Wafanyakazi wa Ndege wagoma












Na Frank M. Joachim

Wahudumu wa ndani ya ndege za kampuni ya Ujerumani ya Lufthansa katika uwanja wa ndege wa Frankfurt, ulio na shughuli nyingi, leo wanaendesha mgomo wa kwanza kati ya  mingi inayopangwa kufanya kudai nyongeza ya mishahara.

 Mgomo huo ulianza leo saa 11  za asubuhi za hapa Ujerumani na utaendelea hadi saa saba mchanz. Msemaji wa kampuni ya Lufthansa amesema misafara 64 imefutwa hadi sasa, hiyo ni karibu asilimia 25 ya huduma zinazotolewa.


Na Frank Joachim
Mgomo huo umekuja baada ya chama cha wahudumu wa ndani ya ndege, UFO, kusema kwamba  mashauriano juu ya suala la mishahara yameshindwa kufikia muwafaka.

 Chama hicho kinataka mishahara iongezwe kwa asilimia tano, hivyo kumaliza kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo wafanya kazi hao hawajaongezewa mishahara.

Related Posts :