WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MWANZA IS THE BEST: KILIO CHA AMANDOLA NA TIZZO, KINA UKWELI KABISA NDANI YAKE.
Featured Mwanza
KAMA ilivyo kawaida yangu, jana Nilipata nafasi
ya Kupita katika Mtaa wangu wa BUGARIKA, jijini Mwanza.
Nashukuru mungu huwa nina Chama kubwa ambalo
huwa tunajumuika kupiga Story za hapa na pale hasa Muziki na masuala mengine,
Huku tukipata “UJI” wa jioni, ambao husukuma Story zetu.
Lakini wakati stoty Zimenoga, Walikuja ghafla
Vijana hawa wawili, AMANDOLA na TIZZO MIPANGO, ambao ninawafahamu vizuri maana
tunaishi pamoja Mtaa mmoja.
Katika kitu ambacho nilikinukuu kutoka kwa
AMANDOLA na TIZZO ni kwamba “HATUJAKATA TAMAA, LAKINI TUTAFANYAJE KAMA HUKO JUU
KUMEZIBWA?”
Wawili hawa wanazo nyimbo zaidi ya Mbili na wote
kwa pamoja wanafanya kazi vziuri sana, ingawa bado wanahitaji Support ya Dhati.
Niliwaza sana namna ya Kuwasaidia, nikasema
hapana, lazima hili nilifikishe TTM, ili tufanye kitu ambacho kinaweza
kueleweka kabisa..
Wanachokililia AAMANDOLA na TIZZO, ni Kitendo
cha nyimbo zao Kuchukuliwa, lakini Mwisho wa siku hata hazipitiwi na
waliozichukua kwa sababu tu, hawana Muonekano wa Kisanii (Mavazi, magari, Viatu
vya gharama, Kusuka Rasta au Mengineyo)
Tofauti na hapo, hata watu wanaoahidi
kuwasaidia, bado wanawakimbia na hata Kushindwa kupokea Simu zao, pale
wanapowapigia na Kuwakumbusha kile Walichopanga.
Lakini Ngoja Nifanye kitu kimoja, Sikiliza Hii
Track yao, inaitwa DEEJAY
EMMY'S LAMODA: ALL BEAUTIFUL GIRLS WA MWANZA, TUNAKULETEA "OFFICIAL LADY" CLOTHINGS..CHEKI HAPA
Featured MwanzaCLARA SALON: HATUNA HAJA YA KUJITAPA..HUDUMA YETU INAELEWEKA MWANZA NZIMA.
Featured Mnada Mwanza
KAMA Wewe Ni Mgeni wa Jiji la Mwanza, haitupatii
Shida kukuelewesha mahali ambako CLARA SALON Wanapatikana. Ukifika katika
Shule ya Sekondari ya Pamba, Ulizia tu CLARA SALON, na kila mtu atakuelekeza
Ilipo. Ni hapo hapo karibu.
Robert Tawile, Ramah D na Ally Ming;arisho
Wakiwa Kazini ndani ya Clara Salon, Upande Wa Saloon ya Kiume
Moja kati ya huduma ambazo ninakuhakikishia
utazifurahia, ni Pamoja na Huduma za Kiume na hata za kike katika Suala Zima la
urembo kuwa sawa.
Ally “Ming’arisho” akiwa katika Kazi yake ya
Kung’arisha Kucha na mengineyo
Tofauti na hayo, CLARA SALOON kuna Mavazi ya
Jinsia ya kike na ya Kiume kwa watoto na watu wazima
Uduma unayoipata hapo, hakika itakushawishi
urudi Mara kwa Mara, na hata kutamani kuendelea kubaki Eneo la Tukio, ukienjoy
kila kinachoendelea
CLARA SALON eneo la Nje, kati kati ya jiji la
Mwanza
CHAMBO RABA RABA: DEEY CLASSIC ANANIRUDISHA TENA KWA KISHINDO….
Featured Mwanza
JIJI la Mwanza bado linazidi kufikia malengo
mazuri baada ya Kila Msanii kufanya kile ambacho kinastahili kufanyika.
CHAMBO RABA RABA, moja kati ya wasanii wanaojituma
sana kuufikisha muziki wao Nje ya mipaka ya Nchi hii, this time ameamua kuja na
Kitu kipya ambacho kitamgusa kila mtu na hatimaye kuelewa kazi nzima kiujumla.
Akipiga story na TTM, CHAMBO amesema Kuwa ,
Track yake hiyo ambayo Imepikwa kunako Studio za REVOLUTION SOUND chini ya “Mguso”
wa DEEY CLASSIC, itafahamika kwa jina la USIKATE TAMAA, huku ikiwa na maudhui
ya kusikilizwa na Rika la aina yeyote.
Tofauti na hayo, Chambo ambaye ameweza kufanya
vema na Traxx tofauti kama vile MAUMIVU na RABA RABA, amesema kuwa Track hiyo
ya MAUMIVU itaachiwa Rasmi Mnamo Mwezi APRIL , mwaka huu
“Ninatarajia kuachia Track hii mwezi wa Nne,
jambo ambalo tumekubaliana na Producer wangu DEEY CLASSIC kutoka Revolution
Sound, hivyo wadau wa Muziki na Wapenzi wa Chambo raba Raba, wasubiri
kushuhudia namna ambavyo DeeyClassicananirudisha katika ramani ya Muziki, baada
ya kukaa kimya kwa muda mrefu kidogo”
Katika kuhitimisha, CHAMBO amesema kuwa Track
hii kwa Mara ya Kwanza kabisa itasikika katika kituo bora Cha burudani Mwanza Nzima
METRO FM 99.4, na hatimaye kusambazwa Sehemu tofauti hasa kupitia mitandao ya
kijamii.
HUDDAH AMEZUA HAYA KWA MARAFIKI NA HATERS WAKE, BAADA YA KUACHANA NA ACCOUNT YAKE YA TWITTER NA INSTAGRAM.
Featured News
Ilikuwa ni kama Mshtuko baada ya kubaini kuwa
aliyekuwa Mshiriki wa BIG BROTHER AFRICA Mwaka 2013, akiiwakilisha Nchi ya
Kenya, HUDDAH MONROE, anaachana na
Mitandao Miwili ya Kijamii, TWITTER na INSTAGRAM.
Sasa haya Ndiyo maoni ambayo yalifuatia kutoka
kwa hao niliowataja hapo juu
Errymonroe: I'm having huddah fever, i miss her
sana sana
Bihanifa: I miss huddah
Journeydedan: Huddah i miss u...
Lizndirangu: I lv u Huddah
Imaryam9 :Where is huddah we really miss her
Shirohgee Baddest Bitch.....miss her.
Boynayo: Now that huddah deactivated her acc
y'all can reach her thru her email address Huddahmonroe @ yaHOE .com"
Subscribe to:
Posts (Atom)



















