WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
WEEKEND ROUND UP: MKOSI MWINGINE KWA TUZO ZA MTV VIDEO MUSIC AWARDS, CHRIS BROWN ALIVYOKUTANA NA SHAMBULIZI LA RISASI, SUGE KNIGHT MAHUTUTI
Featured News| CHRIS BROWN NDIYE ALIKUWA MLENGWA |
Wakati mkosi WA Kwanza ukianza kwa
Nicki Minaji, ambapo Dancer wake amengongwa na Nyoka aina ya ANACONDA mwenye
Urefu wa Futi 6, wakati wakifanya mazoezi ya performance itakayofanyika katika
tuzo za MTV VIDEO MUSIC AWARDS, Chris Brown naye amekutana na shambulizi la
Risasi katika ukumbi wa 10 AK ulioko LOS ANGELS, Marekani, katika PRE PARTY ya
MTV VIDEO MUSIC AWARDS 2014
![]() |
| SUGE KNIGHT HALI YAKE SIO NZURI |
Kwa Mujibu wa Chanzo ambacho
kimetweet Taarifa hii katika Dawati la TTM, inasemekana kuwa, Chris Brown
alikuwa ni HOST katika Party Hiyo, nay eye ndiye alikuwa Mlengwa katika Tukio
Hilo, lakini kwa bahati mbaya , Risasi hizo zilimpata Produycer Mkongwe katika
Game la Hip Hop, SUGE KNIGHT, ambaye pia ni C.E.O wa BLACK CAPITAL RECORDS.
Aidha taarifa zinazidi kumiminika
kuwa, Hali ya SUGE KNIGHT ambaye ni mmoja wa waliokuwa waanzilishi wa DEATH ROW
RECODS iliyomuhusisha pia 2 PAC, Dr.DRE, na Snoop Doggy, sio Nzuri na ni mbaya
Kiujumla, maana lipigwa Risasi Mbili.
Baada ya Kupigwa Risasi, Suge
alionekana akitoka Nje na Kusaidiwa na Polisi kufikishwa Hospitali
Tofauti na Hilo, wasanii ambao awali
walikuwa eneo la tukio kabla ya Ufyatuaji wa Risasi hizo nne, ni Pamoja na Rapper
THE GAME na JUSTIN BIEBER, ambao waliondoka mapema.
![]() |
| JUSTIN BIEBER ALIKUWEPO KATIKA ENEO LA TUKIO, NA ALIONDOKA MAPEMA KABL:A YA VARANGATI |
Mpaka hivi sasa, Taarifa kuhusu
kujeruhiwa kwa Chris Brown, zinadai kuwa, yuko salama ingawa bado TTM
hatujapata Uhakika
WEEKEND ROUND UP: DANCER WA NICKI MINAJ ANG'ATWA NA NYOKA AINA YA ANACONDA
Featured News
Mmoja kati ya wachezaji wa Nicki
Minaj ameng’atwa na nyoka aina ya Anaconda mwenye urefu wa futi 6 wakati
wakifanya mazoezi ya kwa ajili ya show ya tuzo za video za MTV (MTV Video Music
Awards).
Kwa mujibu wa TMZ, Nicki Minaj
alikuwa jukwaani na dancers wake wakifanya mazoezi ya kucheza hit ya ‘Anaconda’
ambapo dancer mmoja wa kike aling’atwa na moja kati ya nyoka waliokuwa
wamewekwa kwenye kontena kwa ajili ya kufanyia mazoezi.
Inaelezwa kuwa nyoka hao aina ya
Anaconda hawakuwa na sumu lakini wana uwezo wa kusambaza bacteria ambao
husababisha matatizo kiafya.
Msichana huyo alipelekwa hospitalini
kupata matibabu.
Haijulikani kama bado Nicki Minaj
atapanda na nyoka hao katika jukwaa la MTV VMAs, Jumapili .
Nicki hatakuwa mwimbaji wa kwanza
kupanda na nyoka kwenye tuzo hizo, mwaka 2001 Britney Spears alipanda na joka
kubwa wakati anaimba ‘I’m A Slave 4 U’.
WEEKEND ROUND UP: TIZAMA PICHA 20 ZA MWANASOKA WA ZAMANI WA BRAZIL NA REAL MADRID, RONALDO DE LIMA AKIWA NA BABA YAKE PAMOJA NA KISHTOBE CHAKE, UFUKWENI WAKILA BATA
Featured NewsWEEKEND ROUND UP: CHRIS BROWN USO KWA USO NA RIHANNA..
Featured News
LICHA ya Wengi kuhisi kuwa, huenda
Chris Brown na Rihanna hawatokutana kwa Mara Nyingine Tena, This Time Imekuwa
Tofauti..
Chris Brow amejikuta akikutana na
Rihanna, ambaye alikuwa mpenzi wake kabla ya kumwagana chini, katika Shughuli
maalumu inayofahamika kwa jina la ROC NATION’S SUMMER CLASSIC CHARITY BASKET
BALL, iliyofanyika ndani ya Weekend Hii
Ingawa kuna Muda alionekana
kufurahia game hilo, lakini amini usiamini, alikuwa eneo la mbele kabisa ambalo
piga ua, ilikuwa ni lazima amtizame Chris Brown
endapo ataushika Mpira
PETER MSECHU NA BABA LEVO WANAPOMLILIA RUGE...KUHUSU KUKOSA CHANCE YA KUPERFORM FIESTA
Featured NewsINSTACOP: HIVI NDIVYO WALIVYOMVAA DIVA LOVENESS LOVE WA CLOUDS FM, KUHUSU WEAVING LAKE
Featured NewsDAVIDO...
Featured News
UGONJWA wa EBOLA umemgusa Super
Artist Kutoka Nchini Nigeria, DAVIDO, kushiriki katika Mchakato ambao
unaendelea Hivi sasa katika mitandao ya Kijamii , unaofahamika kwa Jina la ICE
BUCKET CHALLENGE, yaani Kujimwagia Maji ya Barafu.
Aidha , baada ya davido kupendekezwa
kuingia katika Challenge Hiyo, na Producer Don Jazzy , Basi hakutia Ngumu wala
kupingana nayo, bali alifanya Hivyo na Kumwagiwa maji hayo yenye Barafu.
Kupitia account yake ya Instagram,
Davido amepost Video Hiyo, na Kutoa Kiasi cha Dolari za Kimarekani 100 kwenda
katika Account ya ALS FOUNDATION, ambayo ndiyo inayoguswa zaidi katika Kupata
Mchango huo wa Fedha kutoka kwa watu mbakli mbali Ulimwenguni, na Kusaidia
walengwa ambao kamwe hawajiwezi.
Tofauti na Hilo, Pia Davido
amewataja watu tofauti kushiriki, akiwemo 2 FACE IDIBIA, na Wengineo.
ICE BUCKET CHALLENGE, ni Mchakato
ambao umekuwa ukichukua nafasi kubwa sana katika Mitandao mbali mbali ya
Kijamii, hasa Instagram, ambapo Mtu anayetajwa kushiriki, basi hana budi
kushiriki kwa Kumwagiwa ama kujimwagia Ndoo ya Maji yenye Barafu na kuchangia
kiasi Kadhaa
Mpaka Kufika AUGUST 18, Kiwango cha Fedha ambacho kilikuwa
kimeshakusanywa kutokana na Mchezo huo ni USD MILION 15.6, na watu ambao
wameshashiriki katika Mchezo huo, ni kama Vile CRISTIANO RONALDO, LADY GAGA,
JUSTIN BIEBER, ICE PRINCE, DON JAZZY, OPRAH WINFREY, LEBRON JAMES, BILLIONEA
BILL GATES, MACLEMORE, MMILIKI WA FACE BOOK MARK ZUCKERBERG, SELENA GOMEZ,
JUSTIN TIMBERLAKE, na wengineo Kibao.
KIDUDU MCHEPUKO ETI KIMEINGIA KATIKA NDOA YA MARIAH CAREY
Featured News
KUNA tetesi ambazo zimeanza kuzagaa
kuwa Nick Cannon na Mkewe Mariah Carey wameshaingiliwa na Kidudu Mchepuko, hali
ambayo inaweza kuleta athari kubwa katika Ndoa yao.
Kitengo Chimbua Chiombua, kimenyaka
Mchakato Mgumu kweli kuutabiri, na kudai kuwa, kumekuwa na Ugomvi wa hapa na
pale baina ya wanandoa hao wawili huku sababu ikiwa ni tuhuma za kuchepuka
zinazomkabili Nick Cannon.
Aidha Mtonyo haujaishia hapo tu, pia
inasemekana Nick Cannon hivi sasa amehamishia Maskani ya Muda, katika Hotel
moja hivi ambayo bado hatujalinyaka Jina
Tofauti na Hilo, Pia Kuna mmoja wa
Ndugu wa karibu kwa wanandoa hao, ambaye alidai kuwa, Mariah carey amechoshwa
na Suala la Mchepuko ambalo mara Nyingi
amekuwa akilifanya Nick Cannon, hali ambayo imemfanya amuwekee walinzi
ambao watazuia warembo wote wanaomsogelea Nick, hali ambayo ilidhihirika Katika
POOL
PARTY moja iliyofanyika Las Vegas, huku Nick Cannon
akiwa ni MC wa Shughuli hiyo.
Mariah na Nick walifunga ndoa mwaka
2008, na Mpaka Hivi sasa bado wanamaisha yao katika Ndoa Hiyo, licha ya Mariah
Carey kutokufanya Vizuri katika Muziki kama ilivyokuwa awali.
BUSTED: JENIFFER LOPEZ NA KISERENGETI BOY CHAKE WAMERUDIANA.
Featured News
MAREKANI....
WANASEMAGA
penzi ni kikohozi na kulificha kamwe huwezi hata siku moja..sasa chukua hii
hapa..
JENNIFER
LOPEZ inawezekana kabisa akawa amerejesha mahba yake niue kwa Kiserengeti boy
chake, Casper Smart
Siku ya
Jumatatu mapema, JLo pamoja na Casper Smart walikamatika na camera za Wadaku
wakiwa Ndani ya gari ambalo linalosadikika kuwa ni la Jennifer Lopez.
Hata Hivyo
basi, baada ya Mwanamama Jennifer kubaini kuwa, kuna wakali wa Maudaku
wanawafuatilia na Kuwadungua mafoto kadhaa, basi alijificha kwa Kuinama ndani
ya gari hilo, lakini kiserengeti Boy
Chake casper Smart, kikibaki kawaida,
sababu ndiye alikuwa anaendesha Gari.
JLO na
Smart walipigana Chini Mwezi Juni, huku lawama zikiangukia kwa Casper Smart
kuwa amekuwa akichepuka na Mtu ambaye alibadili Jinsia, jambo ambalo alipingana
nalo huku akiahidi kufungua mashtaka kwa yeyote anayeanzisha mastor Hizo
Subscribe to:
Posts (Atom)


































