10 WAHOFIWA KUFARIKI KENYA





Watu watano wameokolewa kufikia sasa baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababisha maafa katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Watu 10 wanahofiwa kufariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko.
Ripoti zinaarifu kuwa hali hiyo imeathiri pia mifugo na makazi .

Aidha nalo Shirika la msalaba mwekundu linasema maiti moja imepatikana, na kwamba waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini bonde la Kerio.Shirika hilo linasema mvua kubwa inayoendelea kunyesha imetatiza shughuli ya uokoaji.

Habari za hivi punde zinaarifu kwamba kumetokea maporomoko ya ardhi muda mfupi uliopita katika eneo la Kap-tarakwa Toro-plongo-ny karibu na Iten

Related Posts :