Floyd Mayweather aachiwa Huru





Bondia Floyd Mayweather.


Na Frank M. Joachim

New York, MAREKANI.

The Boxing Champ mwenye Utata Mkubwa, Floyd Mayweather Jr, ameachiwa Huru siku ya Ijamaa Aasubuhi kutoka katika Jela ya Vegas, ambako alitumikia Kifungo cha miezi miwili kati ya Mitatu aliyokuwa amehukumiwa kutokana na ukatili wa Nyumbani
Jembe hilo (Floyd) alihukumiwa kutumikia Kifungo hicho mnamo December  mwaka 2010, baada ya Kushushia Kifinyo mama wa mtoto wake mbele ya Watoto wake, lakini Mpiga Nyundo (Hakimu) alimruhusu kuanaza kutumika Kifungo chake Mwezi June, Tarehe 1, kutokana na Kuwepo kwa Mpambano dhid yake na Miguel Cotto uliopangwa kuchimbika May 05 Mwaka jana, ambapo Floyd alishinda.
Msemaji wa Mpiga Masumbwi huyo, amefafanua kuwa, jombaa alihukumiwa  kifungo cha Miezi 6, baada ya kugundulika kuwa na makosa, sambamba na kuwakung’uta watoto wake katika Tukio hilo.
Jamaa huyo naongeza kuwa Floyd alionesha Tabia nzuri akiwa katika kifungo hicho, ambapo pia alitumikia masaa 100 katika shughuli za Kijamii.

Related Posts :