WATU 9 WAUAWA MADAGASCAR





Na Frank M. Joachim

Habari kutoka Madagascar zinaarifu kuwa, watu 9 wameuawa katika mapigano yaliyozuka kati ya polisi na watu wenye silaha kusini mwa nchi hiyo. 

Duru za habari zinaaru kuwa, 6 kati ya watu hao waliouawa walikuwa miongoni mwa wanachama wa kundi hilo lililokuwa na silaha, huku wengine 3 wakiwa wakiwa wanajeshi. Hadi sasa makumi ya watu wamekwishauawa katika ufyatulianaji risasi kati ya wanajeshi na watu wenye silaha ambao wanajihusisha na wizi nchini Madagascar. 

Ni vyema kuashiria hapa kwamba, Madagascar imekuwa ikikabiliwa na hali ya mchafukoge tangu kulipotokea mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani rais wa nchi hiyo miaka minne iliyopita.  

Related Posts :