WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
HATIMAYE JAGUAR AMUANIKA PACHA WAKE
Wengi
Tunaamini kuwa Huenda long time sana, jamaa huyu alikuwa ana ndoto ya kuwa na
pacha wake karibu na hata Kumpata kwa ajili ya usaidizi wa Mishe Kibwena
Mkali
wa KIPEPEO, Jaguar Kutoka Nchini Kenya, hatimaye amamuonesha hadharani pacha
Wake ambayo ni Gari kali aina ya JAGUAR XJ SERIES.
Tukio
hilo lilifanyika katika Moja ya tamasha la Mtandao wa simu nchini Kenya, katika
Kiwanja cha kasarani, ambapo jaguar alionekana akiingia na gari lake hilo lenye
Jina kama lake, na ambalo amekuwa akiliita Pacha wake Mara kadhaa,
Kwa
mujibu wa Wataalamu wa Magari nchini humo, inasemekana kuwa Gari hilo ambalo
lilimgharimu zaidi ya Shillinigi Milioni 10 za Kenya, na ni toleo jipya kabisa
la Mwaka 2013.
Baada
ya Tukio Hilo, jaguar aliipost Picha Hiyo ya gari lake katika Ukurasa wake wa
facebook, huku Waliohuduhuria tamasha Hilo, wakimsifia jaguar hasa kwa kuingia
Vema katika Uwanja huo, huku akishangiliwa na watu Kibao
D’BANJ NA GENEVIEVE NNANJI…..KUNANI?
People fall In Love, lakini D’Banj
aliwahi kukiri kuwa alikuwa amefall In Love na Genevieve, licha ya Kutengana
kwao, bado hatosahau mahaba yake.
Ladies And Gentlemen….
The International Supper Star
akiwakilisha Niger, D’Banji, MR KOKO MASTER Himself, alionekana akiwa na
aliyekuwa Mpenzi wake, GENEVIEVE NNANJI ambaye Pia ni Star Wa Nollywood Movies
Wawili hao walioneakana wakiwa
wenyefuraha na Kukaa beneti kabisa siku za hivi karibuni, katika Club Moja hivi
inayofahamika kwa jina la GULDER CLUB ULTIMATE PARTY, iliyoko katika kisiwa cha
VICTORIA huko Jijini Lagos
Mchoro mzima Ulianza kuchorwa pale
Mtu mzima D’Banj alipoingia katika Eneo hilo akiwa ndani ya ndinga yake kali ya
gharama, aina ya BENTLEY akiwa kanyuka Black and White, na Kisha baada ya
dakika kadhaa, GENEVIEVE naye alitia Timu akiwa na Ndinga yake aina G-WAGON.
Kwa Mujibu wa Pics ambazo
tumezinyaka Pia, zinawaonesha wawili hao waliowahi kupeana maraha na mahaba
makali ya Kubiringika huku na Kule, Katika Kipindi cha Nyuma, ni pale walipokaa
katika Sofa Moja, huku wakionekana Kunong’onezana mawili matatu mara kadhaa, na
hata Kufurahi pamoja.
JAY SEAN APATA AINGIA KATIKA JUKUMU LINGINE
The R&B Singer na Memba wa YOUNG MONEY CASH
MONEY BROTHER, Jay Sean, na Mkewe, Finally wamepata Mtoto wa kike na kuongeza
familia
Wakionekana wenye Furaha za kumwaga, wawili hao
walipost Picha kadhaa kwenye Mitandao ya kijamii kuthibitisha kuwa Familia yao
imeongezeka na Kuwa na kababy Girl waliokapatia Jina la AYYA LOVEEN KAUR JHOOT.
Katika Kudhihirisha furaha hiyo, Jay Sean ambaye
alifanya Vema na Track ya RIDE miaka 6 iliyopita, alipost kupitia Instagram
akisema kuwa, YUUUUP!..I AM A DADY”
Inaaminika kuwa, ongezeko la familia Hiyo,
linaweza kuboresha zaidi ndoa ya wawili hao wapendanao, yaani JAY SEAN na Mkewe
THARA NATALIE
Congratulations
KUNA KITU HIKI AMBACHO KINAMSUMBUA SANA 50 CENTS……
Mkali
wa Rap Nchini marekani The black gorilla, Jackson Curtis “50 Cents”, finaly
ameweka bayana kinachomnyima raha mpaka hivi sasa.
Kwa
mujibu wa maelezo yake, 50 alikiri kuwa moja kati ya Vitu vinavyomsumbua akili,
ni Track yake ya IN DA CLUB, ambayo amekuwa akijitahidi kuikwepa na hata
kutokutamani kuisikiliza kwa namna moja ama nyingine.
FIF
aliongeza kuwa, Ni kweli Track hiyo ilikuwa ni kivutio cha masikio ya Kila mtu
na mpaka hivi sasa ikigongwa sehemu yoyote, bado inakubalika,jambo ambalo huwa
linamtesa kwa namna moja ama nyingine.
Sababu
kubwa za kusumbuliwa na Track hiyo ambayo ilitoka rasmi mnamo mwaka 2003 katika
Albam ya GET RICH OR DIE TRYING, ni kwamba tangia amefanya Kwaju hilo, hajawahi
kutengeneza tena Wimbo wowote ambao utafikia Level ya In Da Club.
Licha
ya Kurudi mara kadhaa katika game, Fifty anakiri kabisa kuwa mara nyingi Wimbo
huoUmekuwa ukimpa mawazo sana, na hata kumuumiza akili, hasa akitizama namna
ambavyo anaweza kufunika kwaju hilo
PICHA 5 ZA MAZISHI YA MAREHEMU PAUL WALKER
HATIMAYE DECEMBER 14, Mwili wa Marehemu
PAUL WALKER, Star wa FAST & FURIOUS, amepumzishwa Kwa amani katika Nyumba
yake ya Milele.
Mazishi
yalifanyika Katika Eneo la FOREST LAWN MEMORIAL PARK, Huko Hollywood Hills,
marekani.
Watu wachache
Hasa familia na marafiki, Ndio waliopata nafasi ya Kuhudhuria mazishi hayo.
Kuna
Uwezekano Mkubwa Kwamba, Mdogo Wake Paul Wallker, CODY WALKER akachukua Nafasi
ya Marehemu kaka Yake (Paul) Katika Filamu Ya FAST & FURIOUS 7
AFUNGIWA KATIKA CHUMBA CHA CHUMA NA WAZAZI WAKE KWA ZAIDI YA MIAKA 40
KIJANA
Mmoja Nchini China PENG WEIQING (48,)
amefungiwa katika Kibox cha Chuma (CAGE) kwa zaidi ya Miaka 40, na mama yake
Mzazi.
Kwa
mujibu wa taarifa za uhakika Ni Kwamba, Mama Huyo ambaye ni Mkazi wa ZHENGZHOU,
Mji Mkuu wa China, amemfungia Mwanae Huyo katika Kibox hicho cha Chuma tangia
akiwa na Umri wa Miaka 6 mpaka anafikisha umri Huo Mkubwa, baada ya kugundulika
kuwa anatatizo la Akili
Pia
mama Huyo ambaye anafahamika kwa Jina la PENG WAIMEI, amesema kuwa alichukua
hatua hiyop, ili kumlinda Mtoto wake pamoja na afya yake, huku akiwa na Hofu
kuwa Huwenda akajidhuru yeyue Mwenyewe, pamoja na kudhuriwa na watu mbali mbali
hasa akiwa Nje.
WAIMEI
aliongeza kuwa, baba Mzazi wa Mtotop huyo, Ndiye aliyejenga Kibanda Hicho,
baada ya kubaini kuwa motto wao hawezi kujihimili yeye kama yeye na hata
Kutulia, hivyo walihisi huenda akajidhuru hata Kwa Kisu wakati hawapo, ama wako
mbali naye
Mama
Huyo alimalizioa kwa kusema kuwa, inaweza kuwa Ngumu kwa Mtoto wake huyo
kuelewa dhumuni la wao kufanya hivyo, na Hivi sasa ana Umri wa Miaka 80, na
mumewe tayari alishafariki. Ila wasi wasi wake ni kuhusu maisha ya Baadye ya
Mwanae huyo, hasa pale nay eye atakapofariki, lakini anaamini atapatikana mtu
wa Kumjali
TIZAMA PICHA ZAKE
TIZAMA PICHA ZAKE
Subscribe to:
Posts (Atom)



















































