WANAJESH WAWILI WAUAWA


WANAJESHI WA NIGERIA


RAIS WA NIGERIA, GOODLUCK JONATHAN

 Wanajeshi wawili wamepigwa risasi na kuuwawa na washambuliaji walioufyetulia risasi msafara wao katika mji wa Okene katika jimbo la Kogi nchini Nigeria. Msemaji wa polisi katika jimbo hilo ameliambisha shirika la habari la AFP kuwa wanashuku mauaji hayo yamefanywa na wanaume waliowaua waumini wasiopungua 19, katika kanisa moja la Kiinjili katikati mwa Nigeria. Hapo jana maafisa walisema waumini hao waliuwawa wakati wanaume waliokuwa wamejihami na bunduki walipolivamia kanisa hilo na kukata umeme kabla kuanza kufyetua risasi wakati giza lilipotanda ndani ya kanisa hilo. Mashambulizi ya jana ni mfululizo wa hivi karibuni wa mashambulizi ya risasi na mabomu dhidi ya Wakristo nchini Nigeria.

Related Posts :