WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
EMINEM AZUNGUMZIA KITENDO CHA 50 CENTS KUONDOKA KATIKA LEBO YAKE.
Music
KITENDO Cha 50 CENTS Kuondoka Shady
Records, Aftermath Entertainment na Iterscope Records, Zimewastua Wengi sana
ambao walikuwa wanafahamu uhusiano mzuri na wa karibu baina ya 50 Cents
Mwenyewe, Eminem na Dr.Dre.
Lakini baada ya Kutoa Taarifa
hapo jana Kuwa ameamua Kutemana na Kampuni hizo ambazo ndizo zimemtoa katika
Music Industry Ulimwenguni kote na Kufikia hapo alipo hivi sasa, Mmoja kati ya
Wamiliki wa Lebo hiyo ambayo ilikuwa ikimsimamia 50 Cents na kazi zake kwa Muda
sasa, EMINEM, amesema kuwa anajivunia Kumfahamu 50 Cents, na Kitendo cha yeye
kuondoka kwao, hakitaathiri Urafiki wao wa muda Mrefu.
Aidha Emenem ambaye pia
anafahamika kwa jina la Slim Shaddy, amesema Kuwa, yeye pamoja na SHADY RECORDS,
wanajivunia Kuwa sehemu ya Mchango wa Mafanikio ya 50 Cents katika Muziki.
Tofauti na hapo, Eminem aliongeza
kuwa, Kama isingekuwa uwepo wa 50 Cents katika Studio Hizo, basi hata Shady
Records isingekuwepo hapo Ilipofikia.
Kwa Upande wake 50, amesema kuwa
amekuwa na Muda Mzuri sana wakati akifanya kazi na Shady/Aftermath/ na
Interscope Records, huku akiwashukuru sana Dr. Dre na Eminem maana amejifunza
Mengi kutoka Kwao. Lakini hivi sasa anahitaji kwenda sehemu Nyingine na
Kujifunza Mtazamo Mpya.
50 Cents anaelekea katika Studio
za Caroline,iliyotokana na CAPITOL RECORDS.
Ingawa Hivi sasa anajiandaa
kushusha Albam yake Mpya ya THE ANIMAL AMBITION, Albam ya GET RICH OR DIE
TRYING ambayo ilikuwa na Mikwaju kama Vile IN DA CLUB, MANY MENT, P.I.M.P,
ilisukwa Vizuri na Lebo ambayo anatemana nayo
NDIO MWISHO WA SAUTI SOUL?..AU KUNA NINI KINACHOENDELEA
Music
SAUTI SOUL Kutoka Nchini Kenya, Limekuwa ni
kundi ambalo wengi wamevutiwa nalo huku wao wakipata mafanikio makubwa sana
barani Afrika.
Kwa Mujibu wa Chanzo ambacho kilipiga Story na
Standard Media Nchini Humo, inasemekana kuwa, kuna uwezekano Mkubwa wa Memba wa kundi hilo kufanya Kazi za Peke yao,
yaani SOLO,ukizingatia hawajafanya hivyo kwa Muda Mrefu.
Ingawa Memba Wote wa SAUTI SOUL awali walikanusha uvumi kuwa kundi hilo
limevinjika, hivi sasa wamekuwa wawazi kuwa, kila memba atashiriki katika
Project yake Mwenyewe, ili kucheki uwezo wao, pamoja na Kupeana uhuru katika
baadhi ya kazi na uwezo wao nje ya Kundi.
DELVIN MUDIGI ambaye Pia ni Memba wa Kundi hilo,
amesema kuwa ameshiriki kazi mbali mbali za Kundi, lakini hivi sasa anatakiwa
kupima Uwezo wake hasa kimuziki, nje ya kundi, lakini Kundi bado Liko poa.
The same to POLYCARP FANCY FINGERS,
amedhihirisha kuwa Kundi bado lipo, na Still litazidi kuwepo, lakini kwa Hivi
sasa, wameamua kwa pamoja na kwa makubaliano, kufanya kazi za Pekeyao, hasa kwa
Kila Memba
LUDACRIS NDANI YA JANGA LA KIFEDHA, AMESHINDWA KUMHUDUMIA MTOTO WAKE.
WENGI Wanaweza Kujiuliza inakuwa Vipi Awe katika
Tatizo la Kiuchumi wakati mwaka Jana alikuwa katika List ya Orodha ya Forbes
kwa Rappers ambao wanaongoza kwa Mkwanja, lakini ukweli utabaki Pale pale.
TTM tumezinyaka kuwa inasemekana LUDACRIS
amevuna Dola za Kimarekani 55,000 sawa na Tshs Milioni 88 kwa Mwaka 2013, jambo
ambalo limemfanya kushindwa kumhudumia Mtoto wake
Kwa Mujibu wa maelezo yake wakati yuko
mahakamani alikoshtakiwa na TAMIKA FULLER, ambaye ni mama wa Mtoto wake wa Kike
mwenye Umri wa Miaka Miwili, Luda alikiri kuwa ni kweli hajamhudumia Mtoto wake
huyo ambaye anatakiwa ampatie Dola 15, 000 Kwa Mwezi , sawa na Tsh Milioni 24,
kwa ajili ya matumizi.
Pia Luda aliongeza kuwa alitarajia kuvuna
Mkwanja Mrefu kupitia Muvi ya FAST & FURIOUS 7, na kuliweka sawa hilo suala
la Kiasi hicho cha gharama za Mtoto, lakini mabo yalienda Ndivyo sivyo baada ya
kusitishwa kwa Muda Utengenezaji wa Muvi hiyo kutokana na Kifo cha PAUL WALKER
LUDA alisema kuwa hivi sasa anaweza kutoa Dola
18000 sawa na Tsh Milioni 2, na Elfu Themanini na nane.
Hakimu wa Kesi Hiyo, alimuamuru LUDA kulipa
gharama za Dola 7000 sawa na Tsh Milioni 11, na Laki 2 kwa ajili ya Matumizi ya
Mtoto huyo, wakati mahakama Ikipitia Taarifa zake za kifedha.
Kama utakuwa ni Mfuatiliaji mzuri wa Ludacris,
Hajawahi kuachia Albam Nyingine tangia Mwaka 2010, aliposhusha Albam ya BATTLE
OF THE SEXES
WYRE NA JOSEE CHAMELEONE, USO KWA USO NA JAY Z, KANYE WEST NA WENGINEO..
Music
Na Oxs Okelleky "Big Dady"
TUNAWEZA
Kusema Shukrani sana kwake WYRE THE LOVE CHILD Kutoka Nchini Keny na Josee
Chameleone kutoka Uganda, kwa Kuzidi kuipeleka Pazuri Afrika mashariki, Kupitia
Sanaa ya Muziki wao.
MIKITO Mikali ya WYRE na CHAMELEONE imeweza Kuwafikisha katika Tuzo za THE WORLD
MUSIC AWARDS kwa Mwaka Huu.
Wyre ambaye hivi sasa anafanya Vizuri na Track
yake ya NO MORE pamoja na Chameleone, ameingia katika Kipengere Kigumu sana cha
WORLD’S BEST MALE ARTIST, ambako watakutana na Vichwa Nguli na
balaa katika
Muziki ulimwenguni kote.
Wawili hao ambao hawakamatiki katika Muziki wa
Dance hall Nchini Kenya, Uganda, na
Afrika Mashariki Kiujumla,w atakutana na Vichwa kama Vile JAY Z, KANYEWEST,
P.DIDY, JOHN LEGEND, CHRIS BROWN, JUSTIN BIEBER, RICK ROS, 2 CHAINZ, PITBULL,
LIL WAYNE, KENDRICK
LAMAR, FUSE ODG, FALLY IPUPA na wengineo Kibwena.
Aidha katika CATEGORY hiyo hiyo, Wasnii wengine Kutoka
Barani Afrika ni Pamoja na DAVIDO, ICE PRINCE, D BANJ, WIZ KID, TIMAYA, OLAMIDE,
FALLY IPUPA,2 FACE IDIBIA, FUSE ODG na Wengineo.
THE WORLD MUSIC AWARDS, ni Tuzo ambazo hutambua
kazi na Ubora wa Wasanii Mbali mbali Duniani
TYGA NA CHRIS BROWN WANAREJEA TENA…..
Music
NA EDNA ELISHA "NATTY E"
MOJA
kati ya Historia ambayo haitakuja kujitokeza, Ni Baada ya Chris Brown kuungana
na Tyga, hatimaye Kutengenza ALBAM ambayo ilikuwa ni “HATOKI MTU HAPA”
Kwa Mujibu wa TYGA katika moja ya Interview
Nchini marekani, TTM tumemnyaka akisema kuwa Historia Hiyo inatarajiwa Kuvunjwa
baada ya wawili hao kujipanga kwa Ajili ya ALBAM Mpya wakiwa Pamoja.
Mnamo Mwaka 2010, wawili hao walishusha Mixtape
ya FAN OF A FAN ambayo ilifanya Vizuri, na Mwaka Huu pia wanakuja na Brand New
Albam ambayo itaitwa FAN OF A FAN 2
Katika maelezo yake TYGA ambaye ni Memba wa
YMCMB, amesema kuwa wawili hao watajiunga Tena na Kufanya Project ambayo itawaweka
karibu sana, huku wakiwapatia Mashabiki wao Kitu ambacho wanakihitaji.
TYGA na Chris Brown waliweza Kuteka masikio ya
Mafanz Wao kupitia Mikwaju Very hot kama
Vile DEUCES na HOLLA AT ME
MB DOG AMEWAHI KUVUTA MILIONI 10 KATIKA SHOW
MKALI
wa Muziki wa KIzazi kipya Kipindi Hicho, MBWANA MOHAMED Maarufu kama MB DOG,
amefichua hili ambalo tulikuwa hatulifahamu Kutoka kwake.
Swahiba Huyo ambaye alifanya vema sana Kupitia
Mikwaju kadhaa kama vile LATIFA, INAMAANA, na Nyinginezo Kibao, amedai kuwa
aliwahi kulipwa Kiasi cha Shilingi MILIONI 10 alipokuwa akipiga Show Moja
katika Nchi ya Burundi
Tofauti na kulipwa Mkwanja Huo, MB DOG aliongeza
kuwa, amewahi kulipwa Shows za Milioni Kadhaa, ingawa Wengi walikuwa hawafahamu
kwasababu kipindi hicho hakukuwa na tabia ya Kutaja Viwango vya Fedha ambavyo
Vinalipwa kutokana na Show, tofauti na Ilivyo hivi sasa, Kila Kitu kiko wazi.
Pia MB DOG ambaye ni Ex Memba wa Kundi la TIP
TOP CONNECTION, ameongeza kuwa Show yake ya Kwanza alilipwa Kiasi cha Shilingi
Milioni 3, huku Show ya Mwisho Ikiwa ni Milioni 10 za Kitanzania mnamo Mwaka
2006, ambayo ilikuwa ni maajabu kwake.
Lakini Mpaka Hivi sasa, Swali ambalo MB DOG
anajiuliza, je Ni kweli anaweza Kupiga Show Yenye Mzuka na Watu Wengi huku
akiingiza Mkwanja Mkali kama Kipindicho?
DEEY CLASSIC NA PROJECT NYINGINE IN TOWN
Mwanza News
DEEY
CLASSIC ana jina Lake Kubwa Tu hapa Bongo baada ya Kuzalisha (Producing)
Mikwaju kadha wa kadha ikiwemo DEAR GOD ya KALA JEREMIAH, na Nyinginezo Kibao
kama JANA NA LEO ya YOUNG KILLA akiwa na STAMINA & QUICK RACKA
Apart From Music ambao ndio Sehemu kubwa ya
Kipaji Chake, DEEY Mwenye makazi yake ROCK CITY Mwanza, akisukuma Beats na Voices
katika Studio kali za REVOLUTION Sound, hivi sasa yuko na “Mkato” huu kwa ajili
ya Friends Wote ambao wanahitaji Kung’aa.
Ziko Available kwa Bei ambayo Inakidhi Kiwango
Chako..
MCHEKI Kupitia 0653 252 526 & 0752 420 903
Subscribe to:
Posts (Atom)











