REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DALA YAWAKA MOTO.

6:52:00 AM Add Comment


Na: Denis Mlowe - Iringa
Zaidi ya abiria 20 wanusurika kufa katika ajali ya gari aina ya daladala inayofanya shughuli za kusafirisha abiria kati ya Mkwawa na Kihesa Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu katika mfumo wa injini.

Ajali hiyo iliyotokea mida ya saa saba mchana ilihusisha daladala aina ya kipanya yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ilitokea katika maeneo ya Mshindo karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Sherry na Kanisa kongwe la Mshindo mkoani hapa.


Shuhuda ya ajali hiyo Anthony Zamilinga amesema kwamba gari hiyo ilikuwa ikitokea maeneo ya Mwangata ilipofika sehemu ya tukio alimwona dereva akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la kupambana na moto uliokuwa ukianza kuwaka na ulipozidi baadhi ya abiria wakaanza kuruka katika gari hiyo na kupiga simu katika kikosi cha zima moto kilichofika haraka eneo la tukio na kuzima katika gari hilo licha ya kuungua na kuteketea kabisa.

Msemaji wa Zimamoto Kaimu Mkuu wa Kituo Sajenti Meja John Zakaria amesema chanzo cha ajali hiyo hitalafu ya umeme iliyotokea katika gari hiyo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa na tabia ya kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika magari yao.

 “kikosi cha zimamoto kinatoa elimu kila mara kuhusu elimu ya kukabiliana na majanga ya moto na kuna namba za simu za dharura ambazo ziko wazi wakati wote lakini wananchi hawana tabia ya kutoa taarifa mapema na ndio maana hasara kama hizi zinajitokeza hivyo hatuwezi kuota kama kuna janga la moto hivyo naomba ushirikiano wa wananchi katika majanga ya moto kama haya” alisema Sajenti Meja Zakaria

Mmiliki wa dala dala hiyo Ayubu Kabigi amesema kwamba amepata hasara ya sh milioni 8 kutokana na ajali hiyo na amewashukuru sana wananchi waliojitokeza kusaidia kuzima gari yake kwani wakati anapigiwa simu alikuwa anajiandaa na safari ya nje ya mkoa.

 “nawashukuru sana wananchi wa maeneo ya mshindo na kikosi cha zimamoto kuwahi kufika mara baada ya kupewa habari kuhusu janga hilo licha ya kwamba gari lilikuwa limewaka moto na kuteketea” alisema Kabigi

USIKOSE..HII NI HAKI YAKO YA MSINGI....FANYA HIVYO SASA..GOOD MORNING

2:32:00 PM Add Comment

HUYU NDIYE ALIYEMALIZA KAZI KABISA.....

12:45:00 PM Add Comment

Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.

Mrembo Catherine Masumbiga jana usiku ameibuka mshindi kwenye shindano la Unique Model lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam. Nafasi ya pili ilikamatwa na Cesilia Michael huku Amina Ayubu akikamata nafasi ya tatu







Washiriki waliongia tano bora.

CHAMBO RABA RABA KUSHUSHA "DOUBLE- DROP"

11:58:00 AM Add Comment


Here we Go !!
Young Disturbing Artist  RABA RABA Himself all the way from ROCK CITY, ameamua kupiga “Double Droping” kunako mwezi wa Kwanza mwakani, yaani 2013, ambapo anatarajia kudondosha Mkwaju wake mpya, utakaotoka katika Audio na Video kwa Wakati Mmoja.

Kupitia Account yake ya Facebook, Mkali huyo wa “raba raba” amemwaga hadharani kuwa amekuwa Kimya kwa Muda Mrefu sasa, so anarudi kwa ujio mpya kupitia Joint hiyo ambayo ataidrop kwa Mpigo na Video Yake. Jamaa mwenyewe kamwagika hivi :

“Sasa kwa kipindi kirefu nilikuwa Kimya. Narudi kwa ujio mpya. Napenda kuwaamba mashabiki zangu hasa pande za kanda ya ziwa, mwezi ujao natambulisha ngoma yangu mpya ambayo naamini mtaelewa nini nafanya. Nashusha mzigo kwenu Audio pamoja na video kwa pamoja. Napenda kuwaambia ni bonge ya ngoma zaidi ya ngoma ya kwanza iliyokuwa inatambulika kwa jina la RabaRaba. Kaeni tayari kwa ujio huu. Nawapenda shabiki zangu.”

MNADA BANNER