REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KUDADADEKI…SHAKIRA HATAKI KUOLEWA NA GERARD PIQUE?

5:12:00 AM Add Comment

Aisee, Hii inaweza kuwa ajabu ya aina yake hasa kwa waleambao wamekuwa wakifuatilia Mahusiano ama mahaba ya Mkali wa HIPS DON’T LIE, Shakira, pamoja na Mchezaji wa BARCELONA, Gerald Pique mwenye Miaka 27..Sikiliza kwa Umakini Mtinyo Huu,

Shakira ameweza kuushangaza Umati wa watu tofauti alipotoa kauli ya kuonekana kutokuwa na Mpango wa Kufunga ndoa na Boyfriend wake huyo wa Muda Mrefu.

Akizungumza kwa ufafanuzi kuhusu kauli yake, Shakira mwenye Umri wa Miaka 37, amesema kuwa hivi sasa hafikirii suala hilo la Ndoa kwa hivi sasa, kwa sababu haitaleta Utofauti wa Aina yoyote katika mahusiano, na bado itabaki kuwa vile Vile.

Aidha Shakira ambaye Mnamo March alikamilisha Albam yake ya 10 aliyoipa Jina la SHAKIRA, ameongeza kuwa, hivi sasa wameshafanikisha kile ambacho wanacho, maana wanapendana kwa Dhati, Wana Mtoto, Uhusiano wao tayari umeshakuwa Mzuri na wenye mafanikio, hivyo suala la Ndoa halitobadilisha Chochote katika masuala hayo Muhimu ambayo wamesha yapata.


Tofauti na Hilo, Shakira alipoulizwa kuhusu sala, ama kitu kinachomfanya awe “happy” siku zote, alesima kuwa ni kushare kila alicho nacho na Mtoto wao Milan, ambaye hivi sasa ana Miezi 17, ukizingatia anapenda kumfundisha kitu kipya Kila Siku

MIAKA 5 YA KIFO CHA MICHAEL JACKSON : HIVI NDIVYO BEYONCE ALIVYOSAIDIWA NA MICHAEL JACKSON.

5:05:00 AM Add Comment

SIKU ya Jana, Ulimwengu Mzima ulikuwa katika kumbu kumbu ya kumpoteza Mfalme wa POP, Marehemu Michael Jackson, ambaye alifariki JUNI 25, 2009.

Katika Kukumbuka Mengi ambayo Michael aliyafanya ama kuchangia katika Kuboresha Ulimwengu wa Muziki kwa Baadhi ya wasanii, Beyonce ni Moja kati yao, ambaye kuna machache ya Msingi sana hatoyasahau kutoka kwa Wacko Jacko…

Akiandika Maelezo Kadhaa katika Website yake, BEYONCE ambaye hivi sasa bado anatisha na kwaju lake la DRUNK IN LOVE, alisema kuwa, Marehemu Michael alimbadilisha kwa Kiasi kikubwa, na Kumfanya Awe Msanii ambaye hivi sasa anaonekana kuwa.

Beyonce aliendelea kwa kuandika kuwa, wakati anaanza game la Muziki, Producer wake wa Kwanza kabisa, alikuwa akimshawishi kumsikiliza Michael Jackson akifanya Live Perfomance ya “WHO’S LOVING YOU”, huku akitizama kwa Ukaribu kile alichokuwa akikifanya kwa Stage

Pia Beyonce ameeleza kuwa Producer huyo alikuwa akitaka ajifunze Roho ya Michael, maana endapo angefanya Perfomance na hata Muziki wake, ungepata nafasi ya kuiskia nafsi yake na hata Roho yake hasa Kile ambacho alikuwa anakifanya, ukizingatia, Michael alikuwa Bado ni Mdogo, na hakuwa na Uzoefu kiasi hicho, lakini watu walimpenda, na hata Kuteka Hisia zao.

Aidha Beyonce aliongeza kuwa, Michael alimfundisha kuwa, Kuna Muda unatakiwa Kusahau kabisa kuhusu Mbinu zako, kusahau kile ulichonacho, bali kuzingatia ni nani ambaye uko naye, anayekukubali, na kumwaga hata machoi kwa ajili yako.

Beyonce amemalizia kwa kumshukuru sana Michael jackson kwa Kumfanya awe msanii Mkubwa hivi sasa.

USWAZI-TAKE-AWAY: HATA AKINA MRISHO NGASSA WAMETOKEA HUKU-WATOTO WA BUGARIKA (BUGAZIL)

6:32:00 AM Add Comment
Licha ya Ugumu wa Mazingira Yetu hasa Sie Watoto wa Uswahilini, lakini kubali, ukatae, hata akina MRISHO NGASSA, wametopkea Huku, hii Ndiyo Burudani Yetu
Tunauwezo Mzuri wa kukabiliana na Adui zetu wanathubutu kunyemelea Magoli Yetu, ingawa hatuna Nyavu

VIWANJA vyetu havina Nyasi, lakini Vumbi na Michanga, ni Nyasi tosha, ilimradi tu, tunapata Burudani, kipaji kinaonekana, uzoefu unaongezeka, na Siku Inaenda

Hatuna Uwezo wa kununua Viatu. Na hata Hivyo, Raha ya "Kabumbu" letu, ni kulisukuma bila Viatu wala Socks

Kuna baadhi ya Sheria za Soka huwa hazifuatwi katika Soka Letu sisi watoto wa USWAZZ, lakini baadhi kama PENALTY, CORNER KICKS, FOULS, na HAND TO BALL, tunaziona saaana, maana tunahitaji Ushindi

Huwa hatubagui watizamaji ama mashabiki. Mara Nyingi hutupa Motisha japo ni wachache




Mashabiki wa Jinsia ya Kike, huwa ni ADIMU sna katika Mechi zetu, na Endapo wakitokea kuhudhuria, basi kila mtu hutumia mbinu zake, na ustadi wake, ili mradi Dada huyo atuone, na kujenga sifa, na ukaribu zaidi

Jezi Zetu mara Nyingi huwa ni Arsenal, ama Machester United na Timu Nyinginezo za Ligi ya Uingereza. Tukiona hivi, basi tunaamini ipo siku nasi tutacheza Ligi kubwa kama hao Wengine

Tunajua Mwanza kuna Mawe, Lakini hata siku moja hayatuzuii kusakata Soka letu, ingawa ni hatari hasa kujikwaa, ama unapoanguka katika Jiwe Hilo

Tunatamani Serikali za Mitaa zitutengenezee Viwanja Vizuri vya kucheza Soka huku Uswaz Kwetu, lakini ni Ndoto kwa kweli

Sio Mawe Tu, Viwanja Vyetu vinakabiliwa na Miti hatarishi iliyokauka, Chupa zinazoweza kudhuru miguu yetu maana hatuchezi na Viatu, pamoja na Mazingira Salama Kiafya

ISHU YA VIDEO YA JAY Z AKIMSALITI BEYONCE IKO HIVI……

4:56:00 AM Add Comment

DEAR FACE BOOK USERS, Tafadhari kuna jambo la msingi sana ambalo mnatakiwa kuzingatia, baada ya kuwepo kwa Kitu kinachodaiwa kuwa ni Video ya Jay Z akikunjuka na “Kishtobe” kingine tofauti na “wife” wake BEYONCE, sasa Iko Hivi…

Info Kamili imeshushwa na Kitengo Chimbua Chimbua kuwa, Kunako Mtandao wa FACEBOOK, kuna jombaa mmoja ambaye alifungua account FAKE, na Kupost Link ambayo inazungumzia, Kuvuja kwa Video ya JAY Z akimsaliti Mke wake BEYONCE, na Video hiyo ilikamatwa na SOLANGE, ambaye ni Mdogo wake BEYONCE.

Lakini ukweli ni Kwamba, Ishu hiyo sio ya Ukweli, na Utawala wa Facebook imetoa Taarifa kwa Watumiaji wote kuepukana na Link hiyo, kwani ni moja kati ya Vitu ambavyo vinalenga Kupotosha Umma, hasa wale watumiaji wa Mtandao huu maarufu, pamoja na Mashabiki wa Jay Z na Beyonce.

Aidha Utawala huo umongeza kuwa, endapo utaclick tayari kwa Kuingia katika Link Hiyo, basi hautakutana na Video hiyo ambayo imetajwa na Mwizi huyo wa Mtandao, bali utakutana na mtandao mwingine ambao utakuomba kukubali baadhi ya Masharti ikiwemo kushare Link hiyo kwa marafiki zako, jambo ambalo ni hatua ya kukaribisha wizi wa Mitandaoni, pamoja na Uharifu mwingine hasa wa kimtandao.

Aidha kama utafuatilia kwa Ukaribu, Picha ambayo imetumika kupamba kichwa cha habari ambacho kinasema VIDEO YA KUSHTUA: KANDA YA VIDEO YA JAY Z AKIMSALITI BEYONCE, IMEKAMATWA NA SOLANGE, ni Picha ambayo JAY Z anaonekana akiwa amekaa na akina dada wawili waliokuwa kwenye Utupu, yaani kama walivyozaliwa.

Katika Kuhitimisha, Utawala wa Facebook umesema kuwa, Video ambayo inatumiwa na Waharifu hao, ni ile ambayo ilifanyika mwaka 1997, katika Interview moja hivi, huku kweli akionekana kuwa na akina dada hao wawili, lakini ilikuwa ni kabla hajamuoa BEYONCE..

So WATCH OUT GUYS……

LICHA YA KUCHIKA MARA KIBAO, JENIFFER LOPEZ BADO ANAAMINI KATIKA NDOA.

4:51:00 AM Add Comment

LICHA ya kuachika Mara 3 katika Ndoa, pamoja na Mara kadhaa katika mahusiano ya kawaida ya Kimapenzi, ladies and Gentlemen, In case hukufahamu, J-LO bado anaamini katika Ndoa mazee.

Akimiminika kunako Interview na Kituo cha Redio cha HOT 97 Nchini Marekani, J-LO mwenye Miaka 44, ambaye hivi sasa amepigana Chini na “Ki-Serenget Boy” chake CASPER SMART, mwenye Umri wa Miaka 27, amesema kuwa, bado hajakata tamaa katika kulisaka Penzi tamu, maana amewahi kuwa katika Ndoa, na alikuwa akitamani kuwa katika Ndoa Imara.

Bibi huyo ambaye alifanya poa sana na Dude la “LOVE DON’T COST A THING”, amesema kuwa ingawa sio kazi rahisi kuwa katika Ndoa na kuhimili mabo zake, lakini anaiamini sana, anaamini katika kujizatiti ndani ya Ndoa, pamoja na kujikita zaidi kwa mtu ambaye unaamini mtaspend maisha yenu yote ndani ya Ndoa.

Pia J-LO ambaye ni mama wa watoto wawili Mapacha, MAX na EMME wenye Miaka 6 Hivi sasa aliozaa na Ex-husband MARC ANTHONY, amesema kuwa, licha ya kwamba amekuwa “USED” sana na watu kadhaa ambao amekutana nao, lakini anaamini yupo Mtu ambaye atampata, na kuishi naye maisha yake yooote katika Ndoa ambayo itakuwa More than Serious.

Aidha, HIT MAKER huyo wa “WAITING FOR TONIGHT” alikanusha kuwa na mahusiano ya Kimahaba na MAKSIM ambaye ni Dancer wake wa karibu, huku akisisitiza kuwa ni Marafiki wa kawaida, pamoja na Kazi…basi

UKO TAYARI "NYOKA" HUYU AKUFANYIE UPASUAJI KATIKA KOO LAKO?..HII HAPA

4:38:00 AM Add Comment

Swali ambalo nitaanza kwa kuuliza, ni Je, ulishawahi kutamani ama kuwaza, Nyoka aingie katika Koo lako kwa ajili ya Matibabu Fulani?...
SASA mseto imekutana na “NYOKA-ROBOTI”, kifaa ambacho kitafanya upasuaji katika Koo lako na Maeneo Tofauti ambayo ni ya Ndani ya Mwili.

Kifaa hicho kilichopewa jina la “FLEX SYSTEM” ama “SNAKE-ROBBOT” kimebuniwa na kutengenezwa na Professor wa masuala ya Robbotics, HOWIE CHOSET, kutoka katika Chuo cha CARNEGIE MELLON, kilichoko PENNSYLVANIA

Aidha Kifaa hicho kilifanyiwa Maboresho zaidi na Kampuni ya Uingereza, inayofahamikla kwa jina la MEDROBITICS CORP, na mpaka hivi sasa, kimeshafanikiwa kutibu wagonjwa wawili katika Hospitali ya Chuo cha DINANT GODINE huko Nchini Marekani

USWAZI-TAKE –AWAY: MWENYEKITI MSTAAFU..TAFADHARI TUHESHIMIANE…KINYESI CHAKO HUKOOOO

4:43:00 AM Add Comment







WIKI hii nzima, UTA (Uswaz-Take-Away) inajikita katika Mtaa wa BUGARIKA hapa Jijini Mwanza, sasa leo nina Hili.

Katika Mtaa huo Husika, kuna Mwenyekiti wa Mtaa Mstaafu (Jina Kinywani) ambaye tunaona anajisukuma na ujasiriamali wake wa vitu tofauti, ameamua kabisaaa…kuliruhusu Tanki la “KINYESI” kujaa na kuanza kutiririsha “Juisi ya Kinyesi” katika Maeneo ambayo tunapita, na hata kuweka Vituo kwa ajili ya Mazungumzo binafsi.

Kama ambavyo unaona hizo picha, kuna baadhi ya Waungwana wanadai kuwa, walishawahi kumwambia Kiongozi huyo ambaye nafasi yake ni EXPIRED kwa hivi sasa, lakini amekuwa akipiga kimya tu, jambo ambalo UTA, tumetafsiri kama “NYODO”

DOH !!!!!

CHRIS BROWN NA KARREUCHE HAWAKUSOMEKA KABISA CLUB

3:06:00 AM Add Comment

KUNA uwezekano Mkubwa kabisa ukajiuliza maswali mengi kuhusu Kurudi kwa mahusiano ya Chris Brown na KarreucheTran, baada ya Breezy kutoka Jela, huku awali ikibainika kuwa alikuwa amepigana Chini na mamito huyo, lakini Hivi Ndivyo inavyoanza kuhisiwa.

Siku ya jana , TTM tulipata Mtonyo na Baadhi ya Picha ambazo zilimuonesha Chris Brown akiingia na Kutoka kunako Night Club Moja, akiwa na Girlfriend wake Huyo, Karreuche, kwa ajili ya Bata za hapa na Pale, lakini baada ya kitengo CHIMBUA CHIMBUA kuzama Kiundani zaidi, kuna hili ambalo limesomeka.

Karreuche Tran hakuwa karibu sana na Chris Brown ndani ya Night Club Hiyo tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa, zaidi ya Kustick na Bibie wa YMCMB, CHRISTINA MILLIAN.

Tofauti na kuwa na Christina, Karreuche alikuwa busy akipiga mtungi wake kawaida, pamoja na Kucheza Mikwaju kadhaa ambayo ilionekana kumuingia, huku Breezy akiwa haishi kumkata Jicho mara kadhaa, hali ambayo iliashiria kuwa huendawawili hao, hawakuwa Vizuri.

Aidha katika Hali Nyingine ambayo ilizua maswali kwa Wengi, Chris Brown alionekana kutokufurahia kabisa Usiku huo ndani ya Club hiyo inayofahamika kwa Jina la SOCIALITE CLUB, inayosifika kwa Kuwahusisha Wapenzi wa Jinsia Moja, huku karreuche akiwa katika Mood Nzuri.

Pia Bibie huyo alionekana kuwa Bize zaidi na Simu kulikokuwa Busy na Chris Brown, lakini baadaye inasemekana kuwa baada ya kutoka Nje kupokea Simu aliyopigiwa na Mtu ambaye hakufahamika mara Moja,aliizima kabisa.


Chris Brown na Karreuche, wamekuwa wakipigana Chini na Kurudiana tangia wameanzisha Mahusiano yao mwaka 2010, ikiwa ni baada ya Breezy kuachana na Rihanna mwaka 2009.

KANYE WEST KUWEKA HOSPITALI NDOGO NDANI YA JUMBA LAKE LA KIFAHARI, LAKINI KIM KARDASHIAN HAONI UMUHIMU...

2:46:00 AM Add Comment

WANASEMAGA, Ukiwa na Mkwanja, basi unaweza fanya chochote ambacho unajiskia kufanya, na hicho Ndicho Rapper Kanye West amthibitisha, TTM tuna Mtonyo Kamili.

Kuna uwezekano Mkubwa kabisa kuwa katika Jengo kubwa la Kifahari ambalo linajengwa Kwa ajili ya Familia ya Kanye West huko, LOS ANGELS, Nchini Marekani, itapatikana Hospitali Ndogo ambayo itakuwa ni Maalum kwa ajili ya Familia Yake.

Kwa Mujibu wa Kitengo aminifu cha Chimbua Chimbua kutoka TTM, Kanye ambaye hivi sasa ana umri wa Miaka 37, anatarajia kutumia EURO MILIONI 3 kwa ajili ya kujenga Hospital Hiyo ndogo ambayo ni mahsusi kabisa kwa ajili ya Afya yake, Mke wake Kim kardashian, pamoja na Mtoto wao North West Mwenye Umri wa Mwaka mmoja hivi sasa.

Aidha katika Hospitali ndogo hiyo ya Ndani, itajumuisha Vitu vifaa kama Vile Mashine ya X-RAY, CT Scanner, ULTRA SOUND MACHINE, na Vifaa vingine kwaajili ya Kuchukua na Kupima Damu.

Tofauti na Vifaa hivyo, Pia Kanye anatarajia Kuwaajili Madaktari na Wauguzi ambao watakuwa wakifuatilia afya za Familia Hiyo mara kwa mara, pamoja na Timu maalum ya kumtizama na kuwa makini na Mtoto wake North West..

Katika hali Nyingine, Kim Kardashian anaamini kuwa Mme wake Huyo Kanye, anaenda Mbali sana katika maamuzi hasa ya Kujenga Hospitali hiyo katika jumba lao, kwani ni kitu ambacho hakina ulazima sana kuwa nacho, lakini hakuna ambacho anaweza fanya ili kumzuia Yeezy.

Moja kati ya watu maarufu ambao wamewahi kujenga Hospital Ndogo katika Nyumba zao ni pamoja na Muimbaji mkongwe wa POP, MADONNA.

Kanye West na Familia yake hivi sasa wanaishi katika Nyumba ya Mama Mkwe Wake, KRIS JENNERS, wakati wakisubiri kumalizika kwa Ukarabati wa Jumba lao hilo huko LA, na wanatarajia kuhamia katika jumba hilo baada ya kila kitu kuwa sawa

UNADHANI RAY C, ATAKUWA KIOO SIKU YA ALHAMIS 26 JUNE?...

2:20:00 AM Add Comment


Harakati za Kupiga Vita matumizi ya Madawa ya Kulevya hasa kwa rika la Vijana, zinazidi kutanuka, baada ya Mwanaharakati RAY C kujitosa katika SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA.

Kupitia account yake ya Instagram, Ray C ambaye aliwahi kufanya Vizuri na Track ya SIKUHITAJI, amepost PICHA za maandalizi ya Banda La taasisi yake ya RAY C FOUNDATION, litakaloonesha shughuli mbali mbali ambazo anazozifanya, katika Siku Hiyo itakayoadimishwa ALHAMIS ya Tarehe 26 Mwezi wa 6, Jijini Mbeya.


Mgeni Rasmi katika Siku hiyo maalum kabisa Duniani, atakuwa Dr.Galib Bilal, makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Ray C amekuwa katika Harakati za kupiga Vita Matumizi ya Madawa ya Kulevya, ikiwa ni Baada tu ya Kusaidiwa Kuepukana na matumizi hayo ambayo yalikuwa yamemuathiri kwa kiasi kikubwa, na mpaka hivi sasa ameshasaidia baadhi ya Vijana ambao wataungana Naye huko Jijini Mbeya katika banda lake.

Kwa Mtazamo wako, Unadhani RAY C atakuwa Kioo cha Watu Wengi Siku Hiyo?

MNADA BANNER