Afutiwa shitaka la kuuza nyama ya binadamu


Ngara.
Mahakama ya Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera imemfutia mashitaka ya kuuza nyama ya binadamu, Pastori Nalingi Blanketi (43) na kumhukumu mwaka mmoja jela kwa kosa la kuingia na kuishi nchini kinyume na sheria.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi wilayani Ngara, Tumaini Membi aliiambia mahakama hiyo kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa Februari 23 mwaka huu katika Kijiji cha Kihinga saa tano  usiku baada ya kunusurika kuuawa na wananchi wa kijiji hicho.

Membi alisema wakati anakamatwa, mtuhumiwa alikuwa akitangaza kuwa anauza nyama ya binadamu kwa Sh100,000 na baada ya uchunguzi ilibainika kuwa alitoa kauli hiyo akiwa amelewa, hivyo havikupatikana vielelezo vya kumtia hatiani kwa tuhuma hizo.

“Baada ya kuhojiwa kwa kina, ilibainika mtuhumiwa alikuwa katika hali ya ulevi wakati akitangaza biashara hiyo na hata hivyo, polisi lilimtia hatiani kwa kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria,” alisema Membi.


Mtuhumiwa anadaiwa kuingia nchini akitoka Burundi tangu mwaka 1981.

Related Posts :