WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
USHER RAYMOND KUMRUDISHA CHRIS BROWN KWA MAFANZ WAKE.
Featured News
Wengi Tunafahamu kabisa kuwa Brown Breezy hivi
sasa Yuko Jela akisubiri Kesi yake na hukumu kwa makosa kadhaa aliyoyafanya
ikiwa ni pamoja na kumfumua Mangumi Jombaa mmoja aliyejitokeza kunako Zoezi la
Upigaji picha bila Idhini yoyote.
Baada ya TTM kuzama kunako info za NYUMA YA
PAZIA, tumeweza kunyaka Mtonyo kuwa, Muimbaji Mkongwe hasa kunako mahadhi ya
RnB, USHER RYMOND, amesema kuwa,
amemshirikisha Chris Brown katika Albam yake mpya, na mashabiki wake wanatakiwa
kusikiliza Ukali uliopatikana katika Track Hiyo.
Usher alifafanua kuwa, Ngoma ambayo wameifanya
(yeye Na Breezy), inajibu maswali mengi sana ambayo wengi wamekuwa wakijiuliza.
Pia ameongeza kuwa, Track hiyo inafafanua namna
ambavyo Binadamu tunakutana na Magumu Mengi, lakini ukweli utabaki kuwa pale
pale kuwa sisi ni Binadamu, na Tuna Mengi ambayo tunatakiwa kupitia.
Tofauti na masuala ya Track, Pia Mkali huyo wa
DJ GOT US FALLING IN LOVE,amesema kuwa hajakutana mara kadhaa na Chris Brown
tangia ameingia Jela, ingawa baada ya Kutoka Rehab, na anaamini kabisa kuwa
baada ya yote yanayomkabili, Atabadilika na kuwa bKijana Mwema
#BRINGBACKOURGIRLS: WATU WAWILI WAMEUAWA KWA KUCHOMWA MOTO…
Featured News
DAWATI
LA TTM
KUNDI LA BOKO HARAM limezidi kuzua
Vitimbi Kila kukicha ikiwa ni baada ya kusadikika Kuwateka watoto wadogo wa
kike kwa Nyakati Tofauti:
Siku ya Jana Kitengo Chimbua Chimbua
Tulitoa Ripoti Kutoka Nchini Nigeria Kuwa Mwanamke Mmoja katika Eneo la ABULE
EGBA, jijini Lagos, aliuawa kwa Kuchomwa Moto baada ya kuhisiwa kuwa alitaka
Kuiba, ama Kuteka wanafunzi ambao walikuwa wakielekea Shuleni
Lakini Siku ya Leo Pia, Tumeweza
kuzipata Kuwa, Mwanaume Mmoja Mkazi wa AKURE, alikutana na Kifo cha Kikatili
baada ya Kupewa kipigo kikali katika makutano ya ADEGBOLA na kasha kuchomwa
Moto, kwa tuhuma za kukutwa na Mtoto ambaye inadaiwa Sio wake.
MBWADIDI
LILIVYO:
Mchakato Mzima Bado unachanganya hasa
Kuhusu Tuhuma dhidhi yake, ukilinganisha hili ni Tukio la Pili ambapo Marehemu
wote haijathibitika kama ni Watekaji, au ni watu wa Kawaida tu waliotaka
kujitolea kwa watoto hao.
Baadhio ya wananchi walidai kuwa
Mtoto aliyepatikana na Jamaa huyo, allikutwa amekufa, huku baadhi ya Wananchi
wakisema Mtoto huyo yuko hai.
Tofauti na Hilo, wananchi wote
waliokuwa katika eneo la tukio, walioshiriki na wale ambao hawajashiriki, wadai
kuwa, Kuna Uwezekano Mtu waliyemuua, alikuwa ni CHIZI, yaani hana akili timamu,
ama Likuwa na ASkili Timamu.
MWISHO WA RIPOTI
KITENGO CHIMBUA CHIMBUA.
SIZE 8 NA NYWELE NYEKUNDU
Featured News
Tunaamini kuwa Kila Mtu Huwa
anapenda sana Kujishughulisha ili kujikwamua hasa Kiuchumi, pamoja na kukidhi
mahitaji mengine.
Lakini tofauti na hilo, Tunaamini
kuwa, kazi ya mtu ni kitu anachojivunia siku zote kulingana na hulka na mtazamo
wake juu ya kazi husika.
Hivi ulishawahi kumuona mtu
akiichukia kazi yake ambayo inampa Riziki?..au, Ulishawahi kuhisi Unaichukia
kazi yako, na kutamani kuiacha?..sababu Ni Hizi:
1.
SABABU ZA MFANYA KAZI
·
Huitambui
Vema kazi yako
·
Huna
malengo na kazi yako
·
Haujitangazi
Vema kupitia Kazi yako ili kupata Channels Tofauti
·
Hushirikiani
na Wenzako, yaani wewe Ni Mbinafsi
·
Huzingatii
Thamani ya Kazi yako.
·
Huna
Heshima katika kazi yako
2.
SABABU ZA KIKAMPUNI
Kampuni Inaweza kuwa sababu kubwa
yaw ewe Kuichukia kazi yako:
·
Kampuni
haikuthamini.
·
Mshara
/Malipo madogo ukilinganisha na Nguvu kazi yako
·
Kampuni
kukosa Shukrani dhidi ya Kizuri unachokifanya
·
Kudharaurika
hasa Kutoka kwa Viongozi
·
Kampuni
Kujenga matabaka baina ya wafanya kazio kisa Muonekano, hali ya Kimaisha, na
Nafasi za upendeleo
·
Kampuni
kushindwa kumpa motisha Fulani Mfanya kazi.
·
Kampuni
kutokufanyia kazi UBUNIFU wa Mfanyakazi pindi aletapo mawazo mapya ya Projects
·
Kauli
Mbaya Toka kwa Viongozi/ Utawala
·
Kampuni
Kutokuthamini matatizo yako hasa ya
Kiafya/Kifamilia/ nk
·
Unyanyasaji
hasa kijinsia
RIPOTI YA KITENGO CHIMBUA CHIMBUA: MWANAMKE AMEUAWA KIKATILI BAADA YA KUDHANIWA ANATAKA KUWATEKA WANAFUNZI
Featured NewsMKUU WA TTM
Ama Kweli Binadamtunaunyama ambao kijumla hautabiriki.
Mwanamke huyu anaeonekana katika Picha, Ameuawa Kikatili na Wananchi Wenye Hasira kali, baada ya Kutuhumiwa kuwa alitaka kuwateka watoto wadogo waliokuwa Wakienda Shule
MKASA WENYEWE..
Ripoti ya KITENGO CHIMBUA CHIMBUA, imebainisha kuwa., mama Huyo aliwasimamisha watoto wadogo hao waliokuwa na umri unaokadiriwa Kuwa Miaka 7-10, na kuwaambia atawapeleka Shule, huku akiwaambia waongozane
Baada ya Kufikia uamuzi huyo, Mpita njia mmoja aliyemuona, alihisi huenda mama huyo anataka kuwateka watoto hao, na kuanza kupiga kelele za Msaada, na wananchi kuanza kumshughulikia.
Mpaka Mwanamke Huyo anakufa Kikatili, hakuna aliyekuwa na Uhakika kama Mwanamke huyo ni Mtekaji..au Lah
MWISHO WA RIPOTI:
KICHICHI-Kitengo Chimbua Chimbua, NIGERIA
TAARIFA NA PICHA KUHUSU BOMU LILILOLIPUKA JIJINI MWANZA
Featured Mwanza News
MHUDUMU wa
nyumba ya kupumzikia wageni wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa
Victoria, jijijini hapa, amejeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu
lililokuwa limewekwa kwenye korido la nyumba hiyo.
Tukio
hilo lilitokea jana (Jumatatu), kati ya saa 1:45 na saa 2:20 usiku, katika eneo
la Makongoro wilayani Ilemela wakati mhudumu huyo Bernadetha Alfred (25)
alipofungua kifurushi cha mzigo alichodhani kimesahaulika kwenye eneo hilo,
kabla ya kumlipukia.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Dayosisi hiyo, Mollel Rogart, kifurushi hicho kilichokuwa
kwenye mfuko mweusi wa nailoni, kilikuwa juu ya kreti (tupu) za soda, karibu na
eneo la kulia chakula lililopo katika nyumba hiyo.
“Ule
mfuko ulikaa pale siku tatu ndiyo usiku huo mhudumu wetu akakichukua
kukiangalia akidhani ni mzigo wa mtu umesahaulika.” Alieleza Katibu huyo na
kudai kuwa kifurushi hicho kilimlipukia mara tu alipokifungua na kujeruhi
vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili.
“Bernadetha
kajeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni na usoni na siwezi kusema
kwamba chanzo cha mlipuko huo ni mambo ya kidini japo ulinzi wetu haukuwa mkali
kiasi cha kudhibiti watu walioingia na vitu.” Alisema
Kamanda
wa polisi mkoani Mwanza, Valentino Mlowola akithibitisha tukio hilo, alisema kwamba
uchunguzi wa awali uliofanywa na kikosi maalum kutoka Dar es salaam umebaini
kuwa bomu hilo limetengenezwa kienyeji.
“Bado
tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili tubaini ni nani kafanya ili kama ni
mtu au kikundi kimehusika tuchukue hatua haraka. Natoa wito kwa wananchi
kutochukua vitu ambavyo hawa uhakika navyo, wanapoona vitu vya aina hiyo, watoe
taarifa kwetu.” Alisema Kamanda Mulowola.
Mlowola
alieleza kuwa, Bernadetha aliyejeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za
mwili, alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando ambako anaendelea na
matibabu.
Kamanda
huyo alieleza kwamba, mabomu (yakiwemo ya kienyeji) yako katika mifumo
mbalimbali hivyo wananchi hususan wahudumu wa sehemu za mikusanyiko wawe na
tahadhari na vitu vinavyoonekana kusahaulika na wasisite kuwajulisha polisi
vinapoonekana hivyo.
Mlipuko
huo uliozusha hofu kwa waumini mbalimbali wakiwemo wa Kanisa hilo, umetokea
ikiwa ni wiki moja baada ya maadhimisho ya ‘Huduma ya Mtoto’ kwa makanisa
mbalimbali ya Kikristu jijini hapa yaliyofanyika kwenye kanisa hilo,
yakitanguliwa na maandamano kutoka uwanja wa furahisha hadi KKKT.
Subscribe to:
Posts (Atom)




















