REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PIMENI KAULI ZENU NA VITENDO VYENU- JK AWAAMBIA VIONGOZI WA DINI NA SIASA

11:07:00 PM Add Comment

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi wa dini na wanasiasa kupima kauli na vitendo vyao ili kuepusha kuligawa taifa kwa misingi ya imani za dini na itikadi za siasa, kama ilivyotaka kujitokeza mwaka 2012.

Katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa Taifa juzi, Rais Kikwete alisema kwa mara ya kwanza mwaka  2012, Tanzania ilifikishwa kwenye hatari ya kutokea mgawanyiko wa Watanzania au hata mapigano kwa misingi ya dini zao.

“Nimeshalisemea jambo hili siku za nyuma na napenda kurudia leo kuwasihi Watanzania wenzangu kupima athari za kauli zetu na matendo yetu kwa mustakabali wa jamii yetu, nchi yetu na watu wake,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Viongozi wa dini, waumini na viongozi wa siasa na wafuasi wao wanao wajibu maalumu wa kuhakikisha kuwa Watanzania wanaendelea kuishi kwa upendo, amani na ushirikiano bila kujali tofauti ya dini zao, makabila yao, rangi zao au maeneo watokako.”

Ingawa Rais Kikwete hakutaja mambo yaliyotaka kuligawa taifa mwaka jana, mwaka huo ulikumbwa na matukio kadhaa yaliyohusishwa na imani za kidini ikiwamo uchomaji wa makanisa katika Miji ya Zanzibar na Dar es Salaam.

Matukio mengine ambayo baadhi ya watu waliyahusisha na imani za dini ni vurugu zilizofanywa na wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Kikundi cha Waislamu wa Taasisi za Jumuiya ya Kiislamu Tanzania ambazo ni pamoja na kuvamia Ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Dar es Salaam na uvamizi wa maeneo ya wazi eneo la Temeke. Hata hivyo, watu kadhaa walikamatwa na kufunguliwa mashtaka katika mahakama mbalimbali nchini kwa tuhuma za ama kushiriki au kuongoza vurugu hizo.

EWURA YASHUSHA BEI YA PETROL NA DIESEL

11:03:00 PM Add Comment

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinayoonyesha kuwa petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.

“Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya taa Sh1,973. Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa Sh2,057.

Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122.
Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita.

“Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia 6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema.

Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na soko.

“Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,” alisema Masebu.

Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo kikomo.

Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema.

Masebu aliwashauri wanunuzi kuchukua stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita ili itumike baadaye kama kidhibiti endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

CHANZO : MWANANCHI

CONFIRMED :SAJUKI AMETUTOKA

10:37:00 PM Add Comment
 Marehemu Sajuki alipokuwa akipata Matibabu Nchini India

 Marehemu Sajuki (kushoto) alipokuja kutembelewa na Wasanii wenzake. Katikati ni Mkewe Wastara Juma

 Marehemu Sajuki akiwa amembeba Mtoto Wao

Marehemu Sajuki akiwa na Mke wake Wastara Juma

Aliyekuwa Msanii maarufu katika Tasnia ya Filamu nchini Juma Kilowoko almaarufu kama  ’SAJUKI’ ambaye amekuwqa akisumbuliwa na maradhi ya muda mrefu, amefariki Dunia  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taarifa hizo za Msiba wa Marehemu Sajuki, zimetufikia Rasmi asubuhi hii Majira ya Saa Moja.
Sajuki amekuwa akisumbuliwa na Uvimbe Tumboni kwake, kwa Muda wa miaka Miwili Sasa. Hali hiyo ilimfanya kupelekwa katika Nchi ya India kwa ajili ya Matibabu zaidi, hali ambayo ilimpatia ahueni na Kurudi Nchini Tanzania, kabla Mauti hayajamkuta.
Aidha taarifa za Kuzidiwa kwa Sajuki, zilitolewa mnamo December 2012, baada ya hali yake kuwa Mbaya kwa mara nyingine tena, na hakupata ahueni mpaka Umaiti unamkuta

Joachimjunior inaungana na Familia ya Marehemu Sajuki, katika Msiba huu Mzito, ulioikumbva Tasnia ya Filamu Nchini Tanzania.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu SAJUKI, maqhali Pema peponi , Amina.

TUTAENDELEA KUKULETEA TAARIFA ZAIDI ZA MSIBA WA MPENDWA WETU SAJUKI. ENDELEA KUWA NASI

HAPPY NEW YEAR

9:54:00 AM Add Comment
BLACK TOUCHEZ (www.joachimjunior.blogspot.com) inakutakia Heri ya Mwaka Mpya wa 2013
Tunawapenda Sana na Endeleeni kuitembelea Blog hii kwa Mengi zaidi

LENZI YA MWAKA NCHINI UGANDA (KATIKA BURUDANI)

8:36:00 AM Add Comment
 Mapacha Wa P. SQUARE (Peter and Paul) Mwezi huu wa 12 (DECEMBER) walidondosha Bonge Moja La SHOW kwa Wala Bata wa Uganda,. Kwa Mujibu wa Wala Bata wa Uganda, SHOW hii ilikuwa ni Kubwa sana na Ilichangamka Sana kuliko vile ambavyo watu walitarajia. 
Kwa Mujibu wa Mwandishi wa Habari wa BLOG HII, NAHCEEB ABOUD ambaye alikuwa katika Tamasha Hilo Nchini UGANDA, anasema kuwa lilikuwa ni Tamashja Zuri la Kufunga Mwaka, ambalo kamwe halitosahaulika kwa Wakazi wa Uganda.

 P. SQUARE wakiwajibika kama akawaida

 Kama Unavyowaona

 Dk. Jose Chameleon alikuwepo kama Kawaida


Wadau walishindwa kabisa Kuzuia Mizuka yani
 
 Huyu Mwanadada alinaswa na LENZI YA MLA BATA akiwa anaongea na Simu...Mitandao Mingi Nchini Uganda walimtafsiri vibaya sana Mwanadada huyu kuwa alikuwa amezima

 VAMPINO (VAMPOS) alishusha Libeneke Haswa

 Watu hawakutaka Kuvikalia Viti Vyao kabisa...........................

 VIP iliweka kando U-VIP Wao na kunyoosha Mikono Juu kama Unavyo waona... Chezea Alingo Wewe?

 Utamwambia nani atulie wakati ana "MIDADI" ya kutosha.....

 Beatiful Lady CINDY hersel alikuwepo kushow love kwa Wadau wa BATA...

VIP ilijaa kama Hivi...na ilikuwa Imesizi kabla P.SQUARE hawajashusha Mzigo wao.....
PICHA NA NAHCEEB ABOUD

SALAMU ZA HERI YA MWAKA MPYA KUTOKA KWA VIONGOZI WETU

8:00:00 AM Add Comment
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk Ali Mohamed Shein,akitoa salamu za kuukaribisha Mwaka mpya wa 2013,kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote kwa ujumla,

Rais Shein amewasihi wananchi kuendela kushirikiana na Serikali yao katika kuendeleza mipando mbali mbali ya maendeleo,na kuwataka kuwa walinzi wa rasilimali pia kuzingatia   taratibu za kisheria, kwa kuwa na elimu bora ya rasilimali hizo.

**********************************************************************************************

 President Yoweri Museveni, of UGANDA

President Yoweri Museveni has congratulated Ugandan upon completing 2012 and wished them a prosperous new 2013.

In his New Year message, the President said: “I greet all of you and congratulate you on finishing 2012 and wish you a prosperous 2013.  I extend condolences to the families who lost their dear ones in the year that is just ended.”

The President noted that the years 2011 and 2012 were full of economic challenges but were also full of economic opportunities for Uganda. 

He attributed the economic challenges partly to global financial crisis in Europe and the USA.

AKILI YANGU ILIVYO FINYU

7:50:00 AM Add Comment
Sisi Ndio Watanzania Bwana ! Hata mfanye hatutobadilika ! Hata Mtupeleke wapi , Hatubadiliki NG'O !!!

Ilianza Kwenye Kusajili LAINI ZA MITANDAO ya Simu zetu za Mkononi. Serikali mkaimba weeeeee...Mkaimba weeeee...Mkaimba weeee...Mkaimba weee...Kila Siku Mkalia weeee...Lakini Wimbo haukuvutia. He, Si ilivyofika Mwisho Tuakajaa sote kwenye vibanda vya Simu?.

Haya, Likaja Suala la VITAMBULISHO Vya Taifa...Mkaimba weeee...Mkaimba weee...Mkaimba weee Mkaimba weee..Mkalia weeee...Lakini Bado wimbo haukuvutia. He ! Si ilivyofika Mwisho tukaanza kugombana na Waandikishaji wa Huduma Hiyo?

Haya Tena....Limekuja suala la DIGITALI. Mkaimba weee...Wapi...Mkaimba weeee...Wapi...Mkaimba weeee Wapi. He, sasa si unatuona tunavyojazana kwenye Maduka ya Vinga'muzi?

Sasa Je, Sisi Ndio Watanzania..Mkandarasi wa Vichwa Vyetu alishafariki Muda Mrefu   

PICHA NA LOYCE AKOTH

CONFIRMED : KIM KARDASHIAN NI "MAMA KIJACHO"

7:33:00 AM Add Comment
Here We Go !!!
Baada ya kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi kuanzia APRIL Mwaka Huu 2012, hatimaye Mwanadada KIM KARDASHIAN amepata Ujauzito ambao utamfanya yeye na Mpenzi wake Rapa Kane West Kuitwa "Papa & Mama"

Habari hizo hivi sasa zimeshasambaa katika Mitandao mbali mbali ya Kijamii huku zikidhirisha rasmi kuwa KARDASHIAN Tayari amenasa Katumbo na Hivi Sasa Ni mama Kijacho. 

FROM MY FACE BOOK WALL

7:24:00 AM Add Comment
 Lutego "Lut B", My Video Production Tuitor during my College Moments at Royal College Of Tanzania (RCT(. He is the employee at  GRM Production. I do Love and appreciate him because he made me my Self in My Talent. Happy New Year of 2013

 Mhhhh.... Frankly Speaking, I was about today when I was Laughing at this Photo Posted by my Friend MASANJA MKANDAMIZAJI..Can you Imagine?....Do you Think this Man can finish all those Stuffs arround Him?...Come on ....

 My Best Frienda Noorjan "Noorah"....She was my fellow Student at My College (RCT) as well as my Hostel Mate in SINZA VATCAN, where we Lived Happily. I real Miss her, and Love Her alot. HAPPY NEW YEAR NOORJAN.

Come on you Little Boy...Will You shut that "Bad smelling"  mouth of Yours?....You are about to kill us buddy. Haha, that's my Home boy Richard "Virus" himself. I dont realy know if he was Hungry, ar awake by that Time. HAPPY NEW YEAR.

Those are some of all i have got on my facebook Wall. Visit me on my facebook Account, www.facebook.com/ Frank Magnus Joachim.

TUKIO LA KUMPIGA RISASI PAROKO LAANZA KUSHUGHULIKWA..WAWILI WAKAMATWA

7:05:00 AM Add Comment
Na Mohammed Dewji
Watu wawili wanashikiliwa na makachero wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumshambulia kwa risasi Padre Ambrose Mkenda wa Parokia ya Mpendae visiwani Zanzibar.


Naibu Mkurugenzi  wa Upelelezi Zanzibar, ACP Yusuf Ilembo, amesema Kunaswa kwa watuhumiwa hao, kumefanikiwa baada ya juzi serikali kutuma makachero kutoka Bara kuungana na wenzao wa Zanzibar kufanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika na shambulio hilo la kinyama.

Padre Mkenda alipigwa risasi na watu wasiojulikana siku ya Krismasi, nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni, akitokea kanisani. Alishambuliwa akiwa ndani ya gari lake na kuanguka.

Ilembo alisema polisi itahakikisha wale wote waliohusika watatiwa nguvu na kukabiliana na mkono wa sheria,  watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sasa kupisha uchunguzi, wanaendelea kuhojiwa na makachero hao visiwani Zanzibar.

Ingawa uchunguzi wa serikali unaendelea, lakini wadadisi wa mambo ya siasa wanalihusisha tukio hilo na uhasama wa kidini.

Tukio la kushambuliwa kwa padre huyo, linafanana na lile la kumwagiwa tindikali kwa Katibu Mkuu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza, hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyeshikiliwa kuhusika na tukio la Mufti kumwagiwa tindikali,  ambalo kwa namna moja au nyingine, limekuwa likihusishwa na mitazamo tofauti ya kisiasa.

 

MNADA BANNER