MASIKINI KENYA....


Na Frank M. Joachim.

Habari kutoka eneo la Tana River nchini Kenya zinasema kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye machafuko ya kikabila katika eneo hilo imepanda na kufikia 40.



 Maafisa 9 wa polisi ni miongoni mwa waliouawa kwenye ghasia hizo. Kitovu cha machafuko hayo ni katika kijiji cha Kilelengwani ambapo magari kadhaa ya polisi yamechomwa moto na vituo kadhaa kuharibiwa. Makabila ya Pokomo na Ormo yamekuwa yakipigania ardhi ya malisho kwa muda mrefu na mwishoni mwa mwezi uliopita mvutano huo wa ardhi uligeuka na kuwa mapigano ya silaha.

 Utulivu wa kiasi fulani ulirejea lakini mwanzoni mwa wiki iliyopita, machafuko hayo yakaanza upya. Habari zaidi zinasema mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye ghasia hizo.

Maafisa zaidi wa usalama wamepelekwa katika eneo hilo ili kutuliza hali ya mambo lakini wakazi wameilaumu serikali kwa kushindwa kuwalinda pamoja na mali zao.

Related Posts :