WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
NICKI MINAJI NA ALIYEKUWA DESINGNER WAKE WA MAWIG, NGOMA HAIKAI.
Featured News
NEW
YORK , Marekani.
Nicki Minaji na aliyekuwa designer
wa mawig yake anayefahamika kwa jina la TRRENCE DAVIDSON, bado ngoma ni ngumu
baada ya wawili hao kuonekana kuingia katika Bifu ambalo linatarajiwa kuwa la
aina yake, TTM Jo vile tushazinyaka.
Kwa Mujibu wa CHIMBUA CHIMBUA, Mwezi
February Designer Huyo alimfungulia Mashtaka Nicki Minaji hasa ya madai ya
kiasi cha USD Milioni 30 kwa madai ya Kudhurumiwa na Bibie huyo Kutoka YMCMB,
lakini Hivi Nicki Minaj ameamua kuvunja Ukimya na kufunguka kama Sio
kumiminika.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ,
Chimbua Chimbua wameshusha Ripoti kuwa, Nicki Minaji amesema kwamba, Desiogner
huyo, amini Msiamini Si lolote, Si chochote bila yeye, maana yeye ndiye
amemfanya kufikia hapo alipo, na hata kipaji chake kimefikishwa mbali na Nicki
Minaj Mwenyewe.
Mkali Huyo wa Looking Back Fella (Looking Ass Niggah), na
Moment For life, amesema kuwa, awali designer huyo, daidson, alitaka
akajihusishe na masuala ya Reality TV shows, kipaji ambacho hakuwa nacho,
lakini alimshauri afanye naye kazi katika Suala Zima la mawigi, jambo ambalo
ana
Ushahidi wa maandishi hasa katika makubaliano yao.
Hata Hivyo, Mpalka hivi sasa Nicki
Minaj Bado hajakubaliana na madai ya Desgnerhuyo, hivyo anabaki tu kuchekelea
Kuhusu mashitaka hayo.
IS DRAKE MOVING ON?..AONEKANA NA MCHUCHU MWINGINE BAADA YA KUTEAMANA NA RIHANA
Featured News
NEW
YORK, Marekani
Kuna Uwezekabno Mkubwa Kwamba Rapper
Drake kutoka YMCMB akaaamua kupiga hatua ya kuenjoy maisha ya Kimahusiano,
baada ya kutemana na Rihanna
Rapper huyo Mwenye Umri wa miaka 27,
amepost Picha yake na Bibie mmoja ambaye inasadikika kuwa aliwahi kuwa mahaba
Niue wake kipindi cha Nyuma, anayefahamika kwa jina la BRANDY PRINCE.
Tofauti na Kupost Picha Hiyo, Dreezy
ambaye Hivi sasa ameingia katika kinyang’anyiro cha BET AWARDS-2014, aliandika
Maelezo kuwea, yuko na Mpenzi wake wa toka kitambo, hivi sasa, na Tena na tena.
Ikiwa ni baada tu ya Drake kupost
Picha hiyo, mamito huyo naye alipost Picha ya kaka yake anayefahamika kwa jina
la JAS PRINCE, akiwa ameketi meza Moja na Drake (Shemejiiiii), huku wakigonga
Mvinyo wa kutosha Pamoja na kupiga story za hapa na pale.
Mpaka hivi sasa Rihanna hajaonesha
makali yake Ingawa wengi wanahisi huenda akarudisha majeshi kwa Aliyekuwa Honey
wake Chris Brown, Pindi tu atakapomaliza Kifungo chake cha mwaka mmoja Jela, na
Kukaa sawa.
Dreezy na Rihanna walilripotiwa
kurudisha mahusiano yao mnamo Mezi February, lakini hivi majuzi tulipata mtonyo
kuwa wawili hawa wamepigana Chini kwa kile kinachosadikika kuwa ni Drake
kumpenda kupita maelezo Rihanna , na hata kufikia Kugombana haswa mara kadhaa
ALBUM YA MARIAH CAREY IKO TAYARI HIVI SASA
Featured News
NEW
YORK , Marekani.
Hatimaye Albam ya 14 iko tayari
kutoka Baada ya Wiki Moja kuanzia sasa, na hatimaye kurudisha Hadhi na heshima
ya Mariah Carey katika Muziki wa R&B.
Albamu hiyo ambayo itafahamika kwa
Jina la ME. I AM MARIAH CAREY, inatarajiwa kuachiwa Mnamo May 27, huku ikiwa
imeshirikisha Vichwa Mbali mbali katika Soko la Muziki Kimataifa, akiwemo NAS,
MARY J. BLIDGE, FABULOUS na WALE.
Pia katika Suala Zima la Production,
Mikono iliyosimama pale ni pamoja na Mkono wa JERMAIN DUPRI, HIT-BOY,RODNEY
JERKINS na MIKE WILL MADE IT
Albam Hiyo ambayo unaweza kui-order
hivi sasa kupitia I TUNES, imesheni Mikwaju kama Ifuatavyo
1. Cry.
2. Faded
3. Dedicated (feat. Nas)
4. #Beautiful (feat. Miguel)
5. Thirsty
6. Make It Look Good
7. You’re Mine (Eternal)
8. You Don’t Know What To Do (feat. Wale)
9. Supernatural
10. Meteorite
11. Camouflage
12. Money ($ * / …) (feat. Fabolous)
13. One More Try
14. Heavenly (No Ways Tired/Can’t Give Up Now)
15. It’s a Wrap (feat. Mary J. Blige)
2. Faded
3. Dedicated (feat. Nas)
4. #Beautiful (feat. Miguel)
5. Thirsty
6. Make It Look Good
7. You’re Mine (Eternal)
8. You Don’t Know What To Do (feat. Wale)
9. Supernatural
10. Meteorite
11. Camouflage
12. Money ($ * / …) (feat. Fabolous)
13. One More Try
14. Heavenly (No Ways Tired/Can’t Give Up Now)
15. It’s a Wrap (feat. Mary J. Blige)
Deluxe Version:
16. Betcha Gon’ Know (feat. R. Kelly)
17. The Art of Letting Go
18. Me. I Am Mariah…The Elusive Chanteuse
16. Betcha Gon’ Know (feat. R. Kelly)
17. The Art of Letting Go
18. Me. I Am Mariah…The Elusive Chanteuse
HATIMAYE CIARA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME
Featured News
LOS
ANGELS, Marekani.
Kama Obama Land hawatosema “Hayawi hayawai sasa yamekuwa”, kibongo Bongo
inabidi Tuseme hivyo Tu, kama ambavyo TTM tumeweza kuinyaka
Finally Ciara hivi sasa anaingia
katika jukumu Jingine Jipya kabisa baada ya kujifungua Mtoto wa kiume mapema
Jumatatu ya Wiki hii
Ciara ambaye ujauzito wake umekuja
kubainika Mnamo DECEMBER Mwaka jana kabla hata hajaweka wazi kama Kweli tayari
ama lah, Hivi sasa yuko katika Furaha ya aina Yake na Mchumba wake Future
ambaye ni rapper, Mtunzi, Muimbaji na Producer
Akizungumzia furaha Aliyonayo Ciara
ambaye alikita na Kwaju la BODY PARTY, anasema hawezi kuielezea kiujumla, kwa
sababu anaamini kila kitu kimeenda Vizuri, na anashukuru kamwe hakutamani
kuishia Njiani katika safari yake ya kumpata motto wake.
Pia akielezea kuhusu Changamoto za
Ujauzito wake, Ciara amesema kuwa, ujauzito huo haujampatia Changamoto ngumu
yoyote, bali imekuwa Ni hatua Nzuri kwake, na umekuwa ni uzoefu Mzuri sana
kwake.
Kupitia Account yake ya Instagram,
Ciara amesema kuwa, mtoto wao amepewa Jina la FUTURE ZAHIR WILBURN, n hata
hivyo Picha bado hazijaachiwa rasmi kunako Mitandao ya Kijamii, kasoro Tu,
Mkono wa Kuchanga hicho amao uliachiwa na mama yake Ciara.
HAWA NDIO FISI WALIOKUTWA NA SHANGA PAMOJA NA ROZALI KIUNONI. MKOANI MWANZA
Featured Mwanza
NA G-SENGO
MSAKO wa
Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa Kata ya
Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu.
Maajabu hayo yamehusishwa na imani za
kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya 12 waliouawa, kukutwa wamevalishwa
shanga na Rozali, kiunoni.
Msako huo wasiku tatu ulioanza juzi (Jumapili)
unahusisha mamia ya wananchi wa Kijiji hicho na vitongoji vyake vya
Mwanzabalemi, Mwanega na Mwang’ombe, wanaotumia siraha za jadi na mbwa wapatao
50.
Habari za ndani kutoka Kijijini humo zimesema
kwamba, kabla ya wananchi hao kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi
wanadaiwa kumilikiwa na watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina,
wazee wa Kijiji na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na
nguvu za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo.
Kwa mujibu wa baadhi ya wazee wa kijiji hicho
ambao hawakutaka majina yao yaandikwe, walisema kuwa makamanda wa jadi
wanaoongoza msakao huo pamoja na mbwa wao, wana kinga za kupambana na imani za
kishirikina vinginevyo wasingeweza kuua fisi wenye shanga na Rozali wanaotumiwa
kishirikina.
Diwani wa Kata ya Hungumalwa Shija Malando
akizungumza na waandishi katika Kijiji hicho jana, alisema wananchi walifikia
maamzi ya kufanya msako huo wa siku tatu, baada ya kundi kubwa la Fisi hao
wanaokadiliwa kuwa zaidi ya 80, kuwa tishio kwa watoto na mifugo.
Alisema kuwa, kwa muda wa miaka miwili iliyopita
hadi sasa, licha ya wanyama hao kuharibu hekali moja ya matunda aina ya Tikiti
Maji yaliyokuwa yamelimwa na mwanchi mmoja, wameua ng’ombe 109, Mbuzi 135,
kondoo 127 na Nguruwe 15 katika Vitongoji hivyo.
“Njooni muone maajabu haya.” Alisema Malando na
kufafanua “Jana (juzi Jumapili) wananchi walifanikiwa kuua fisi kumi wawili
kati yao wakiwa na maajabu. Mmoja aliukuwa na Rozali kiunoni na mwingine akiwa
na shanga kiunoni huku uume wake ukiwa umetahiriwa kama binaadam.”
Alisema fisi waliokutwa na vitu hivyo kiunoni,
kwa imani za kabila la Kisukuma, wanadaiwa kumilikiwa na baadhi ya watu wenye
imani za kishirikina na kwamba, waliuawa majira ya saa 8 hadi saa 10 mchana
kwenye eneo la mlima wa Mwanzabalemi.
Alifafanua kuwa, fisi kumi waliuawa (jumapili)
siku ya kwanza ya msako huo na wengine wawili waliuawa jana asubuhi na kwamba
maeneo ya milima ya Mwanangi katika Kijiji cha Buyobo na Kitongoji cha
Mwanzabalemi yanasadikiwa kuwa na fisi wengi zaidi.
“Pamoja na kushambulia mifugo wetu, ilifika
mahali wananchi walikuwa hawawezi kutembea kwa uhuru nyakati za usiku na baadhi
ya watoto wanaosoma mbali kukatisha masomo kwa kuhofia kuliwa na fisi hao.”
Alieleza Mwenyekiti wa Kijiji cha Hungumalwa, Clement Kaswahili.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwang’ombe Joseph
Kisena alisema hadi kufikia leo (siku ya tatu ya msako huo) watakuwa wameua
fisi wengi zaidi kutokana na ushirikiano mzuri wa Vitongoji hivyo vinavyotumia
mbwa 50 na siraha mbalimbali za jadi ikiwemo mikuki, mapanga na marungu.
Kisena alisema, pamoja na maajabu ya fisi kuvaa
shanga na Rozali kiunoni ambayo wamejionea na kuzua imani za ushirikina kwa baadhi
ya wananchi, hawatarudi nyuma, hadi walitokomeze kundi la wanyama hao ambalo ni
tishio kwa wananchi na mifugo wao.
BAADA YA KUDAIWA KUMTELEKEZA MTOTO WAKE KATIKA GRADUATION YAKE, 50 CENTS AJIBU TUHUMA..
Featured News
ATLANTA, Marekani
50 CENTS amejitokeza na Kudai kuwa hakumtelekeza
mtoto wake siku ya graduation yake, kama ambavyo mwanae huyo alilalamika.
Marqiuse Jackson, hivi majuzi alikuwa anahitimu
masomo yake ya Diploma huko nchini marekani, lakini jambo la kushtua ni kwamba,
Marquise alipost Picha Huku akionekana Kulalamika baba yake 50 Cents
kutokuhudhulia, huku akipata Kampani ya kutosha toka Kwa mama yake na dada
yake.
50 Cents
anadaiwa kujiskia Vibaya baada ya kuona Picha ya Mtoto wake Huyo akiwa
amemkumbatia mama yake huku akionekana Kulia, na amevalia Joho, na kuandika
maneno makali kama yale.
Hata Hivyo, TTM imebaini kuwa, 50 Cents alidai
kuwa hakuambiwa ni lini, na Ni wapi ambapo Mahafali ya Mwanae yalifanyika,
tofauti na hilo angehudhulia.
FIDDY amekuwa katika kutokuelewana na mama wa
Marquise, na Dio maana huenda hakupewa hata hiyo taarifa kuhusu Graduu ya Mtoto
Wake huyo wa Kwanza, iliyofanyika katika Shule Moja huko Jijini ATLANTA
CHECK PICHA ZA MTOTO HUYU WA 50 CENTS
RAY JAY ATATOA ZAWADI KWA KIM KARDASHIAN. NI FAIDA ILIYOPATIKANA KATIKA MKANDA WAO WA NGONO
Featured News
KUNA UWEZEKANO MKUBWA, Ray J akawa ana lake
jambo baada ya Kuamua Kufanya kitu ambacho wengi tuklikuwa Tumeshaanza
kukisahau
Ray J ameahidi kumpa Kim kardashian zawadi ya
Faida aliyopata katika Mkanda wao wa Ngono uliovuja Miaka kadhaa iliyopita.
Ishu hiyo iliyoteka Vichwa kibao Vya habari
Duniani, Inasemekana Kuwa, itafanyika katika Ndoa pamoja na Sherehe ya Kufunga
Ndoa kwa kanye West na Kim kardashian, ambapo Ray J amesema atatoa Zaidi ya USD
LAKI 40, ambazo amezipata ndani ya Miezi Minne
Pia ray J ameshusha Hesabu zake ambazo amezipata
Kuanzia mwezi January ambazo Ni kama Ifuatavyo
-- January $6,135.60
-- February $20,097.31
-- March $9,674.76
-- April $10,931.52
-- January $6,135.60
-- February $20,097.31
-- March $9,674.76
-- April $10,931.52
Aidha Kwa mujibu wa Mtandao wa VIVID ENTERTAINMENT,
inasemekana kuwa Video Tape Hiyo ambayo ilifanyika 2007, imeuza mpaka Kupata
Kiasi cha USD MILIONI 50
Hata hivyo Mitandao ya kidaku ilijitahidi kumtafuta Kim
kardashian Ili kuzungumza kama atapokea zawadi Hiyo toka kwa ray J, lakini
hakupatikana.
Pia Ray Jay amedai kuw3a, kama Kim hatopokea Zawadi hiyo,
basi ataipeleka katika kituo cha Kulea watoto yatima ambacho Kim Kardashian
anakipenda.
Subscribe to:
Posts (Atom)

























