SORRY BIRDMAN & LIL WAYNE...ALBAM YA TYGA INASHUKA SOKONI DECEMBER


Black Touchez Editor/Hot New Hip Hop
TYGA amezidi kudhihirisha kuwa, Si Lil Wayne ama Birdman wanaweza kuendesha Maisha yake hasa katika Upande wa Kipaji chake.

Finally T Raw ametangaza rasmi tarehe ambayo albam yake itaachiwa rasmi na Kuingia Sokoni kwa ajili ya kufanya Biashara pamoja na kukata Kiu ya mashabiki wake ambao walikuwa wakimsubiri kwa hamu haswa.

Albam yake ya THE GOLD ALBUM, inatarajiwa kuingia Sokoni DECEMBER 23, huku ikiwa na Mikwaju kadhaa sambamba na 40 Mill ambayo ilipikwa poa na Kanye West na mkwaju mwingine MAKE IT WORK

Kupitia account yake ya Twitter, T-Raww akiwa ni “JESHI LA MTU MMOJA”, ameanza kupiga Promo juu ya Albam hiyo, huku kukiwa hakuna hata neon lolote kutoka katika Familia yake YMCMB ambayo imekuwa ikimsupport kwa muda kadhaa

Tyga aliingia katika Changamoto Nzito baada ya kuamua kuwalipua YMCMB kuwa wanambana hasa katika kuachia Project zake, huku akitishia kuvujisha Albam hiyo endapo haitoachiwa Mwaka huu.


Related Posts :