WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MAUZO MABOVU YAWATENGANISHA MARIAH CAREY NA PRODUCER WAKE WA MUDA MREFU.
Featured News
SUPER VOICE MAMITO Mariah Carey
ametemana na producer wake wa Muda Mrefu, JERMAIN DUPRI, baada ya Albam yake
kupata mauzo mabaya tofauti na ilivyokuwa imetarajiwa..TTM tunao Mtonyo Kamili.
Aidha inasemekana kuwa, Muimbaji
huyo Mwenye Umri wa Miaka 44 hivisasa, amefikia uamuzi huo mgumu dhidi ya
Jermaine Dupri, ambaye wamedumu katika kazi kwa Muda wa takriban Miaka 20, na kuamua
kuungana na Msimamizi Mwingine, KEVIN LILES.
Kwa mujibu wa Info ambazo TTM bado
tumezipata katika kukamilisha Data Hizi, inasemekana kuwa, wawili hao ambao
walianza kazi rasmi mnamo 1995, awali walienda vizuri na mafanikio makubwa sana
ikiwemo kufanya Hit single ya WE BELONG TOGETHER, lakini baada ya kuachiwa kwa
albam Mpya ya ME I AM MARIA, huwezi amini zimeuzika nakala 100,000 tangia Mwezi
May, mpaka hivi sasa.
Tofauti na Hilo, Pia Jermaine
aliwahi kuingia kunako Noma Nzito baada ya Kumuandalia Perfomance Mariah Carey,
juu ya Wanasiasa wa Angola, jambo ambalo lilipigwa Vita na Wanaharakati wa haki
za binadamu, kwa madai kuwa alifanya kitu kisicho kizuri hasa kwa Siasa
zinazokiuka haki za Binadamu.
HATIMAYE TUMEINYAKA TAREHE YA KUTOKA KWA MIXTAPE YA LIL KIM
Featured News
LONG time sana tumekuwa tukisubiri
kwa hamu ujio wa Mixtape ya The Queen Bee, Lil Kim, na hata wengine kukata tama
kuhusu kuachiwa kwa Mixtape hiyo, hatimaye TTM tumeinyaka Tarehe ambayo Mzigo
huo unaingia Ofisini.
Kupitia account yake ya Twitter, Kim
ametangaza rasmi kuwa Mixtape Hiyo itaachiwa Rasmi SEPTEMBA 11, na watu wajipange
kuskiliza kile ambacho bibni huyo kakishusha baada ya kukaa kimya Muda Mrefu.
Mixtape hiyo, imepewa Jina la
HARDCORE 2K14, likiwa ni Jina amablo limewahi kutumika katika Moja ya Kazi zake
aliyoifanya Mwaka 1996, na ilikuwa ni Albam ya HARDCORE
Lil Kim Hivi sasa Ni mama wa Mtoto
Mmoja, na Wiki kadhaa zilizopita aliachia Remix ya Beyonce FLAWLESS na ya Bobby
Shmurda HOT FELLA (NIGGA).
Tofauti na Hizo, Lil Kim ameachia
Track ya Kumdiss Nicki Minaji inayokwenda kwa jina la IDENTITY THEFT
SELFIE TIME: JAMAA AVAMIWA NA NDEGE WAKATI AKIJIPIGA SELFIE
Featured NewsWANGAPI mnampenda kupiga Selfie…Okay sasa kuna jambo jambo hapa ya kusikia.
Jombaa mmoja amevamiwa na Ndege mwenye hasira wakati akijifyatua Kitu Selfie ambayo imepata umaarufu kupita maelezo hasa katika Mitandao ya Kijamii
STEVEN TAKATA, alimuona Ndege huyo anayevutia katika eneo la kufugia wanyama, ZOO, lenye jina la GREAT BEND ZOO, iliyoko
KANSAS, MIDWEST, Marekani, na kuamua
kumsogelea mbele yake ili ajifyatue Selfie, na alipokuwa akifanya Zoezi hilo,
kumbe Ndege alimaind na hakutaka kuuza Nyago kwenye mitandao kama vile Insta.Sasa Noma likaja pale alipojigeuza ili aweke Poz Vizuri na kupiga picha picha hiyo, kwa hasira Ndege huyo alirefusha shingo kutoka katika Fensi yake, na kumvaa huku akimkwangua Jombaa huyo, na kumuachia makovu madogo.
Licha ya kwamba STEVEN alipata majeraha, bado alijikausha na kufyatua Selfies Kadhaaa
ILIKUWA NI VITA YA CHATU NA MAMBA.........SASA TIZAMA VITA YA MAMBA NA KIBOKO
Featured News
TUKIO
hili limetokea KRUGER PARK, Huko Afrika ya Kusini, ambapo Mamba Huyu Mkubwa
alimvamia KIBOKO huyu Mdogo, baada tu ya mama yake (Kiboko Mama) kumpa Mgongo
Mtoto wakati wako katika harakati zao.
Inasemekana
kuwa Mamba Huyu Mkubwa, alikuwa katika Mawindo na amefanikiwa kumchukua Mtoto
huyo (kiboko) kwa ajili ya Kitoweo
HONGERA PASTOR MYAMBA WA BONGO MOVIE
Featured News
SIKU ya Jana Kupitia Account za Instagram za
Mastaa mbali mbali wa Bongo Muvi, Kulisheheni Picha za Muigizaji machachari,
PASTOR MIYAMBA, pamoja na Mke wake ambaye TTM hatujanyaka Jina Jina lake.
Sasa, kwa Mujibu wa Picha na Info ambzo bado
zinasambaa kunako Mtandao huo wa Instagram, inasemekana kuwa, Ndo hiyo
ilifanyika zaznzibar, na Sio daslaam kama ambavyo wengi walidhani, huku Mstaa
kibao akiwemo JACOB STEVEN na wengineo wakihudhuria katika pilau hilo.
Aidha Mchakato umezidi kutufikia kuwa, Moja kati
ya zawadi ambayo Pastor Miyamba amepokea, inaweza kumfanya afungue Kampuni yake
tena kubwa tu na ya kutosha kujiendeleza
Zawadi ambazo TTM tumebahatika Kuzinyaka, ni
Pamoja na Fedha Taslim MILLION 250, ambazo zimeonekana katika picha iliyotupiwa
Instagram, pamoja na Ndinga ambayo bado hatujaiona, na kazi ya kulisaka
tumewakabidhi KITENGO CHIMBUA CHIMBUA.
TIZAMA: PICHA ZA MASHOGA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NCHINI JAMAICA
Featured NewsINGAWA ni kweli kabisa kuwa, Nchi ya Jamaica, hupinga Pia Masuala ya Ushoga yaani Mapenzi ya Jinsia Moja, lakini bado Shughuli hii inaendelea
Mashoga hawa, ambao wamekuwa wakiishi katika
wakati Mgumu sana, unaweza kurejea katika hali ya Ubinadamu endapo utawaona.
KWANZA wanaishi katika Mazingira ya ajabu na
Machafu. Mahali ambapo wameweka makazi yao, ni katika Mitaro na Mifereji ya
Kupitisha Maji machafu.
PILI wanakutana na Changamoto kubwa sana, ambayo
lazima ujwaonee huruma, ikiwemo kupigwa vikali na Wananchi, na hata kuchomwa
Moto, na kukatwa na Mapanga
TATU, soko lao, ama ulimwengu wao umeingiliwa,
jambo ambalo huwafanya wasiaminike na hata kutamanika katika Mji hasa wa
KINGSTON Jamaica. Kuna baadhi ya waharifu wamekuwa wakitumia Mwanvuli wa USHOGA
kufanya uharifu, mfano kuwaibia watu, kuwachoma watu na Visu, na hata
kuwamwagia Tindikali wabaya wao. Jambo ambalo huwafanya watu waamini kuwa Mashoga
hao ndio waharifu
NNE Jeshi la Polisi ni Sehemu ya Misuko suko
yao, baada ya kuwakamata mara kwa mara wakiamini ni waarifu
Subscribe to:
Posts (Atom)


































































































