Watalii wa Kigeni Watekwa Nyara Nigeria



                                                                 Lagos, Nigeria

Na Frank M. Joachim.

Watu wenye silaha wameivamia mashua inayomilikiwa na kampuni ya huduma za mafuta katika bandari ya Nigeria leo, na kuwateka nyara raia wanne wa kigeni na kuwaua Wanigeria wawili.

Msemaji wa Jeshi la majini la Nigeria, Kabir Aliyu, amethibitisha kutekwa kwa wataalamu hao wanne wa kigeni na kuuawa kwa mabaharia wawili.

Pia ameongeza kuwa, uraia wa wageni waliyotekwa nyara bado haujathibitishwa. Maafisa sita wa jeshi la majini, ambao wote ni raia wa Nigeria walikuwepo kwenye mashua hiyo, ambayo inamilikiwa na kampuni ya Sea truck Oil Services, kuhakikisha usalama.
Wawili kati yao waliuawa na wawili walijeruhiwa, alisema Aliyu. Aliongeza kuwa jeshi la majini la Nigeria limetuma boti na helikopta katika eneo la tukio.

Related Posts :