POLISI AUWA NA KUCHUKULIWA BUNDUKI YAKE




Afisa wa polisi ameuawa kwa kupigwa risasi na bunduki yake kuibwa, katika shambulizi mjini Mandera karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Kwa Mujibu wa Taarifa zilizothibitika kutoka Nchini Kenya, imesemekana kuwa Afisa huyo wa Polisi alikuwa katika doria pamoja  na wenzake wakati waliposhambuliwa saa tatu usiku wa alhamisi, huku  mwenzake huyo akipona kuuawa  na pia hakujeruhiwa.

Maafisa wa polisi wanasema ujumbe uliopatikana kutoka kwa wanachama wa kundi hilo unaonyesha kuwa kundi hilo liko tayari kutoa shilingi 890 000 kwa kila mwanamgambo anayemuua afisa mmoja wa usalama wa Kenya.

Zaidi ya maafisa 20 wa usalama katika eneo la Kaskazini Mashariki wameuawa katika mashambulizi yanayoaminika kutekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab.

Related Posts :