KIMENUKA TENA LIBYA-WATU WENYE SILAHA WAUA ASKARI WATATU

Watu wenye silaha wamewaua polisi watatu katika kituo kimoja cha upekuzi na usalama mashariki mwa Libya. 

]Hayo yamethibitishwa na polisi ya Libya kwamba polisi hao wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambapo askari mwengine amejeruhiwa vibaya katika tukio hilo. Serikali ya Libya tayari imetangaza kuanzisha uchunguzi ili kuwajua wahusika wa mauaji hayo. 

Tangu ulipoangushwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi na hususan katika miezi ya hivi karibuni, askari wa ulinzi wakiwemo wa polisi na jeshi la nchi hiyo, wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya watu wenye silaha wanaosadikiwa kuwa na mahusiano na Kanali Muammar Gaddafi.

Related Posts :