MB DOG AMEWAHI KUVUTA MILIONI 10 KATIKA SHOW


MKALI wa Muziki wa KIzazi kipya Kipindi Hicho, MBWANA MOHAMED Maarufu kama MB DOG, amefichua hili ambalo tulikuwa hatulifahamu Kutoka kwake.

Swahiba Huyo ambaye alifanya vema sana Kupitia Mikwaju kadhaa kama vile LATIFA, INAMAANA, na Nyinginezo Kibao, amedai kuwa aliwahi kulipwa Kiasi cha Shilingi MILIONI 10 alipokuwa akipiga Show Moja katika Nchi ya Burundi

Tofauti na kulipwa Mkwanja Huo, MB DOG aliongeza kuwa, amewahi kulipwa Shows za Milioni Kadhaa, ingawa Wengi walikuwa hawafahamu kwasababu kipindi hicho hakukuwa na tabia ya Kutaja Viwango vya Fedha ambavyo Vinalipwa kutokana na Show, tofauti na Ilivyo hivi sasa, Kila Kitu kiko wazi.

Pia MB DOG ambaye ni Ex Memba wa Kundi la TIP TOP CONNECTION, ameongeza kuwa Show yake ya Kwanza alilipwa Kiasi cha Shilingi Milioni 3, huku Show ya Mwisho Ikiwa ni Milioni 10 za Kitanzania mnamo Mwaka 2006, ambayo ilikuwa ni maajabu kwake.


Lakini Mpaka Hivi sasa, Swali ambalo MB DOG anajiuliza, je Ni kweli anaweza Kupiga Show Yenye Mzuka na Watu Wengi huku akiingiza Mkwanja Mkali kama Kipindicho?

Related Posts :