TUMPONGEZE AISEE !! : RICK ROSS NA MWANAMITINDO BRIANA CAMILLE WAPATA MTOTO WA KIKE


Na Baba Juti    
#WatuWaMungu kuna habari Njema na Tamu kutoka kwa Huyu mama ambaye tunafahamu kuwa ana ujauzito wa Rapper na Big Boss wa MMG, RICK ROSS

kama Utakuwa unakumbuka Vizuri sana, Wiki iliyokata tulikupa Taarifa kuwa, Mwanamitindo na Mtaalamu wa Maozezi Nchini Marekani BRIANA CAMILLE wanatarajia kupata Mtoto, baada ya bibie huyo kutoa Taarifa kuwa anatarajia kumleta Mwanafamilia Mpya.

Sasa kwa Taarifa ambazo WAUNGWANA tumezinyaka, ni kwamba BRIANA CAMILLE amefanikiwa kujifungua Mtoto wa Kike, tafsiri inayoweka wazi kuwa Rozay ni Baba kwa Mara Nyingine Tena

Taarifa hiyo ya kupatikana kwa Mtoto huyo, ilifahamika kupitia Instagram account yake Briana Camille, ambapo vilipostiwa Viatu vya Kike na kisha Briana kuandika kuwa "Tayari Baba ameshaanza Fujo Zake"
 
WAKATI HAYO YOTE YANATOKEA  
Licha ya Kupostiwa kwa hayo yote, Bado Rozay hajazungumza Chochote mpaka hivi sasa ambapo tunakupatia Taarifa Hii

Lakini kama ulikuwa hujui, Rick Ross hivi sasa yupo katika Mahusiano na Bibie anayefahamika kwa Jina la Liz Hagelthorn, ambaye ni Boss wa Mtandao wa Twitter.

Related Posts :