CHRIS BROWN NA RIHANNA NI SIKIO LA KUFA


TTM Leo tumebaini kuwa Kumbe Chris Brown na aliyekuwa Mpenzi wake Rihanna, bado wako In Touch na Kuna Kila aina ya Dalili ya kurudisha mahusiano yao ya kimapenzi.

Kama utakuwa ni Good member wa TTM, jana tulikupa Mtonyo kuwa Drake anaweza kuwa ni Mwanaume ambaye anamfanya Rihanna afurahi, kumbe WaaaalaaaH, Rihanna anamchora tu Kijana wa Watu.

Chanzo Kilichopo karibu na Rihanna, kimedai kuwa Tangia Breezy atoke Rehab alikopiga Siku 90, ili kumsaidia kucontrol hasira zake, amekuwa akichat mara kwa mara na Chris brown , jambo ambalo Rihanna ameonekana kulifurahia kwa Kiasi Fulani.

Aidha chanzo hicho kimeongeza kuwa Breezy ameanza kumtext, yaani kumtumia Messeji Rihanna, tangu alipokuwa akisherehekea Birthday yake ya kutimiza miaka 26.

Tofauti na hilo, inasemekana kuwa RIRI ambaye ni Mkali wa DIAMONDS, awali hakujibu meseji za Chris Brown, lakini kadri Muda Ulivyokwenda, RIRI alipata hamasa ya Kumjibu na hatimaye kumwandikia maneno kama AHSANTE, na Kisha akamuuliza Chris Brown alikuwa akiendeleaje huko Rehab.


Katika Kuongeza hilo, Chris Brown na Mpenzi wake wa sasa Karrueche, hawako pamoja kama marafiki wanapatikana katika account ya Twitter, tofauti na ilivyokuwa Awali.

Related Posts :