho amesema kuwa anafurahia sana kuwa na UKE, kiungo muhimu sana ambacho kila mwanamke yeyote yule duniani, hujivunia kuwa nacho...
Alisema hivi...
"Familia yangu ilinitoa OUT, na kusherekea mimi kufanikiwa kuwa na Uke"
PICHA ZAIDI
Related Posts :
HANGOVER MONDAY: HAIKUWA WEEKEND NZURI KWA MTOTO WA LIL WAYNE , REGINAE CARTER NA BOYFRIEND WAKE BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI
Na Baba Juti
IKIWA leo ni Jumatatu, Kupitia Weekend kuna matukio mazuri na mabaya ambayo yalitokea, ila kubwa zaidi, ilikuwa ni hili la Mtoto wa Rapper Lil Wayne na Boyfriend wake kulambwa na Pingu walipokuwa katika moja ya kiwanja cha Bata huko Nchini Marekani.
Reginae Carter (Binti wa Lil Wayne na Toya Wright) mwenye miaka 19 akiwa na Boyfriend wake YFN Lucci mwenye miaka 27 ambaye pia ni Rapper, walikutana na noma hilo Usiku wa kuamkia Jumamosi walipokuwa maeneo ya KNOXVILLE, TENNESSE, Marekani ambako YFN alikuwa meenda kwa ajili ya shughuli ya Special Appearance
Ingawa haijawekwa wazi chanzo cha tukio hilo ni nini, lakini Camera ziliwansa wawili hao wakibishana na Polisi waliokuwa katika eneo la tukio, hali iliyosababisha kutiwa pingu na kupelekwa kituo cha Polisi cha Knoxville na kuwekwa ndani kwa masaa kadhaa
Pia baada ya muda kidogo, Binti huyo wa Lil Wayne alipost kupitia instagram account yake akidai kuwa yuko sawa na hayupo jela.
Mpaka hivi sasa taarifa rasmi kuhusu kukamatwa kwao hazijawekwa bayana ingawa wengi wanaamini inawezekana kabisa kulikuwa na kutokuelewana baina ya YFN Lucci na waandaaji wa Show hiyo.
Wawili hao walianza kutajwa kuwa na mahusiano mapema mwaka huu ingawa Reginae Carter alikuwa akikanusha uwepo wa mahusiano yao, lakini hivi sasa mambo yako hadharani
Related Posts :
MAMBO YAMEKUWA MABAYA : RAPPER T.I ANAOMBA KESI YAKE NA KAMPUNI YA INAYOMDAI...ITUPILIWE MBALI !!!!
Na Rich Sam
#WatuWaMungu Rapper T.I ameamua kupinga mashtaka ya kukatisha mkataba na kutokulipia "vito" vya thamani a.k.a "Bling Bling" za moja kati ya kampuni ambayo ilifungua mashitaka dhidi ya Rapper huyo.
KAMA ULIKUWA HUFAHAMU.....
Wafanya Biashara wakubwa wa Vito hivyo vya thamani AYDIN & CO ambao huuza vitu kama vile cheni, saa Heleni kwa Watu maarufu wenye majina nchini Marekani, mwaka 2015 walifungua Kesi dhidi ya Rapper T.I kwa madai kuwa Hit Maker huyo wa WHATEVER YOU LIKE alikiuka makubaliano yao ambayo yalikwekwa kwa njia ya mazungumzo (Oral Agreenment) kuhusu yeye kuchukua na kutumia vito hivyo vya thamani, na tayari alikuwa hajalipia takriban USD 775,000 ya vitu ambavyo alichukua kwa wafanya biashara hao
Katika Madai yao, Kampuni hiyo inadai kuwa kati ya mwaka 2004 na 2012, walimuuzia T.I Bling za kiasi cha Maelfu ya Dolari za kimarekani ikiwema Heleni za madini ya Diamonds zinzogharimu USD 9500, Cheni yenye madini ya Diamonds inayogharimu USD zaidi ya 9000, Cheni aina ya DOG TAGS zinzogharimu USD 10,000, Cheni ya Mkononi ya kike yenye madini ya Diamonds inayogharimu USD 24,500, Saa ya Madini ya Diamonds yenye rangi ya Blue inayogharimu USD 30,000 pamoja na pete ya ndoa ya kiume inayogharimu USD 13,000
KINACHOENDELEA
Sasa, baada ya kukutana na mashtka hayo na kesi kusikilizwa May 18, T.I ameiomba mahakama kupuuza na kutupilia mbali mashtaka hayo dhidi yake maana hakuna ukweli wowowte ndani yake, bali wanataka tu kufaidi kupitia yeye
Hata hivyo, mmiliki wa Kampuni hiyo, FEVZI AYDIN alidai kuwa, Kampuni yake pamoja na T.I walifungua akaunti maalum kwa ajili ya malipo, na T.I alikuwa akilipa mpaka Mwaka 2013 ambapo aliacha ghafla kulipa mkwanja huo.
Kesi hiyo imeahirishwa na kusikilizwa tena mpaka mwisho wa kipindi cha Joto
Related Posts :
JUNE 04TH : TAILOR'S DAY
DAYS OF THE YEAR
Tailors Day is a day where people are encouraged to dress their best and to reach out and thank the person that helps them achieve their high level of sartorial elegance.
While off-the-peg clothes may have become commonplace, even among some of the best dressed, the tailor still plays an integral part in ensuring some people look their best, and Tailors Day is the day to thank them.
There is no doubting the skill of a good tailor. They can create the perfect outfit, for any event, and can make even the most casual dresser appear elegant and attractive. It stands to reason, therefore, that they should be properly celebrated.
Arguably the best way to celebrate the day, and to show thanks, is to wear a suit or outfit that was professionally tailored to fit. However, some people that are especially grateful choose to buy cards and even gift baskets for their tailors.
Arranging for a new suit could be considered an appreciable means of showing love for a tailor, because it means that they will be enjoying new custom and the sale of their skilled service.















